Naomba kujua kuhusu safari ya Dar kwenda Dodoma kwa pikipiki

Shukrani sana mkuu, kwa upembuzi yakinifu
 
Mikumi pe mbugani utapitaje mkuu? Ukikutana na mjomba Cheetah je?
 
Case closed, akileta kichwa ngumu poa...
 
Mambo ya muhimu ni haya yafuatayo kama utaamua kusafiri na pikipiki:

1-Hakikisha unafanya service nzuri kabla ya safari kama vile, kumwaga oil, tyres, brakes, n.k

2-Hakikisha bike ina side mirrors maana ukiwa high way ni ngumu kuona gari ndogo ikiwa inakuja kwa mbali kwa kasi..kuna gari zingine zina rangi ya majani.

3-Hakikisha nyuma unapakia mzigo usipungua kilo 50 kwa ajili ya stabilization ya bike ukiwa kwenye speed kubwa.

4-Hakikisha una boots, vaa jeans, koti kubwa linalofika shingoni.

5-Hakikisha Unatafuta kipande cha box weka kifuani kupunguza makali ya baridi ya upepo..koti pekee halitoshi.

6-Hakikisha helmet yako ina kioo cha mbele kulinda macho na wadudu,michanga na vumbi

7-Hakikisha una scarf shingoni kuzuia upepo unaoponyoka kichwani kuingia mwilini.

8-Hakikisha una akiba kwa ajili ya dharura.

9-Pia tembea na toolkit, waya wa clutch, sparkplug,n.k

10-Jaza mafuta full tank kutoka Dar lita 11 kwa boxer halafu utaenda jazia lita 5 utakapofika GAIRO.

11-Muda wa kuanza safari ni saa 11 alfajiri uwe unatoka mbezi luisi. Hakikisha hanzi safari kwenye mida ya mabasi ya mikoani watakuua haraka tu.

12-Kupumzika si lazima, ila ikikupendeza pumzika morogoro kwa muda wa nusu saa wakati unakunywa chai acha bike ikiwa silencer.

13-Hakikisha unatafuta sponge kwa ajili yakuweka makalioni. Maana kiti cha bike kigumu kiasi. Kama utavumilia ni sawa.

14-Kuwa makini na barabara hususani kwenye miinuko kiasi usikimbie malori huwa yanachimba barabara na kufanya ziwe na mawimbi unaeza tolewa nje ya chaki.

15-Mwendo mzuri kwa afya ya bike za cc ndogo ni 80Kph ukinogewa saaana basi 100Kph lakini utaisikia injini inatetema.

16-Muda wote washa TAA za mbele full ili uweze kuonekana vizuri na vyombo vingine mbele.

17-Kama utakuwa na BEGI basi livae mbele, ukivaa nyuma litakuchosha mgongo kiasi.

18-Kama bike sio mpya basi msikimbize saaana.

19-Msiache kumuomba MUNGU kabla hamjaanza safari yenu.

20-Ukifika mwisho wa safari acha bike kama nusu saa hivi ikiwa silencer halafu ndipo uizime. Usisahau kubadili oil kabla yakuendelea na harakati zingine

NB; Nawatakieni SAFARI NJEMA.
 
Shukrani mkuu
 
Sijui unataka kugundua nini unapotaka kusafiri na pikipiki umbali wote huo.Risk za kutembea na pikipiki umbali huo ni kubwa.Pia unaweza hata ukifika unaumwa hasa mgongo.By any possible means uzisafirishe kuliko kuendesha huo umbali humo njiani unaweza hata kupata msukosuko wa marahamia kutaka kuchukua hizo pikipiki kwa gharama yoyote watu wanaweza hata kuanza kuwafuatilia humo njiani.
 
Shukrani mkuu kwa tahadhari
 
Madereva wawili huo ni uzembe kuna jamaa mmoja atembea haojue toka Mbagala hadi Majengo sokoni Dom siku moja tu
 
WE JAMAA UMEMSHAURI HUYO JAMAA KOTAALAM...HUJAMKATISHA TAMAA USHAURI WAKO UNAWEZA KIMFANYA JAMAA AJUE NJEMA NA MBAYA.....WAZUNGU WANASAFIRI NA HIZO ILA WANAFUATA VIGEZO ULIVYOAINISHA...INGAWA INGEKUWA MIMI NINGEPAKIZA KWENYE MALORI MAANA MAANA WENGI WETU (WABONGO) HATUNA PROTECTIVE GEARS ZA UENDESHAJI ZILIZOTHIBITISHWA KITAALAM...HONGERA UNAONEKANA KUWA NA BUSARA NA HEKIMA....Nimeona nisihangaike na kitufe cha like.
 
Waombolezaji wanasubiria kinuke wajikusanye kwenu
 
muulize Paskali,nae alisafiri na Pikipiki kutoka Dar kwenda DODOMA,bahati mbaya hakufanikiwa kufika DODOMA salama,alipata mzinga katikati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…