Naomba ushauri jinsi ya kumuapproach aliyenitafutia kazi, nataka kuacha kazi

Nature ya Kazi ni Kudeal na mikopo Sasa nimejitahidi kuendana na mfumo lakini najikuta nafsi inakataa ni kazi ambayo inataka roho mbaya afu usiwe msikilizaji na pressure kutoka juu ni kubwa sasa Mimi ni good listener inshort sipo tayari kuifanya
Piga chini huo ujinga , mikopo unatakiwa uwe na roho mbaya , alaf anayenufaika ni aliyeko juu huku wewe mtenda dhambi kuu unakula kiduchu ...!!
 
Umenikosha sana "Tape measure" na comment yako hii.... Huyu jamaa ni KenchyType Islamabad kabisa....
 
Mie mwenyewe kaniudhi...afu ukute ni me😝
 
Hahah dah huyo jamaa bado haha experience maisha huyongoja aingie mtaani huku Hana kazi
 
Kumbe wewe ushakuwa sugu wa kuacha acha kazi, utakuwa na pepo linakufanya uichukie kazi...
Ukitoka hapo uanze tena kuomba utafutiwe kazi...
Kama ulijua una mishe zako, kwanini ulimsumbua mzee wa watu akutafutie kazi?
True huenda ana roho za ajabu
 
Kumbe wewe ushakuwa sugu wa kuacha acha kazi, utakuwa na pepo linakufanya uichukie kazi...
Ukitoka hapo uanze tena kuomba utafutiwe kazi...
Kama ulijua una mishe zako, kwanini ulimsumbua mzee wa watu akutafutie kazi?
Huo ni mtazamo wako Bantu lady na naheshimu mawazo yako.
 
Aisee ilishawahi kunitokea hii, nilipataga connection ya chombo, nikaingia chomboni, nikapiga kozi ya awali 6 months nikaona akili na nafsi vinakataa kabisa. Yani ni kama niliingia bila kujishauri mara mbili, badae wakati nasubiri kozi ya ajira nikaona isiwe case kwanini nikafanye kazi nisiyoipenda..nikachomoka zangu kimya kimya bila kumwambia aliyeniunganisha, ila aliyeniunganishaga chomboni alikujaga kupata taarifa kuwa nimeachia ngazi, Tena nayeye alikua mtu mkubwa tu chomboni...nilinuniwa weee sikujali. Sasa hivi ninafanya kazi niliyoipenda..All is well
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…