Naomba kuuliza kwa wote wanaomuamini Yesu

Naomba kuuliza kwa wote wanaomuamini Yesu

ajabu ni kwamba hizi hoja kuna mtu zimemfanya awe muislam kinda kinda na yupo tayari kuzifia akiamini ana hoja zinto.
Wakati fulan uko nyuma nikapata Msala nikatupwa Gwanta siku 14.
ndani ya Sero yetu kulikuwa na sehem ndogo kwa ajili ya ibada ya waislamu nikawa najumuika kama kawaida.
katika kundi ilo la waumini ndani ya sero yetu nikafahamiana na kijana mmoja mwenye mkazo wa imani mbali na kuwa ni mtu pekee aliyekuwa ana hakikisha maji ya kushikia hudhu hayakosekani alikuwa ni mtoa Adhana.
baadae nikagundua anaitwa Charles, na ameslimu miezi kadhaa uko nyuma.
siku moja sikumbuki nini kilituingiza katika mjadala wa uislamu na ukristo.
akaniambia:, kilichofanya nislim mbali na sababu zingine zote ni pale kila nikifungua Biblia kuisoma na kutana na Neno Wagidion WAFANYABIASHARA .anaendelea kusema:, nilikuwa najiuliza, kwanini neno la Mungu lifanyiwe biashara?.
Inamaana hawa Wagidion wamekoswa biashara ya kufanya hadi wafanye biashara ya neno la Mungu!! toka hapo nikajua ukristo na biblia kwa ujumla ni utapeli, nikaamua kuslimu.

kwake Charles concept ya TRINITY haikuwa shida , swala la Yesu kuvaa ama kutovaa kanzu, kusujudu etc vyote hivyo kwake si hoja, hoja kwake ni WAGIDION wafanyabiashara😂😂.

nilimuangalia kwa sekunde kadhaa kwa umakini nikagundua upungufu wa maarifa ndiyo umemtoa katika imani yake ya hawali si wa Gideon, angelijaribu kutafuta maarifa jina wagidion lisingempa shida.
Watu wangu wanaangamia kwa kukoswa MAARIFA*.
kuna makumi out there wanaslimu kwa hoja kama hizi.
Hoja za kuwafanya waslimu ni hizi hizi kama za mleta Mada , kwakuwa hawana maarifa uwaona wahubiri wa hoja hizi kama watu watafiti na makini kumbe ni chenga tupu.
Tukiamua kuulizana humu kwanini wewe ni mkristo au kwanini wewe ni muislamu basi naamini unaweza kushangaa tena kwa sababu ambazo watu watatoa.
 
Watu wanatoka mapovu baada ya kuleta hoja🤣🤣🤣, kimsingi wakristo wapo mbali sana na mafundisho ya biblia,

Dini ambayo ukiwa na hela tu unaanzisha kanisa lako na dhehebu lako unapiga pesa🤣🤣🤣

Halafu wanaweka sanamu la muigizaji kwenye makanisa yao wakiitikadi ni yesu,

Dunia simama nishuke🏃🏃🏃🏃
Dah usiseme mengi kanisa la maombi lilinishirikisha wizi wa spika njaa mbaya ..bora nibaki korelo
 
Sasa ndugu yangu mtoa mada, yesu hawezi kurudi amevaa kanzu. unajua kwann? Akiwa anashuka toka mbinguni ataonekana uchi kwa sisi tulio chini uku 😂😂😂Apa piga geuza lazma agonge suti😂😂
 
utamkuta katika hari gani?kavaa kanzu anaswali au utamkuta kavaa suti anahubiri kwa sauti?hilo ndiyo jibu ninalolitaka,sababu dini zote zinahubiri Yesu ataludi
Mkuu nashukuru kwa elim yako hii pana, nilikuwa sijui kumbe DINI zote zinamsubiria YESU arudii?? Ivi ni yeye yule mnazareth? Je wakati huo YESU anarudi Mtume Muhammad yeye atakuwa wapi? Na je kama atarudi kuhukum au kuhitimisha mwisho wa dunia atakuwa ametumwa na nani?? Ivi msemo ule wa kiswahili usemao akufae kwa dhiki (wakat mgum) ndie rafiki wa kwel una mantiki apa? Naomba kuwasilisha
 
