Naomba mnisaidie niweze kula vizuri🙏🏼🙏🏼

Naomba mnisaidie niweze kula vizuri🙏🏼🙏🏼

Mimi ushauri wangu punguza vyakula vya michuzi,sijui hizo njegere za nazi,mara mchuzi wa wa sangara mara dikodiko kama la birian utakinai sana.....Bad ilishanishinda spices,unaweza amua kupika nyama ukaitia kitunguu,ndimu na chumvi tu....kaanga iwe ya brown kaanga mzuzu kula .. au chemsha viazi ulaya vikiiva vizuri vimekauka maji vizuri ila havijaungua tea blue band yako kiasi @ kuvisonga mpaka vilainike kula @,Sometimes nunua mahindi mabichi na maharage mabichi na njegere kidogo pika kande zako vizuri kula...mambo ni mengi ngoja nikuuitie wataalam Pridah Missy Gf Nuzulati
Mimi hapa nikae tu na mimi nijifunze nikisema nijitie uchef naweza kuharibu kabisa appetite ya mtoa mada😷
 
Spice kwa ajili ya samaki na beef hasa ikiwa masala ni hii, ikiwa sekela hasa samaki weka mamacita
Screenshot_20241222_102833_Chrome.jpg
 
Kwakua umeomba ushauri

Maake vyote ndo vyakula vyetu vya kila siku, na ndo Bora kwa afya

Ukipika ugali, wali hakikisha una mboga ya majani zaidi uipendayo, matunda, au juice ya matunda... plus samaki au nyama au maini ama dagaa

kwenye nyama unaweza pika Leo sotojo, kesho ukaoka, siku nyingine unaikaanga Cha msingi kuwa na taste tofaut tofauti ......

zingatia viungo kwenye upishi wako, carrots, nyanya, pilipili, kitunguu na vinginevyo bila kusahau masala ni nzuri kwa kunukia na kukufanya u enjoy msosi

Siku nyingine pika mchemsho tuu wa samaki au unachopenda ...... Ni msosi tosha

wali jitahd uwe na ubunifu nao.....

Leo wali maua, kesho kaanga kitunguu kimoja, siku nyingine kaanga, siku nyingine chemsha maji then pika, usipende kutumia rice cooker

kingine relax wakati wakula usiwe na issue za anxious... woga woga ondoa furahia msosi.....

Usile kama hutokula Tena..... Kula kuridhika zaidi

Pia fanya mazoezi ili upate appetite ya kula,
secretarybird @
Umemaliza, sina cha kuongeza kwa sasa.
 
Mimi ushauri wangu punguza vyakula vya michuzi,sijui hizo njegere za nazi,mara mchuzi wa wa sangara mara dikodiko kama la birian utakinai sana.....Bad ilishanishinda spices,unaweza amua kupika nyama ukaitia kitunguu,ndimu na chumvi tu....kaanga iwe ya brown kaanga mzuzu kula .. au chemsha viazi ulaya vikiiva vizuri vimekauka maji vizuri ila havijaungua tea blue band yako kiasi @ kuvisonga mpaka vilainike kula @,Sometimes nunua mahindi mabichi na maharage mabichi na njegere kidogo pika kande zako vizuri kula...mambo ni mengi ngoja nikuuitie wataalam Pridah Missy Gf Nuzulati
Abee
 
Kula vizuri ..ni kitafuna huku umefumba mdomo basi ... Hakuna kula vizuri zaidi ya hapo.....
Kwanza nimecheka sana aseh!!, Lkn kula vizuri, ni tafsiri ya mtu mwenyewe,,mi naweza kwambia mfano kwangu chakula kizuri ni ugali wa dona kwa mboga ya senene walioungwa baada yakukaangwa kwenye mafuta na baadae nyanya na vitunguu baasi,naridhika sana,pia mboga iyo iyo kwa ubwabwa,ndizi nk,kama wapenda chukua hiyo.
 
Shawarma sehemu nyingi elf 5, urojo sehemu nyingi elf 2 mpaka 3, ushakunywa uji wa ngano nzima?? Mtindi na viazi vitamu je? Au uchemshe karanga zenye maganda zile weka chumvi unapochemsha unashuhia na mango juice ya baridi.. sometimes nunua chocopops or your fave cereals kula na maziwa fresh au kata matunda au salad!!

Bila kusahau chapati za kumimina, kuku/samaki ya kukaanga + chai ya maziwa! Hapo snacks kama pringles, lays, danish cookies ziwepo.
 
Back
Top Bottom