Naomba kujuzwa gharama za msingi kwa nyumba ya ghorofa moja

Mtoa mada tunakungoja mana wewe ndio utakuja na hesabu halisi
 


Ghorofa Moja mkuu no way
 

Nimefuatilia hii post kwa umakini mtoa maada Wewe ni mtu na nusu
Barikiwa sana political Engineer 2
 
samahani mleta mada nipo nje ya mada kidogo,mimi ni fundi wa kufunga cctv camera,electric fence,gate motor pamoja na video door bell,kwa mwenye kuhitaji huduma naomba tuwasiliane kwa namba 0622667749 au 0674376787 nipo Dar es Salaam
 
Kwa 17m msingi, hilo ghorofa litaanguka mara baada ya kukamilika. Huyo jamaa aliyesema 50m yawezekana (kwa kutumia Wataalam sio Fundi Maiko). Maana binafsi nilitumia 40m kabla bei ya Nondo haijaongezeka.
 
Mkuu tupe mrejesho umefikia wapi, wapw experience wakuu
 
Kwa 17m msingi, hilo ghorofa litaanguka mara baada ya kukamilika. Huyo jamaa aliyesema 50m yawezekana (kwa kutumia Wataalam sio Fundi Maiko). Maana binafsi nilitumia 40m kabla bei ya Nondo haijaongezeka.
M17 inatosha kulingana na ukubwa wa Hilo ghorofa, ambayo yana chini ya 100sqm huwa inatosha kulingana na gharama za fundi

Kwa hizi za kawaida za kuishi zinazojengwa, hizi za residential hiyo 50m huwa Kuna uongo. Wengi hupenda kuonekana wametumia gharama ili kuongeza value ya kitu chake na yeye kuonekana yupo vizuri.

Ujenzi wa ghorofa upo overrated na watu ndio maana hutaja overprice. Ni gharama, lakini sio kama zinazotajwa na watu. Nimeongea through experience kwa maana naujua uhalisia
 
Bora wewe unaandika uhalisia maana wengine dah ukiwasoma ni mwijaku style
 
Uzi mzuri sana, hongera mtoa mada,
Kuna maswali tumekosa majibu, pia tulipenda kuona picha ya msingi wa 9 M.

Mtoa mada amepotea au ndo alidondokewa na ghorofa goba au lile la kigamboni(jokes)
Mtoa mada hataki kuongea na nyie ambao hamna maghorofa.. 😁 panapo majaaliwa si kitambo kirefu, mimi pia naanza ujenzi wa ghorofa yangu, uzuri ni kwamba site engineer ni mimi mwenyewe, nina degree ya civil engineering, ramani nimekwishachora (both architectural and structural).

Najaribu kufanya material estimation naona kabisa sipo mbali sana na mtoa mada, gharama zangu na zake hazitofautiani sana (zangu zipo juu kidogo).
Column natumia nondo 4 za 16mm
Plinth beam na beam ya floor ya kwanza pia natumia 16mm
Slab na stair nasuka top na bottom kwa 12mm 200c/c.
Stirrups au ringi natumia 8mm.
Msingi ni mrefu kidogo. 900mm

Aina ya nyumba ni victorian gothic.
Nyumba ina 9x9m
Ground floor kuna.
Self contained room 1.
sitting room 1.
Dinning room.
kitchen & store

1st floor kuna.
Master bedroom kubwa tu
Self contained room 1.
library.

Aidha kwa mwenye uhitaji wa ramani ya nyumba au ushauri wa masuala ya ujenzi.
Kindly pm.
Kuna jambo likitimia naanza kutafuta mafundi tufanye kazi.

Nikimaliza ujenzi ntaanza kuongea na wenye maghorofa wenzangu tu kama alivyofanya mtoa mada. 😁(jokes)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…