Umechanganya sana mambo,Yesu ataludi kama mwanadamu na kwa sura yake aliyeondoka nayo,sasa kama huwa mnamtafsiri kwa sura za watu wengine wa kuchora,hapo ndipo utakapokuwa mtihani
Sijachanganya hata kidogo nadhani ni mtazamo wako! Kama umedanganywa kwamba Yesu atarudi kifala kama alivyokuja imekula kwako!!!! Jiandae kwa mshangao! Maandiko yameweka wazi hatarudi kimasikini kama alivyokuja awali! Atarudi na nguvu, na utukufu, na mamlaka!! Tulimchezea na tumeendelea kumchezea vya kutosha! Ingia makanisani uone yanayoendelea humo!! Ni kinyaa na ni aibu! Endelea kusubiri uone kama atarudi kama mwanzo!!
 
Kifupi kabisa ni kwamba, Uislamu haujakanilika!
Ni imani pekee Duniani ambayo inategemea imani nyingine ili ikamilike.
Bora hata wabaoabudu Ng'ombe hawahitaji dini nyingine kujikamilisha.

Uislamu haupo bila kujihalalisha kwa Ukristo
 
Yaani huu ubishi wote ni katika ku justify dini ipi ni ya kweli. Hapa ulipo unatoka mpaka mishipa ya shingo kutetea dini ambayo uko hapo sababu tu umezaliwa na wazazi walioko hapo, sio kwamba ume study dini zote ukaamua uifuate ipi.

Uko radhi hata ubague yule asieamini katika unachoamini wewe Kwa kujiona wewe ndio sahihi zaidi yake. Hivi niwaulize wafia dini zote/wote, what if ukija kukuta dini ya mwenzio ndio ilikua sahihi kuliko yako? Or what if dini zote ni Sahihi? Or what if dini zote sio Sahihi? Or what if hizi story za Mungu, Yesu, Mtume Muhammad (SAW), sijui Adam, Mussa ni uzushi tu?

Fanya yaliyo mema hapa duniani, amini unachoamini wewe na waache wengine waamini wanavyoamini wao. Usiwashikie wengine akili zao wala usishikiwe akili na wengine.

Tanzania ni Nchi kubwa yenye mikoa zaidi ya 25. Anaekaa Arusha leo anafurahia maisha kuliko ukamuhamisha akakae Songea. Vivyo hivyo aliezoea kukaa Songea anafurahia maisha kuliko ukamuhamisha akakae Arusha. Huwezi kusema mmoja yuko sawa kuliko mwengine. Mtu akikuambia Uislam/Ukristo ndio dini ya kweli kuliko ingine mjibu tu poa.
 
Ukiachana na mambo ya kimwili (kuvaa, kula, kutembea nk), naona ungeweka ya kiroho, mfano, hivi Yesu alihubiri kulipa kisasi au kutoa msamaha? Nadhani hapo ndipo panapotofautisha uisilamu (unaohimiza kulipa kisasi) na Ukristu (unaohimiza kutoa msamaha)
so yesu alihubiri ukristo?
[emoji848][emoji848]
 
Kwanza mimi sio mkatoliki so siwezi kuwa msemaji wa wakatoliki. Na huo mchoro haujautoa kwenye Biblia. So sielewi unachojaribu kusema.
Hebu kuwa wazi tatizo lako ni nini?

Kama ni Mungu mkuu, hilo halina shaka. Yesu ni Mungu mkuu, na siku yaja kila mtu, bahati mbaya kwako, utakuwemo, kuwa Yesu ni Bwana!

Wafilipi 2:
"5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba."
dah...
mungu mkuu, bwana, mungu baba..
 
