ajabu ni kwamba hizi hoja kuna mtu zimemfanya awe muislam kinda kinda na yupo tayari kuzifia akiamini ana hoja zinto.
Wakati fulan uko nyuma nikapata Msala nikatupwa Gwanta siku 14.
ndani ya Sero yetu kulikuwa na sehem ndogo kwa ajili ya ibada ya waislamu nikawa najumuika kama kawaida.
katika kundi ilo la waumini ndani ya sero yetu nikafahamiana na kijana mmoja mwenye mkazo wa imani mbali na kuwa ni mtu pekee aliyekuwa ana hakikisha maji ya kushikia hudhu hayakosekani alikuwa ni mtoa Adhana.
baadae nikagundua anaitwa Charles, na ameslimu miezi kadhaa uko nyuma.
siku moja sikumbuki nini kilituingiza katika mjadala wa uislamu na ukristo.
akaniambia:, kilichofanya nislim mbali na sababu zingine zote ni pale kila nikifungua Biblia kuisoma na kutana na Neno Wagidion WAFANYABIASHARA .anaendelea kusema:, nilikuwa najiuliza, kwanini neno la Mungu lifanyiwe biashara?.
Inamaana hawa Wagidion wamekoswa biashara ya kufanya hadi wafanye biashara ya neno la Mungu!! toka hapo nikajua ukristo na biblia kwa ujumla ni utapeli, nikaamua kuslimu.
kwake Charles concept ya TRINITY haikuwa shida , swala la Yesu kuvaa ama kutovaa kanzu, kusujudu etc vyote hivyo kwake si hoja, hoja kwake ni WAGIDION wafanyabiashara[emoji23][emoji23].
nilimuangalia kwa sekunde kadhaa kwa umakini nikagundua upungufu wa maarifa ndiyo umemtoa katika imani yake ya hawali si wa Gideon, angelijaribu kutafuta maarifa jina wagidion lisingempa shida.
Watu wangu wanaangamia kwa kukoswa MAARIFA*.
kuna makumi out there wanaslimu kwa hoja kama hizi.
Hoja za kuwafanya waslimu ni hizi hizi kama za mleta Mada , kwakuwa hawana maarifa uwaona wahubiri wa hoja hizi kama watu watafiti na makini kumbe ni chenga tupu.