Naomba ushauri kuhusu biashara yangu inakoelekea inaenda kukata roho sio muda

Naomba ushauri kuhusu biashara yangu inakoelekea inaenda kukata roho sio muda

aBuwash

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2023
Posts
262
Reaction score
497
Habarii wana JF natumai wote mko salama.

Mimi ni mfanyabiashara wa mchele hapa Dar es Salaam
Nauza jumla na rejareja.

Ila nasikitika toka nifungue hiii baishara yangu nimepitia changamoto nying sana mpka leo na nimekuwa mtu ambaye sikatii tamaa nikijipa moyo kwamba ndo napata experience maana ndo mara yang ya kwanza hii biashara.

Lakini changamoto amabyo imenipelekea kuandika huu uzii ni hapa ambayo nimetumia njia zote nimeshindwa biashara naiendesha kwa hasara sipatii faida hata kidg na basi ikipatikana inakuwa ni ndgo sana..

Hiyo changamoto ni kwamba kila nikileta mchele kweny store yang wateja wanarukaruka kwamb mchele wanaona siyo mzurii najitahidii kugradee jambo amablo linapelekea faida yang yote kuishia huko ilimradii tu niwateke wateja kwa vitu vizurii lakini wapi nimejikuta napoteza mtaji wang nusu nzima mpka sasa.

Na kingine mimi nipo mbagala dar es salaam nzima wanasifia mbagala kuuza mchele bei rahisii ni kwelii huku bei ni rahissiii jana nimetoka nimeenda sehem nyingine nimekuta mchele naouza mimi huku 1400 wao wanauza 1600
Sasa niko nawaza nifunge hapa flemu nikatafute sehem nyingine niendelezee baishara hiii hii ya mchele au nitafutee tu biashra nyingine nifanye naomba mnisadie sana.

Ushaurii wenu unahitajika hii biashara hemu imagine miezii saba sasa haijawah kunipa faida hata kidg nimevumilia nimechoka nahisii napoteza tu kila siku.

Maduka ya mchele sasa yamejaa kila kona kila mtu anauza mchele, na wakulima hawajkaa mbalii kila mkoa unalima mchelee.

Miaka yotee huu mwezii wa tisaa michele inapanda bei ila mwaka huu mpka mchele wa 1300 ninao mimi ofisini afu baishara haiendii kabisa yaniii

Nitafute eneo linginee au nibadilishe baishara msaada wenuu wakuu
 
usikate tamaa katika biashara kuna wakati unaweza pitia kipindi kigumu sana ila endelea kukomaa mambo yataakaa sawa mpambanaji.
Napambana ila napoteza tu kila siku mzee mpka kwenda kufungua ofis mtu unaona kaziii kwasabab unajua kabisa naenda kuuza mzgo ambao haunipii faida yani kama nacheza tu na mwisho wa mwezi watu wanalamba kodii zao daah
 
Kitu chochote unachokifanya kwa kutumia nguvu nyingi na kinakupa matokeo hafifu kuliko nguvu ulizotumia.

Ujue hiko si Kitu kinachofungamana na wewe so usipoteze muda endelea kujitafuta kwenye biashara nyingine na ipo siku utaangukia kwenye biashara moja na once utakapoianza utajutia why hukuianza tangu zamani na usikute ndio biashara ambayo ulikua unatamanigi kuifanya ila ukawa unaidharau kwakua watu hawaizungumzii sana.
 
Pole kwa bei hiyo mimi naona umejikita uuze kwa bei ya chini mzigo mzuri na uwe unatoka ila umefeli kwani unaambulia faida kiduchu,

Badili mfumo weka mali kali na bei pia iwe mkasi ila usiwasahau wa bei ya chini wawekee nao mzigo wao.. wapo wateja ambao bei kwao sio ishu wanataka mali safi utawapata.

Weka na bidhaa nyingine za kusindikiza mchele kama mafuta unga Dagaa Mayai.

Ukifeli pia usikate tamaa utakua umejifunza angalia location nyingine au badiri biashara.
 
Pole kwa bei hiyo mimi naona umejikita uuze kwa bei ya chini mzigo mzuri na uwe unatoka ila umefeli kwani unaambulia faida kiduchu,....
Mzee ninavioo pale ofisini achaa nina super za kila aina tena zinanukia blaaa ila ujinga wake zeneywe utokaji wake ni mudg kwa sabab mbagala wengii ni kipato cha chini kwaiyo wanahitaji michele ya bei ndg na ndo yenye mznguko mkubwa
 
Kitu chochote unachokifanya kwa kutumia nguvu nyingi na kinakupa matokeo hafifu kuliko nguvu ulizotumia ujue hiko si Kitu kinachofungamana na wewe so usipoteze muda endelea kujitafuta kwenye biashara nyingine na ipo siku utaangukia kwenye biashara moja na once utakapoianza utajutia why hukuianza tangu zamani na usikute ndio biashara ambayo ulikua unatamanigi kuifanya ila ukawa unaidharau kwakua watu hawaizungumzii sana.
Umeongea point kaka nimejaribu njia zote zinadunda natoka naenda nkaaa maporini huko wiki nzima kutafuta vitu vizurii lakini wapiiiii naishia kuambulia patupu
 
Biashara ya hasara sana hiyo....uchawi mwingi mno.Unaweza dhani wauza mchele kumbe wateja waona chumvi ya mawe.

Kuna mtu jirani hapa yalimkuta,yeye anauza kuni Kila siku wateja wanalalamika kuwa Kuni mbichi haziwaki.

kimuonekano Kuni ni kaukau balaa...kumbe.

walishambadilishia walimwekea miwa yeye hajui
 
Biashara ya hasara sana hiyo....uchawi mwingi mno.Unaweza dhani wauza mchele kumbe wateja waona chumvi ya mawe....Kuna mtu jirani hapa yalimkuta,yeye anauza kuni Kila siku wateja wanalalamika kuwa Kuni mbichi haziwaki....kimuonekano Kuni ni kaukau balaa...kumbe walishambadilishia walimwekea
Dah kwaiyo ushaurii wako upii kaka
 
Back
Top Bottom