Naomba kujua kwanini ukimtolea Mwenyezi Mungu Fungu lake la 10% kutoka katika Mshahara wako huku ukiwa na Furaha nae hukubariki maradufu?

Naomba kujua kwanini ukimtolea Mwenyezi Mungu Fungu lake la 10% kutoka katika Mshahara wako huku ukiwa na Furaha nae hukubariki maradufu?

Asante sana Kwako uliyenipa hii Elimu kwani tokea nianze Kufululiza kuhudhuria Ibada zangu Kanisa Katoliki na Kumtolea Mwenyezi Mungu Fungu lake la Kumi ( 10 ) Maajabu yanayonitokea ya Kimafanikio, Baraka na Neema huwezi kamwe kuyapata kwa Mganga wa Kienyeji au wale Waganga Watatu wa Madhabahuni Kawe, Kimara Temboni na huyu mpya wa Buza kwa Lulenge.

Ukiona kila Mwezi unatoa Fungu la Kumi Kanisani Kwako halafu huoni Mafanikio yoyote yale jua hiyo Hela unaitoa huku ukiwa na Usununu ( Hasira ) Moyoni mwako au Wewe ni Mchanganya Maombi na Mzururaji tukuka wa Kutwa kwa Waganga wa Kienyeji.

Akhsante Mungu kwa BARAKA zako!!!
Mola hadanganyi...

Mkinishukuru nitakuzidishieni (Quran 14:7)
 
157d3ca7737a256e3dac71983df233b6.jpg

Akili timamu ikiwa katika ubora wake
 
Mimi huwa najisikia fulaha (Amani) sana pale naposaidia masikini wenzangu wasio na uwezo wa kutafuta..
 
Mimi huwa najisikia fulaha (Amani) sana pale naposaidia masikini wenzangu wasio na uwezo wa kutafuta..
Hii nayo ni sawa tu na Kumtolea Fungu la Kumi Mwenyezi Mungu, hivyo uko mule mule tu.
 
Muda mwingine huwa nawaza kwa Mungu hamna muongozo. (Hayana muongozo)

Kuna watu wanatoa fungu la Kumi kwa uaminifu bila masononeko lkn bado biashara zao zinakufa
Wengine hawatoi biashara zao zinakua bila kutumia hata ndumba...

Mimi huwa nina moyo wa kumsaidia mtu mwenye shida kumpa mtu 500 sio tatizo kama ninayo... Niligundua muda tu ninapotoa hela na mimi napata hela.

Hayanaga muongozo kila mtu na bahati yake...Muda mwingine Mungu haeleweki😔
Bint haeleweki tena?
 
Ni kweli mkuu upo sahihi. Pia huwa najiulizaga matajiri kama kina Elon Musk ama Aliko Dangote kama wanatoaga fungu la kumi
 
Mafanikio ya ki Mungu yana utaratibu wake, hata biblia imeandika Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu na si Mungu wa machafuko.
Kutoa zaka pekee haitoshi ikiwa Imani yako na moyo wako hauko thabiti kwa Mungu, ukisoma kitabu Cha mwanzo 3:1 na kuendelea unaona sadaka ya Habeli ilikubaliwa na ya Kaini ilikataliwa, Hilo la kwanza lakini pia watu wengi katika maombi yetu hasa pale tunapokuwa na uhitaji juu ya jambo Fulani tunajikuta tunaweka nadhiri lakin tunapofanikiwa tunasahau kuzifuta nadhiri, nakwambia hata uwe muaminifu katika zaka nasadaka bila kuzifuta nadhiri hutoboi rejea kumbukumbu la torati 23: 21-23.
Pia katika biblia wapo wengi walio weka nadhiri Mungu akawafanikisha lakini hawakusahau kuzifuta nadhiri zao na Mungu alizidi kuwastawisha na kuwabariki, soma kitabu Cha Mwanzo 28 Yakobo alipokuwa akiweka nadhiri pindi alipokuwa akimkimbia kaka yake Esau, lakin pia 1 samweli sura ya 3 Hana alipoweka nadhiri mbele za Mungu ndipo akampata Samweli na mwisho wa siku Samweli alitumika Kama ilivyokuwa nadhiri iliyowekwa.
Kiukweli njia za Mungu SI Kama tunavyozichukulia rejea Isaya 55:8...
Unaweza ukawa muaminifu katika utoaji na baraka zake Mungu usizione, kumbuka hata biblia imeandika sadaka yake mtu muovu ni chukizo mbele za Bwana.
Kumbuka hata mali za shetani unaweza ukawa mtoaji mzuri wa kafara lakin ukakosea sharti Moja tu utajiri wote kwisha na unaweza poteza uhai pia rejea kisa Cha Marhem Kanumba.
Kuhitimisha ni kweli Fungu la kumi ni lango la mafanikio na baraka na utajiri wa Ki Mungu, kwa maana fedha na dhahabu ni mali yake Hagai 2:8, ila haitoshi tu kutoa fungu la kumi lazima kuuishi utakatifu na kuzingatia taratibu zote za Ki Mungu kumbukumbu la torati 28: 1-15...
Maarifa ya Mungu ni mapana Sana acha niishie hapa kwa leo, kikubwa jitahidi kupata maarifa sahihi kabla ya kufanya chochote vinginevyo utaishia kusema dini ni utapeli, kumbe ni kukosa maarifa rejea Hosea 4:6.
Mungu akubariki Sana na akupe ufahamu wa kumjua yeye na Kumtumikia.
Muda mwingine huwa nawaza kwa Mungu hamna muongozo. (Hayana muongozo)

Kuna watu wanatoa fungu la Kumi kwa uaminifu bila masononeko lkn bado biashara zao zinakufa
Wengine hawatoi biashara zao zinakua bila kutumia hata ndumba...

Mimi huwa nina moyo wa kumsaidia mtu mwenye shida kumpa mtu 500 sio tatizo kama ninayo... Niligundua muda tu ninapotoa hela na mimi napata hela.

Hayanaga muongozo kila mtu na bahati yake...Muda mwingine Mungu haeleweki
 
Ujue huo ni unyonyaji uliojificha, tangu lini Mungu mwenye uwezo mkubwa kiasi hicho ategemee hivyo vijisenti vyako? Mfalme Constantine wa Rome aliupokea Ukristu ili apige pesa, mpaka leo hii hiyo biashara imeshamiri. Vatican ni taifa tajiri sana duniani. Kama umetoa na ukafanikiwa usitudanganye, unazingatia moyoni kuwa "mafanikio ni siri na siri ni mafanikio " Eti nimefanikiwa kwa kutoa fungu la kumi, Acha hizo! Ni fix iliyokomaa.
 
Back
Top Bottom