Hivi yesu alivaa kanzu au Suluari?na alitawaadha au hakutawadha,na alipiga ishara ya Msalaba au alisujudu. Alikaa kwenye mabenji wakati wa kuswali au alikaa chini kitako


Na mama yake pia Bikira Maria alivaa gauni,sketi,suluari,au Baibui? Alivaa Hijabu au aliacha kichwa wazi,alipiga ishara ya msalaba au alisujudu,aliimba kwaya wakati wa kusali au alikaa kimya
Hizi akili hizi,miaka 2000 iliyopita hakukuwa na tekinolojia ya kutengeneza suruali!angevaa ipi?
Leo hii wewe unatumia smartphone,kipindi hicho hakukuwa na smartphone,kwahiyo wewe sio muumin kama wao wa kipindi hicho!
Kuvaa kanzu,kutawaza,kusujudu,kuimba kwaya hayo yote,ni mambo ya kimwili zaidi,hayaonyeshi status ya roho yako,ambayo Mungu anaitaka,
 
Yesu au Issa bin mariamu ni mtume wa mwenyezi Mungu kama mitume wengine,ingawa alisema wengine watasema tulihubiri kwa jina lako,lakini yeye atawakana.Swali langu linakuja je kina nani hao wanaohubiri kwa jina lake?
Sasa unauliza nini wakati unafahamu unachokiuliza acha chokochoko kwa watu wenye Yesu wao wewe endelea kuamini unavyoamini.
 
Pamoja na kujiunga jf juzi ila maswali kama haya yanaulizwa huko facebook, ni ya kitoto sana.

Then kama walivaa kanzu na akasujudu what gonna get fixed your heart.

Kwa nini ndugu yangu?nilichouliza kina ubaya
 
Nimesoma na nimesikiliza wanazuoni wa Kiislam, hii ya figurative unaitoa wapi? Unaweza kuleta hadith au Quran verse inayoonesha ni figurative?


Biblia iko wazi kwenye hilo. Inatumia devices kama Anthromophism, hyperboles, parables et al.

Ila tunaongelea Allah, Quran na Hadith. So achana na Biblia kwa sasa. Kwa sababu Allah ana Mguu na Mikono, Je kwa criteria zako unamkana kuwa siyo Mungu wako?



Hii ya pili ni video ya critic but inanukuu wanazuoni wa kiislam



Narudia tena swali langu. Kwa kuwa Allah ana jicho, mguu na mikono, unamkana kuwa hawezi kuwa Mungu?

I hope utajibu swali this time badala ya kujizingusha na kuja na nukuu badala ya jibu. Na katika hili swali weka pembeni Biblia, Yesu au Ukristo

Hizo nukuu lazima uwekewee ili usikwepe. Nimeshakufa mfano. Je mbingu zina mdomo au kijiti mungu wenu kwa sababu aliongea na Musa? Unakwepa nini hapo? Majibu mengine inalazimu tuwekee vyanzo kwenye vitabu vyenu humo humo ili muelewe vizuri.


Wala hana anaye fanana naye hata mmoja(112:4)

Hao wenyewe mnaodai wayahudi mnaotumia pamoja agano la kale hakuna mambo hayo ya utatu ya Mungu kugeuka mtu. We vumilia ndiyo haki ilivyo japokuwa ukweli unauma. Sio rahisi kupinga kitu ambacho umeaminishwa kuanzia udogoni hadi ukubwani. Vumilia ndiyo haki ilivyo.
 

Attachments

  • If God can do everything, can He become a physical being_.mp4
    10.2 MB
Hizo nukuu lazima uwekewee ili usikwepe. Nimeshakufa mfano. Je mbingu zina mdomo au kijiti mungu wenu kwa sababu aliongea na Musa? Unakwepa nini hapo? Majibu mengine inalazimu tuwekee vyanzo kwenye vitabu vyenu humo humo ili muelewe vizuri.
In cae una kichwa kigumu kuelewa, nitajaribu mara ya mwisho. Umesema haukubali Yesu ni Mungu kwa sababu Mungu hawezi kuwa na mwili. Nikasema sawa, twende na logic yako. Allah anasema ana mwili. Ana mikono, ana jicho ana mguu. Na haya hakuongea kama figure of speech wala hakuandika kama mfano kuelezea concept ili wanadamu tuelewe. Aliandika akionesha jinsi alivyo.

Sasa kwa kuwa kwa logic yako Mungu hawezi kuwa na mwili under any circumstance, unamkana Allah? Hili ndilo swali la msingi. LIJIBU!

Kuleta Biblia kama smoke screen haisaidii. Hata kabla ya Yesu, Mungu wa Biblia amejitokeza mara kadhaa katika umbo la mwanadamu. Na pia kuna sehemu nyingi ameongea kwa mifano, na figure of speech. Kwa hiyo kwa Wakristo hilo sio tatizo, ndio maana nikakwambia usipoteze muda kunukuu kitu ambacho kwetu sisi sio tatizo.

