Naomba kuelezwa ni nani Mwingine zaidi ya Dkt Tulia na David Kafulila amewahi kurejesha Chenji Serikalini?

Ndugu zangu Watanzania,

Kuna watu ni WAZALENDO kwelikweli,ni wasafi sana, ni waaminifu waliopitiliza,ni wacha Mungu na wenye Hofu ya Mungu sana na wana uchungu mkubwa Sana na Maisha ya watanzania. Miongoni mwa watu hao basi ni hawa watu wawili ambao wamewahi ishitua Tanzania na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Ngoja niwape story bila kuwachosha kuelekea wikendi. Ilikuwa hivi Mheshimiwa Chuma Mwenyewe David Kafulila akiwa katibu Tawala Mkoa wa Songwe alipewa Billion Sita kujenga mpaka kumaliza ujenzi wa Makao makuu ya mkoa wa Songwe yanayopatikana katika kata ya Mlowo Eneo la Nselewa. Lakini Chuma kwa kutumia mfumo wa Force Akaunti katika ujenzi wa Makao makuu hiyo hakumaliza pesa hiyo.

Ambapo mpaka jengo linamalizika na kukamilika Chuma Kafulila akabakisha Chenji ya Karibu Billion Mbili.Siku hiyo anasoma taarifa hiyo mbele ya waziri mkuu mwaka 2020 Ofisi za makao makuu ya mkoa ,watu wote walibaki Midomo wazo na kustaajabu Uzalendo alio uonyesha CHuma Kafulila. Nakumbuka siku hiyo alisoma taarifa hiyo kwa umakini na utulivu wa hali ya juu sana. Na kwa bahati nzuri mimi mwenyewe nilikuwepo siku hiyo na nilikuwa karibu sana eneo la Tukio na nilikuwa nimesimama jirani na Mheshimiwa David Silinde ambaye siku hiyo alipewa nafasi ya kuzungumza pia. Nilikuwa jirani maana nilikuwa ni kiongozi wakati huo kwenye jumuiya ya vijana yaani UVCCM.

Siku hiyo nakumbuka wakati tunarejea majumbani Chuma Kafulila alikuwa ni gumzo sana tena sana midomoni mwa watu ,kwa namna alivyo onyesha uzalendo wa kipekee na uaminifu wa kiwango cha juu sana.

Mwingine ni Dada wa Taifa na Rais wa IPU na msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini.huyu sina sababu ya kueleza mengi maana mnakumbuka Billion kadhaa alizorejesha serikalini baada ya kubana matumizi kule Bungeni.

Nimeamua niandike haya kueleza kuwa kuna watu ni waaminifu na wazalendo sana,ambao miongoni mwao ni hawa niliowataja hapa.

Jiulizeni ndugu zangu watanzania ni mara ngapi mmesikia kuwa mradi fulani Umepelekewa mamillioni kwa mamillioni ya pesa, lakini pesa zimekwisha na mradi haujafika hata nusu na hela haieleweki iliko kwenda? Mara ngapi mmesikia miradi kama vile ujenzi wa shule au kituo cha afya au barabara au usambazaji wa maji unakatu umekwama kukamilika kwa kuwa tu mapesa yaliyotolewa yameliwa na kuisha kabla hata mradi haujafika hata Nusu yake? Hamjaona haya wanapofanya ziara mawaziri wetu huko mikoani wakisikitika mpaka wanatamani kulia baada ya kukuta pesa zimeliwa? Hamjaona waziri mkuu wetu akiongea kwa uchungu na kwa huzuni na kuagiza ukaguzi na uchunguzi ufanyike kubaini waliotafuna pesa?

Lakini vyuma hivi Mheshimiwa Dkt Tulia pamoja na David Kafulila vilirejesha Chenji ya mamilioni kwa mamilioni,pesa ambazo wangeamua kuzichepusha kutunisha akaunti zao benki. Lakini kwa uzalendo wao wakasema hapana acha turejeshe pesa hizi ili zikajenge vituo vya afya ,shule, usambazaji wa maji safi na salama,umeme, barabara n.k.

