Naomba kujua kuhusu safari ya Dar kwenda Dodoma kwa pikipiki

Naomba kujua kuhusu safari ya Dar kwenda Dodoma kwa pikipiki

Kwanza tujue.

1. Dar dom km ngapi
2. Unaenda kwa km ngapi kwa saa
3. Lita inakupeleka km ngapi
4. Je una vifaa vya kujikinga, koti, helmet nk
5. Je una tool box
6. Una pesa ya dharura.

Inawezekana kabisa. Wanaokutisha hata pikipiki hawajui kuendesha. Jipange, inawezekana.
Bodaboda hajui hata moja kwenye hiyo list
 
Dar - Dom ni roughly 450 km

A. Fuel consumption ya TVS/boxer ni 40 - 60 km/l

Zinahitajika lita 10 (roughly) ambayo ni kama 26,000 TZS kwa kila pikipiki.
OIL - 8000 TZS, Achilia mbali gharama za chakula pamoja na risks za safari ndefu kwa pikipiki.

B. Kusafirisha kwa lori Dar - Dom ni around 50,000 TZS kwa pikipiki.

1. Kama ni mzoefu wa safari ndefu na unataka adventure nenda na A

2. Kama ni vinginevyo nenda na B
 
Wengi wanaokushauri huenda hata pikipiki hawajawahi kuendesha, Safari ya Dar Dom ni Safari flani ya kawaida Sana,Tena atakayeendesha TVS 150 ata enjoy zaidi,hapo vituo ni vitatu tu unapiga gia unatoboa Dom,mi nishaendaesha hiyo pikipiki umbali mrefu ilikuwa Dom -Arusha,Arusha-Singida,Dom-Iringa
 
shida si kuendesha tu.si uwezo wa pikipiki peke yake.wewe unaweza kuendesha hicho chombo katika muktadha wa safari ndefu, ya jua pengine na mvua, usiku na mchana? tena kwenye barabara zinazohitaji umakini wa hali juu? kama moyo wako unatone la wasiwasi hata gram mbili pakiza hizo boda kwenye basi au lori bro..
 
Mkuu, kama kufika haraka sio issue kwako, piga gear vyombo hivyo. Adventure.

Utatumia siku 2. Pumzika kila baada ya 2 hours au kila baada ya kilometa 100-150. Pumzika kwa saa moja hivi.

Uzuri izo pikipiki ni famous, kwahiyo kila unavyopumzika unaweza enda sehemu penye mafundi wakacheki upepo na vitu vidogo vidogo.

Ukibadirisha oil huku hauna haja ya kubadirisha hadi Dom.

Mi nishaenda na pikipiki Dar to Mbeya, na ilikua air-cooled, TVS apache 180, na ilikua poa sana.

Utachoka kingese ila iyo safari hautakaa ukaisahau maishani mwako.

Narudia tena, kikubwa usiwe na haraka.
Dar - Mbeya ulipitia Mikumi, Masasi ua Mtera?
 
Kuna mwamba katoka Kigoma kwa mguu anaelekea Kilimanjaro!
Anaenda kwa ishu gani?
Mi kwetu kigoma ila sipendezwi na hii tabia ya kutembea kwa miguu, huyo sasa atakuwa mtu wa tatu kutembea kwa mwaka huu.
Karne ya 21 kutemvea kwa miguu ni aibu kwa nchi, hii inaashiria uchumi duni wa watu.
 
Haihusiani na uchumi mkuu, ni yeye kajitolea kwa uzalendo…. anahamasisha watu wapate chanjo ya uviko.
 
Habari za leo wakuu,

Ninafikiria kati ya njia mbili za kusafiri, aidha kwa pikipiki au kuisafirisha chombo yangu used kwa malori ya mizigo. Kwa wale wenye uzoefu na route hii kwa pikipiki mnaweza kunipa muongozo wa sehemu za kupumzika, kufanya service nikiwa njiani, muda wa safari kwa makadirio na changamoto zilizopo barabara hiyo ya Dar - Dodoma.

Chombo ni mbili moja boxer cc125, na Tvs cc 150 madereva tupo wawili.

Natanguliza shukrani.
Naomba USIJARIBU... Kwa habari zaidi za Onyo langu Muulize Pascal Mayalla wa JF. UTANISHUKURU BAADAYE.
 
Nlishapiga Mwanza - Moro na sanlg 125 Mara mbili ila ukipishana na mabus had upepo unakutoa nje ya barabara kwahyo unatakiwa ukiziona gar kwa mbal unapunguza speed maana ukiwa kas pikpik inakua nyepes unaweza kupoteza uwezo wa kuimiliki.
kama huna uzoefu ndugu zako watakuja kuokota kipande cha mfupa wa goti tu wakazike
 
Kuna uzi upo jamaa alifika tabora kwa siku moja na dom ilikua kituo cha Kwanza kusimama.
 
Habari za leo wakuu,

Ninafikiria kati ya njia mbili za kusafiri, aidha kwa pikipiki au kuisafirisha chombo yangu used kwa malori ya mizigo. Kwa wale wenye uzoefu na route hii kwa pikipiki mnaweza kunipa muongozo wa sehemu za kupumzika, kufanya service nikiwa njiani, muda wa safari kwa makadirio na changamoto zilizopo barabara hiyo ya Dar - Dodoma.

Chombo ni mbili moja boxer cc125, na Tvs cc 150 madereva tupo wawili.

Natanguliza shukrani.
Naomba USIJARIBU... Kwa habari zaidi za Onyo langu Muulize Pascal Mayalla wa JF. UTANISHUKURU BAADAYE.
Mkuu Kaluluma , kama ulivyoelezwa na Mkuu Tusker Bariiiidi, mimi ni biker.

Kuna bikes za aina tatu,
1. bikes za matumizi ya kawaita, ambazo ni za masafa mafupi, na safari fupifupi sio za safari za masafa marefu. Hizi zina cc. ndogo from 50cc -250cc
2. Kuna bikes za starehe for fun, na michezo ya pikipiki kama racing, zinaitwa Street bikes, na off roads, hizi pia sio pikipiki za safari ndefu. CC. ni kuanzia 250cc hadi 650cc.
3. Kuna pikipiki za safari au za masafa, hizi ni big bikes kuanzia 750cc -1,800cc. Hizi ndio pikipiki za safari au za masafa.

Mimi kwa upande wangu nilikuwa na seti zote 3, hivyo nilikuwa nakwenda kila mahali na bike. Niliwahi kuwa nafanya kazi Morogoro naenda asubuhi na kurudi jioni. Dar Moro kwa big bike ni 90min.

Dar Dodoma ni 4 hrs
Dar Moshi ni 5 hrs.

Kwa vile hizo bikes zako ni ndogo na sio za safari hivyo zipakie kwenye lori zilete.

Japo mimi kwa upande wangu, nimesafiri sana na bikes, lakini baada bike kunifanya kitu mbaya, sishauri kusafiri kwa pikipiki long distance au masafa marefu kwasababu barabara zetu hazina bike lane, hivyo ni hatari sana. Nchi za wenzetu, wana pedestrian lane, cycles lane, bikes lane na njia za magari.
P
 
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom