10 Jun 2020
Serikali mkoani Kilimanjaro imeongeza timu ya wataalam kufanya utafiti wa kina kubaini kiini cha chemchemi chini ya jengo la kituo kipya cha mabasi cha kimataifa Ngangamfumuni mjini Moshi, Tanzania.
Habari za ziada :
July 9th, 2020
Moshi, Kilimanjaro
Tanzania
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo ametoa ushauri kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Mjini kukaa na wataalam ili wafanye utafiti wa kina wa jinsi ya kukabiliana na maji yaliyopo chini ya ardhi katika eneo lililojengwa kituo cha Mabasi.
Picha : Ujenzi wa Stendi mpya ya Kimataifa ya mabasi , Moshi Tanzania
Ujenzi Wa Stendi Ya Mabasi Moshi Mjini unakabiliwa na changamoto Mkondo Wa Maji unaoibua chemchem katika ghorofa ya chini ya ardhi katika ujenzi wa stendi hiyo.
Ametoa kauli hiyo leo baada ya kukutana na uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Moshi wakati akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Mhe. Jafo amesema kuwa kwa sasa maji yanapita katika eneo hilo lakini yakiwa yamepungua, huku wataalamu wakiendelea kutafuta ufumbuzi kwa maji kujaa yakitokea chini ya Ardhi.
Ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Moshi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo hasa katika ujenzi wa miradi ya kimkakati japokuwa mradi huo umekuwa na changamoto ya jengo kujaa maji kwa chini.
Aidha Mradi wa Stendi ya Mabasi Mkoani huo utagharimu shilingi bilioni 28 fedha ambazo zilitolewa na Serikali kwa Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa Miradi ya kimkakati.
Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Bw. Michael Mwandesi ameeleza kuwa mradi wa stendi ya mabasi umepata changamoto kubwa ya jengo kujaa maji chini jambo ambalo lilisababisha Halmashauri kusimamisha ujenzi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa chanzo cha maji hayo.
Amesema mpaka sasa wataalam wameshafanya utafiti wa kina na imegundulika kuwa jengo hilo halijaathrika na maji hayo, kutokana na uimara mkubwa wa jengo hilo.
Source :
Jafo aagiza wataalamu kufanya utafiti wa maji yaliyochini ya ardhi mradi wa Stendi ya Mabasi
21 June 2020
Moshi, Kilimanjaro
Tanzania
Wataalamu wa Jiolojia wafanya utafiti wa Chemchem mkoani Kilimanjaro
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kurugenzi ya Huduma kwa Umma pamoja na Idara ya Jiologia kutoka Ndaki ya Sayansi Asili na Sayansi Tumizi, imeleta wataalamu wa maji ya ardhini ili kuisaidia Manispaa na Moshi kupima na kuangalia maji yanayotoka ardhini na kujaa kwenye makazi ya watu na katika mradi mpya wa Stendi maeneo ya Majengo. Msafara huo wa wataalamu unaongozwa na Dkt. Mona Mwakalinga- Mkurugenzi Huduma kwa Umma, Dkt. Simon Melekioly, Dr. Remigius Gama na Bwn. Majura Songo kutoka Idara ya Jiolojia.
Source : University of Dar es Salaam