Mwisho niseme tu kuwa mimi ni mzalendo na nimekuwa na tabia ya kutetea na kuwasemea wazalendo wote. Mimi sioni haya wala aibu kumtetea na kumsemea mzalendo bure kabisa pasipo malipo ya aina yoyote ile wala kupewa hata mia tano tu ya Vocha. Nataka Taifa liwe na utamaduni wa kuwaunga mkono wazalendo na wachapakazi wa Taifa letu ,tusiache wakachafuliwa na kushambuliwa na wabaya .ndio maana kuna watu awali wakasema mara nalipwa kwa uchawa ,wengine wakasema nalipwa na Mheshimiwa Dkt Tulia,wengine wakasema Nalipwa na Mwamba Mwenyewe Paul Makonda na sasa wengine wanasema nalipwa na Chuma Kafulila.ila hawasemi nalipwa shilingi ngapi na kwanini nilipwe na kila mtu na na kwa watu wote hao? Na hawasemi kwamba wao wanalipwa na nani kuchafua watu humu jukwaani na mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kigezo cha uzalendo ni kurudisha pesa tu? Hakukuwa na shida nyingine ofisini kwao ambayo wangeitatua Kwa kutumia bakaa hiyo mfano madeni ya wazabuni na watumishi, vitendea kazi na mengineyo?
 
Hoja hapa ni kubana matumizi kubadilisha matumizi baada ya bakaa ni jambo jingine nadhani ndio hoja ya muhusika
 
Wewe ni shabiki wa Chama Cha waganga njaa , Chadema
Kumbe ni hivyo tu.Mimi nikadhani unataka nishabikie walafi,wezi,majangiri,wauzaji wa vyombo vya ndani vya kupikia,wenye kulea majumbani mwao mashoga na wasagaji,wavivu wa kufikiri,wapeanao madaraka kihuni na wajingawajinga.?
 
Huko Sasa ni zaidi maana Mataputapu tuu mnakutana mapanga ,mkiona pesa za Umma itakuaje? 😂😂
 
Utakufaa tu na wivu wako
Sasa ukimuonea wivu mtu badala ya kujitafuta unakuwa unawaza vizuri kweli?Haiwezekani mkaleta agenda za upigaji debe JF kienyeji na muda haujaruhusu.Mnawaharibia.Kamati ya maadili ikiwatandika viboko watu wenu msijinunishe.Subirini.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna watu ni WAZALENDO kwelikweli,ni wasafi sana, ni waaminifu waliopitiliza,ni wacha Mungu na wenye Hofu ya Mungu sana na wana uchungu mkubwa Sana na Maisha ya watanzania. Miongoni mwa watu hao basi ni hawa watu wawili ambao wamewahi ishitua Tanzania na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Ngoja niwape story bila kuwachosha kuelekea wikendi. Ilikuwa hivi Mheshimiwa Chuma Mwenyewe David Kafulila akiwa katibu Tawala Mkoa wa Songwe alipewa Billion Sita kujenga mpaka kumaliza ujenzi wa Makao makuu ya mkoa wa Songwe yanayopatikana katika kata ya Mlowo Eneo la Nselewa. Lakini Chuma kwa kutumia mfumo wa Force Akaunti katika ujenzi wa Makao makuu hiyo hakumaliza pesa hiyo.

Ambapo mpaka jengo linamalizika na kukamilika Chuma Kafulila akabakisha Chenji ya Karibu Billion Mbili.Siku hiyo anasoma taarifa hiyo mbele ya waziri mkuu mwaka 2020 Ofisi za makao makuu ya mkoa ,watu wote walibaki Midomo wazo na kustaajabu Uzalendo alio uonyesha CHuma Kafulila. Nakumbuka siku hiyo alisoma taarifa hiyo kwa umakini na utulivu wa hali ya juu sana. Na kwa bahati nzuri mimi mwenyewe nilikuwepo siku hiyo na nilikuwa karibu sana eneo la Tukio na nilikuwa nimesimama jirani na Mheshimiwa David Silinde ambaye siku hiyo alipewa nafasi ya kuzungumza pia. Nilikuwa jirani maana nilikuwa ni kiongozi wakati huo kwenye jumuiya ya vijana yaani UVCCM.

Siku hiyo nakumbuka wakati tunarejea majumbani Chuma Kafulila alikuwa ni gumzo sana tena sana midomoni mwa watu ,kwa namna alivyo onyesha uzalendo wa kipekee na uaminifu wa kiwango cha juu sana.

