Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Yeah.Nilikuja nikajifanyia tathimini nikaona mpira ni nonsense nika declare sitozungumzia mpira kwa 10
Nilifikiria labda mpira unaweza kuwa na sense kama ajira. Kwa wanaocheza.Nikaona hata hiyo ni kitu cha kupangwa na watu hakina umuhimu hivyo. Tena wacheza mpira wanaliowa sana kwa kazi isiyo na maana halafu watu wanaofanya kazi za maana sana za kugundua madawa na kuokoa maisha ya watu hawalipwi vizuri hivyo.
Nikasema labda una umuhimu kwenye mazoezi, nikaona kuna namna za kufanya mazoezi zilizo objectively more efficient.
Nikasema labda unajenga community. Kuna siku mimi mwenyewe nilikuwa Philadelphia nimevaa kofia ya New York Yankees (Marekani kuvaa hivyo lazima uwe mshabiki wa Yankees sio huko kwingine unavaa tu kofia zile za NY, mimi nilivaa kwa sababu ya kukaa New York tu).
Kuna jamaa nilikutana naye kwenye mall alinifurahia sana kwa sababu Philadelphia hakuna washabiki wa New York wengi. Ikawa kama kakutana na ndugu yake bila kutegemea, wakati hata hatujuani. Nikaona labda hapa ndipo umuhinu wa hii michezo ulipo.
Nikaja kugundua unaweza kujenga community hivyo efficiently zaidi bila kuhitaji michezo.
Nikaja kugundua michezo hii ni mabaki ya tamaduni fulani zilizotusaidia ku bond na ku evolve katika groups huko nyuma lakini sasa hivi haina umuhimu huo, inajaza nafasi ya kupoteza muda kwa bored people tu, ila vichwa vyetu havija evolve kuwa sawa na muda huu.