Naomba ushauri juu ya hii biashara ya kuagiza bidhaa mchanganyiko kutoka Japan

Simple way, tafuta mtu anaefanya kazi bongo uingie nae partnership,

Au promote page yako mitandaoni, ila wabongo wanahitaji mtu awepo na ofis bongo ili wamuamini, so kuweka ofisi bongo ni lazima
Hapo lazima afaulu akifuata ushauri huu itakuwa rahisi kuyaendea yale atakayo
 
Engine za Boti kama unaleta used jaribu kuleta za miaka ya 2007 kupanda juu. Spare za Engine za Boti za Japan bei ipo juu, huku Tanzania watu wanakimbilia copy ya mchina kwa bei nafuu
 
Mkuu vip kuhusu baiskel uko japana zinauzwaje
 
Ongea na KC Global.Mnaweza kufanya kazi pamoja
 
website yako ilikuwa haieleweki kwa hiyo ilikuwa rahisi kwa mtu kuipotezea, kingine ilitakiwa uwe na page instagram na youtube kwa ajili ya ku display bidhaa bila kusahau kulipia matangazo,mbona watu wengi wamefanikiwa kama dantraders anatuma vitu kutoka sweden,sasa hivi inabidi uje kivingine ushindani na china umekuwa mkubwa.Sasa hivi unaweza kuanza ukiwa umeajiriwa cha kufanya ajiri social media & customer care manager anae ijua kazi yake vizuri kisha baadae itakubidi ufungue ofisi hapa bongo
 
Acha ubinafs mkuu....biashara ni ushirikiano...unafeli sababu una ule ubinafs.

Funguka tafuta washirika weka share mezani mpige kazi.....una nafasi nzuri ya kutengeneza pesa ila ndo hvyo hutaki wengne wale kupitia wewe..

Tafuta connection hao tra bandarini ni waraini sanaa,
 
Ungepitia vizuri bandiko langu naona umekuja kiungonvi badala ya kushauri

Hakuna sehemu nimesema TRA ni kikwazo wala Mtaji kuwa kikwazo,

Niliomba ushauri wa kutumia njia za kikisasa za digital platforms kufanya biashara ambazo wanunuzi ulipia kabla ya ku Derivery mizigo,badala kununua bidhaa kuzipakia kuzisafirisha kulipia ushuru Kisha ukaziingiza sokoni na zikakosa wanunuzi huu sio nfumo sahihi kwenye biashara

Utakapotoa ushauri wako ujikite kwenye Mada.
 
Nimekuelewa mkuu....sorry kwa lugha niliyoitumia.

Ila nakushauri tafuta connection ya wawekezaji au share holder..muwe mnagawana faida na hasara pia ukizingatia wewe upo nje ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…