Mkuu
Kaluluma , kama ulivyoelezwa na Mkuu
Tusker Bariiiidi, mimi ni biker.
Kuna bikes za aina tatu,
1. bikes za matumizi ya kawaita, ambazo ni za masafa mafupi, na safari fupifupi sio za safari za masafa marefu. Hizi zina cc. ndogo from 50cc -250cc
2. Kuna bikes za starehe for fun, na michezo ya pikipiki kama racing, zinaitwa Street bikes, na off roads, hizi pia sio pikipiki za safari ndefu. CC. ni kuanzia 250cc hadi 650cc.
3. Kuna pikipiki za safari au za masafa, hizi ni big bikes kuanzia 750cc -1,800cc. Hizi ndio pikipiki za safari au za masafa.
Mimi kwa upande wangu nilikuwa na seti zote 3, hivyo nilikuwa nakwenda kila mahali na bike. Niliwahi kuwa nafanya kazi Morogoro naenda asubuhi na kurudi jioni. Dar Moro kwa big bike ni 90min.
Dar Dodoma ni 4 hrs
Dar Moshi ni 5 hrs.
Kwa vile hizo bikes zako ni ndogo na sio za safari hivyo zipakie kwenye lori zilete.
Japo mimi kwa upande wangu, nimesafiri sana na bikes, lakini baada bike kunifanya kitu mbaya, sishauri kusafiri kwa pikipiki long distance au masafa marefu kwasababu barabara zetu hazina bike lane, hivyo ni hatari sana. Nchi za wenzetu, wana pedestrian lane, cycles lane, bikes lane na njia za magari.
P