Yaani sinagogi ni msikiti? Alikuwa anatania au serious?
Pili Yesu hakuwahi kuwa Muislam, unless uamue tu kufanya uhuni wa kulazimisha awe. Yesu alizaliwa na Wayahudi, aliwekwa Wakfu na Simoni Myahudi katika hekalu la Mungu wa Wayahudi. Akakulia kati ya Baba seremala Myahudi, Mama Myahudi na waalimu Wayahudi. Aliishi katika Yudea na Samaria pekee, eneo la Wayahudi, na alifundisha juu ya Mungu wa Wayahudi na Mungu wa Baba zao, Yakobo (Israeli), Isaka na Ibrahimu, wote hawa Wayahudi.
Akafundisha kuhusu sheria ya Musa (Myahudi) na namna ilivyompasa Masihi wa Mungu (Myahudi wa kabila la Yuda), kufa kwa ajili ya kuukomboa Ulimwengu wote. Akashtakiwa na Baraza la kidini la Wayahudi, Sanhedrin. Kwa kuwa Yudea na Samaria lilikuwa koloni la Warumi, Wayahudi hawakuwa na ruhusa ya kuua mtu pasipo na ruhusa ya Kaisari. Ndio maana walipompeleka kwa Herode akawaambia wampeleke kwa Pilato (Mrumi) kwa sababu alikuwa ndiye mwakilishi wa Kaisari.
Yesu akashtakiwa kwa sheria ya Kiyahudi kuwa alikufuru kwa kuwa alisema Yeye ni Mwana wa Mungu na Wayahudi walielewa wazi hii ni kusema Yesu ni Mungu. Pilato hakuona kama Yesu alistahili kifo cha juu kabisa kwa sababu hakufanya kosa lolote. Wayahudi wakasema tuna sheria yetu na kwa hiyo tunamshtaki. Pilato (Mrumi), akawaruhusu Wayahudi wakamwue Yesu sawa na sheria yao baada ya kuwanawa. Wayahudi kwa msaaada wa Warumi wakamtundika Yesu. Na kibao cha mashtaka kiliandikwa Yesu, Mfalme wa Wayahudi. Wazee wa Kiyahudi walilalamikia kuwa kibadilishwe Pilato akagoma!
Kwa hiyo Yesu hajawahi kuwa Muislam. Usilam ulianza miaka zaidi ya 700 baada ya Yesu kuwapo duniani!
Mtu anayedai Yesu alikuwa Muislamu ni mmoja kati ya hawa
1. Hajui anachokisema/Kakariri
2. Hamjui Yesu au Uislam na Historia yake au hajui vyote
3. Ni tapeli!