Naomba ushauri: Kijana wangu amepata kazi Shirika la Good Neighbors na Halmashauri, aende wapi?

Naomba ushauri: Kijana wangu amepata kazi Shirika la Good Neighbors na Halmashauri, aende wapi?

Kama Halmashauri ni Mkataba wa muda mrefu aende Halmashauri kwasababu Good Neighbours wa kawaida sana...ingekua Mashirika makubwa angeacha hiyo ya Halmashauri...Halafu huyo Jamaa yako anasali kwa Mungu yupi anaempa kazi mbili mbili wakati watu wameoga na mafuta ya manabii hawapati hata Kibarua ??
Maandiko yanasema mwenye nacho ataongezewa na asiye nacho ata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa Mkuu.
 
Aende Halmashauei akithibitishwa kama ana hulka ya kufanya kazi kwenye mashirika anaomba likizo bila malipo anapiga mzigo huko mashirikani kwenye mashara mnono na nafasi yake huko halmashauri inabakia kumsubiria.
 
Aende halmashauri akiiacha hiyo nafasi atajuta. Serikalini nafasi ni chache na wanaopata ni bahati.
 
Ni kitinda mimba wangu. Amepata kazi Serikalini kwenye Halmashauri moja Mkoani Shinyanga na pia kwenye Shirika linaitwa Good Neighbors Tanzania. Mishahara ni kama inalingana, aende wapi?

Naomba ushauri wapendwa.
Ha!! Unajiuliza.Aende Halmashauri maana kama kweli mishahara inalingana ujue Halmashauri utazidi...usiulize sana.
 
Back
Top Bottom