Kwa mara nyingine nikukumbuashe tena, kuwa swali ni Allah ana mwili na umesema under any circumstance Mungu hawezi kuwa na mwili. So logical conclusion ni kuwa unamkana Allah kuwa sio mungu wako? Na kama Allah ana mwili na huoni kama ni tatizo, huoni ni unafiki na double standard unapoukataa Uungu wa Yesu kwa sababu hiyo?

Hili ndio swali unalolikimbia. Naomba niulize tena, ili hata kama ni slow catcher ulielewe. Allah ana mwili kwa maana ana jicho, ana mguu na ana mikono kwa uchache. Quran na Hadith zimesema wazi. Wanazuoni wa Kiislam wamesema wazi na nimekuwekea video hapo ujionee!
SWALI: UTAMKANA ALLAH KUWA SIO MUNGU WAKO KWA SABABU ANA MWILI?

Nategemea utajibu badala ya kuruka kama walivyofanya waliokutangulia!
 
Kifupi kabisa ni kwamba, Uislamu haujakanilika!
Ni imani pekee Duniani ambayo inategemea imani nyingine ili ikamilike.
Bora hata wabaoabudu Ng'ombe hawahitaji dini nyingine kujikamilisha.

Uislamu haupo bila kujihalalisha kwa Ukristo
Una maana gani mkuu kwamba uislamu haukamiliki hadi hujihalalishe na utatu au kwamba Yesu ni Mungu au vp mkuu hebu fafanua? Au kwamba Yesu ni mali ya wakristo na hakuna mwengine anaruhusiwa kumuelezea Yesu tofauti na wanavyomueleza na kuamini wakristo?
 
Hivi yesu alivaa kanzu au Suluari?na alitawaadha au hakutawadha,na alipiga ishara ya Msalaba au alisujudu. Alikaa kwenye mabenji wakati wa kuswali au alikaa chini kitako


Na mama yake pia Bikira Maria alivaa gauni,sketi,suluari,au Baibui? Alivaa Hijabu au aliacha kichwa wazi,alipiga ishara ya msalaba au alisujudu,aliimba kwaya wakati wa kusali au alikaa kimya
alivaa kanzu yesu,,,Maria alifunika kichwa chake...

What is your point?
 
That white dude so called jesus he never existed...

Tafuta ushahid popote pale dunian kamwe hutoona ushahid wa mabaki wala ya kihistoria kuhusu uwepo wa icho kiumbe mnachokiita yesu.

Kwanza hilo taifa la huyo yesu wenu hapo middle East halijawai kuwepo before 1945 so where your jesus found?[emoji23][emoji23].

Someni histories za kweli achaneni na vijihabar vya kutunga vya uongo wa biblia na Quran, hakuna ukwel huko, ni makanjanja wachache waliamua kuchakachua history ya mtu mweusi wa kale na kuamua kuedit ili kupata matoleo ya nakala za vitabu vya hizo dini za kizushi zinazowatawala leo akili zenu na roho zenu.

Kuna mengi ya kuthibitisha kuwa hao Bible's characters wenu mnaowaabudu na kuwaita watakatifu hawajawai kuwepo na hawatowai kuwepo.

Ni aibu jitu jeusi kupigania na kushadadia dini za mtu mweupe, aibu sana, babu zenu wakifufuka hivi leo, watashangaa sana , yale waliyoyapinga ninyi mmeyakubari kiwepesi japo maisha yao yalipotezwa na hao waliokupeni hizo takataka mnazoabudu..

SHAME ON YOU religions believers

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
View attachment 2166502
Mkuu unaamini ngozi ya rangi inamfanya mtu kuwa bora?
 
Una maana gani mkuu kwamba uislamu haukamiliki hadi hujihalalishe na utatu au kwamba Yesu ni Mungu au vp mkuu hebu fafanua? Au kwamba Yesu ni mali ya wakristo na hakuna mwengine anaruhusiwa kumuelezea Yesu tofauti na wanavyomueleza na kuamini wakristo?
Nina maana kwamba, wakristo hawauhitaji uislam wala chochote kilichoko katika Quran ili wakamilike. Tofauti na waislam
 
Back
Top Bottom