Naomba kufahamu Madhara ya kupeana talaka baada ya ndoa Kuvunjika

Madhara ya Talaka ni makubwa Sana hasa Kama Jambo au mgogoro wenu unaweza tatulika kwa mazungumzo ya kupatanishwa.
Tafuta suruhu kabla ya kifikilia talaka, shirikisha wazazi, viongozi wako wa kiroho na marafiki.
 
Sio stress na depression pekee...lazima uwe na tahadhari sana hapo.... Usipokua makini kizazi chako chote kitaanza kuharibika kuanzia hapo.... usiombee kuwa na watoto wenye mama tofauti, labda kama Hauna watoto....
Ni kweli ulichoandika ndio maana hii kitu imekuwa inanisumbua sana kwenye kutafakari kwangu nakubali nimekosea but what the steps to take-off niepukane na madhara yote mbeleni.. its too hectic na huku nchi tulizopo kufa kwa stress ni kawaida sana
 
Ni kweli ulichoandika ndio maana hii kitu imekuwa inanisumbua sana kwenye kutafakari kwangu nakubali nimekosea but what the steps to take-off niepukane na madhara yote mbeleni.. its too hectic na huku nchi tulizopo kufa kwa stress ni kawaida sana
Fungua macho yako angalia mbele
 
Kama ww ni mkristo mambo ya talaka ya nn tena jaman, si mpk kifo kiwatenganishe.
 
Madhara ya Talaka ni makubwa Sana hasa Kama Jambo au mgogoro wenu unaweza tatulika kwa mazungumzo ya kupatanishwa.
Tafuta suruhu kabla ya kifikilia talaka, shirikisha wazazi, viongozi wako wa kiroho na marafiki.
Asante kwa ushauri mtu wangu.. appreciated 🙏
 
Usijaribu kumwambia hata kwenye uzi wako kule watu walikushauri, hiyo kitu inakutesa kwa sasa kwa sababu ni mwanzo ila hauna miezi miwili utazoea na tena huyo dem akishajifungua ndo kabisa wala haitakuumiza, huyo mtoto alieko Finland utamtambulisha kwa ndugu au rafiki yako unayemuamini incase of danger yoyote inayoweza kutokea kama kifo na awe anawasiliana nae, wewe as long as mfini anajua una familia atakua anajua jinsi ya kulea mtoto wako na wewe ukienda kumuona mara moja moja ukipita hiyo mitaa, kwa ulivomzungumzia mkeo na wewe pia unaonekana hauna wasiwasi kuvunjika ndoa ila usijaribu hicho kitu, hili jambo uje kumwambia mkeo baada ya yule mtoto akishakua na miaka kumi and above kama unaona unataka sana kumwambia kwa sababu pia hata ukimwambia usidhani huyo mfini kuna siku atakupa mtoto ukae nae labda likizo tu.
Ukimwambia mtoto akiwa ameshakua mkubwa itakua worse zaidi ila ni nafuu kwa sababu hata umri wa mkeo utakua umeshaenda hivyo sio rahisi kukuacha.

Happy Sunday.
Cc. TATA MKURIA

Nje ya mada, Mkuu naomba connection ya kazi huko naona unasafiri nchi mbalimbali.
 
Kama ww ni mkristo mambo ya talaka ya nn tena jaman, si mpk kifo kiwatenganishe.
Ni kweli lakini character ya mke wangu haitaniacha salama inahitaji akili nyingi kuepuka hiki kikombe cha talaka sipendi kinikute ndio maana najaribu kupata mawazo tofauti ili niweze kupata njia nzuri zaidi ya kuepuka talaka but akilazimisha kudai itanibidi nilibebe though sijui madhara yake yatakuwaje kiroho na kisaikolojia.. jambo hili ndio linanisumbua kwasasa...
 
Ushaur mzur sana huu
 
Unaonekana you are ready kabisa kuachana na mke wako.
Yaani you've made up your mind kwamba hata akidai talaka sawa tu. Maana ake humtaki tena.

Kama bado wamtaka kwann umwambie sasa wkt mwenyew unasema unamjua mke wako atadai tu talaka... meza. Kama ulivokaa nalo siku zote mpk saiz endelea kukaa nalo ivo ivo.
Otherwise mwambie, achananeni, talaka haitakuletea effects yyt.
 
Changamoto niliyonayo ni kwamba nahisi hatia ndani mno na njia pekee ya kuwa na amani ni mpaka nimwambie mke wangu huu ukweli sasa kadri nnavyoendelea kukaa nalo nakosa amani najikuta nimebeba jambo zito mno na sijui sababu nini maana kuna mengi sijamwambia na yamebaki kuwa siri ila hili la mtoto nje ya ndoa nashindwa kulibeba linanisumbua sana ila sasa nikimwambia tu kuna hatari nyingi zinaweza kutokea nafikiri japo sikuwahi kupitia such experience ya kupeana talaka
 
Usiseme bora ahic tu mwenyewe mkuu
 
Mtagawana mali mlizochuma wakati wa ndoa yenu (zile ulizokuwanazo kabla ya ndoa hazihusiki)
Kuna possibility kubwa ya wewe kutenganishwa na watoto wako na kuingia gharama za unawahudumia wakiwa mbali.

Mda mwingine tunadanganya au kukaa kimya ili kuepuka reaction inayoweza kujitokeza baada ya ukweli kujulikana
 
Huyo mtoto wa nje ya ndoa na ndoa yako nani ana umri mkubwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…