Mwingine ni Dada wa Taifa na Rais wa IPU na msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini.huyu sina sababu ya kueleza mengi maana mnakumbuka Billion kadhaa alizorejesha serikalini baada ya kubana matumizi kule Bungeni.

Nimeamua niandike haya kueleza kuwa kuna watu ni waaminifu na wazalendo sana,ambao miongoni mwao ni hawa niliowataja hapa.

Jiulizeni ndugu zangu watanzania ni mara ngapi mmesikia kuwa mradi fulani Umepelekewa mamillioni kwa mamillioni ya pesa, lakini pesa zimekwisha na mradi haujafika hata nusu na hela haieleweki iliko kwenda? Mara ngapi mmesikia miradi kama vile ujenzi wa shule au kituo cha afya au barabara au usambazaji wa maji unakatu umekwama kukamilika kwa kuwa tu mapesa yaliyotolewa yameliwa na kuisha kabla hata mradi haujafika hata Nusu yake? Hamjaona haya wanapofanya ziara mawaziri wetu huko mikoani wakisikitika mpaka wanatamani kulia baada ya kukuta pesa zimeliwa? Hamjaona waziri mkuu wetu akiongea kwa uchungu na kwa huzuni na kuagiza ukaguzi na uchunguzi ufanyike kubaini waliotafuna pesa?

Lakini vyuma hivi Mheshimiwa Dkt Tulia pamoja na David Kafulila vilirejesha Chenji ya mamilioni kwa mamilioni,pesa ambazo wangeamua kuzichepusha kutunisha akaunti zao benki. Lakini kwa uzalendo wao wakasema hapana acha turejeshe pesa hizi ili zikajenge vituo vya afya ,shule, usambazaji wa maji safi na salama,umeme, barabara n.k.

Mwisho niseme tu kuwa mimi ni mzalendo na nimekuwa na tabia ya kutetea na kuwasemea wazalendo wote. Mimi sioni haya wala aibu kumtetea na kumsemea mzalendo bure kabisa pasipo malipo ya aina yoyote ile wala kupewa hata mia tano tu ya Vocha. Nataka Taifa liwe na utamaduni wa kuwaunga mkono wazalendo na wachapakazi wa Taifa letu ,tusiache wakachafuliwa na kushambuliwa na wabaya .ndio maana kuna watu awali wakasema mara nalipwa kwa uchawa ,wengine wakasema nalipwa na Mheshimiwa Dkt Tulia,wengine wakasema Nalipwa na Mwamba Mwenyewe Paul Makonda na sasa wengine wanasema nalipwa na Chuma Kafulila.ila hawasemi nalipwa shilingi ngapi na kwanini nilipwe na kila mtu na na kwa watu wote hao? Na hawasemi kwamba wao wanalipwa na nani kuchafua watu humu jukwaani na mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kurudisha chenji serikalini si kigezo cha uadilifu.

Mkapa alisharudisha chenji sana serikali za urais wa Nyerere na Mwinyi, akapewa nchi, akaiba mara nyingi ya akizorudisha kwenye EPA na ma deal mengine.
 
Mkapa aliiba nini? Be serious aisee
 
Kuna kurudisha Kwa sababu pesa imevuka mwaka na miradi haikutekelzwa ipasavyo.

Hoja ni mradi umekwisha na chenji imebakia.

Jerry na Bashungwa walikataa Rushwa za mabilioni

Kurudisha chenji serikalini si kigezo cha uadilifu.

Mkapa alisharudisha chenji sana serikali za urais wa Nyerere na Mwinyi, akapewa nchi, akaiba mara nyingi ya akizorudisha kwenye EPA na ma deal mengine.
Futa hi kauli plz
 
Uzalendo ufundishwe Mashuleni yaani watu wanamlaani mtu kurudisha chenji aiseeee my country😭😭
Hapo ndipo unapoweza kuona laana ya watanzania.badala ya kumtia moyo wao wanaona wivu . Ndio maana wezi na mafisadi wanapata kiburi cha kuiba sana pesa za umma maana wanajuwa watatetewa sana na watanzania hao hao walioibiwa kodi zao
 
Back
Top Bottom