Hiyo safari igawe siku2 kwa kutembea saa sita sita.
Fanyia service pikipiki, badili oil weka mpya, rekebisha nyororo, kaza kaza nut zote, taa iwake na tube nzima.
Ondoka Dar hadi Moro, lala pumzika.
Kesho yake Moro to Dom.
Ukifika mwisho wa safari mwaga oil.
Asikutishe mtu kama wewe ni dereva mzoefu, tembea 60-80 hadi 100 kmph kutokana na eneo.
Mimi nilikuwa natembea saa6, km300 kwa kutumia rouph road lakini nafika bila tatizo lolote.
Hiyo barabara ya lami wala hautachoka kivile, isipokuwa kama utadunda dunda sana kwenye makorogesheni muda mrefu, makalio mzee, kumbuka zile fimbo ulizokuwa ukitandikwa shule ndivyo yatakavyosoma.
Anzisha safari yako kama saa1 kabla ya muda wa mabasi ya abiria utatembea bila bugudha njiani.
Kama walivyoshauri wengine, spana ni muhimu na pesa ya dharula.
Waweza tembea hadi mwisho wa safari wala usikumbane na kikwazo chochote.
Nikutakie safari njema.