Hbarii wan jf natumai wote mko salama.
Mimi ni mfanyabiashara wa mchele hapa Dar es Salaam
Nauza jumla na rejareja.
Ila nasikitika toka nifungue hiii baishara yangu nimepitia changamoto nying sana mpka leo na nimekuwa mtu ambaye sikatii tamaa nikijipa moyo kwamba ndo napata experience maana ndo mara yang ya kwanza hii biashara.
Lakini changamoto amabyo imenipelekea kuandika huu uzii ni hapa ambayo nimetumia njia zote nimeshindwa biashara naiendesha kwa hasara sipatii faida hata kidg na basi ikipatikana inakuwa ni ndgo sana..
Hiyo changamoto ni kwamba kila nikileta mchele kweny store yang wateja wanarukaruka kwamb mchele wanaona siyo mzurii najitahidii kugradee jambo amablo linapelekea faida yang yote kuishia huko ilimradii tu niwateke wateja kwa vitu vizurii lakini wapi nimejikuta napoteza mtaji wang nusu nzima mpka sasa.
Na kingine mimi nipo mbagala dar es salaam nzima wanasifia mbagala kuuza mchele bei rahisii ni kwelii huku bei ni rahissiii jana nimetoka nimeenda sehem nyingine nimekuta mchele naouza mimi huku 1400 wao wanauza 1600
Sasa niko nawaza nifunge hapa flemu nikatafute sehem nyingine niendelezee baishara hiii hii ya mchele au nitafutee tu biashra nyingine nifanye naomba mnisadie sana.
Ushaurii wenu unahitajika hii biashara hemu imagine miezii saba sasa haijawah kunipa faida hata kidg nimevumilia nimechoka nahisii napoteza tu kila siku.
Maduka ya mchele sasa yamejaa kila kona kila mtu anauza mchele, na wakulima hawajkaa mbalii kila mkoa unalima mchelee.
Miaka yotee huu mwezii wa tisaa michele inapanda bei ila mwaka huu mpka mchele wa 1300 ninao mimi ofisini afu baishara haiendii kabisa yaniii
Nitafute eneo linginee au nibadilishe baishara msaada wenuu wakuu
Naomba na mimi nikushauri mambo matano (5), jambo la NNE ni muhimu zaidi.
✍️KWANZA: Usibadili biashara kwasababu hiyo ni biashara ulioizoea. Huwezi kuthibitisha kuwa hiyo biashara ya mchele ni mbaya kwasababu umesema wenzako wanaofanya biashara hiyo hiyo wamesonga mbele. Hivyo sikushauri kubadili.
✍️PILI: Hilo wazo lako la kubadili Location kwa biashara hiyo hiyo ni wazo zuri sana. Kwasababu Location inaweza kuchangia kukurudisha nyuma hasa aina ya wateja wako wanaokuzunguka - wateja wengine wapo kama Muhindi ambaye anaruka saluni kumi za mtaani kwake anakwenda kunyoa saluni ya muhindi mwenzake iliyopo mtaa wa saba. Hivyo fanya uchunguzi kama tatizo sio biashara yako ni wateja, fanya mpango uhame Location.
✍️TATU: Ni vizuri pia unapoona biashara moja haitembei changanya biashara nyingine, lengo ni kujitofautisha na wengine. Biashara yako ya mchele inafaa kuchanganya na biashara ya Maharage ya rangi tofauti, Njegele, karanga, n.k.
✍️NNE: Hebu chunguza uone wenzako wanauza mchele wa aina gani. Kwenye biashara (bidhaa) kuna vitu vingi sana, kwa sasa nikwambie vitu vitatu vifuatavyo......
1. UBORA (QUALITY) - Nashukuru umesema kuwa kipengele hiki cha ubora umekizingatia. Lakini ngoja nikuongezee; asilimia kubwa ya wateja wa mikoa ya ukanda wa pwani (Tanga, Zenji, Dar, Pwani, hata Moro) huwa kwenye mchele wanapenda harufu (mchele unaonukia sana) kuliko ubora mwingine, hivyo hakikisha kwenye hilo.
2. CHAPA (BRAND) YA BIDHAA - Wateja wengine hawavutwi na ubora wa bidhaa, wanavutwa na chapa ya bidhaa. Kuna watu tangu utotoni wameshakaririshwa kuwa mchele wa kutoka mahali fulani ni mzuri kuliko wa sehemu fulani. Mteja mwingine ukimwambia huu mchele ni wa kutoka Mbeya tayari ushammaliza hata kama sio mchele mzuri, mwingine ukimwambia huu mchele ni wa kutoka Morogoro ushammaliza hata kama siku hiyo ulijumua mchele mbovu. Yaani mtu anafuata BRAND tu. Ndo maana sikuhizi usishangae kumkuta mtu mwenye iphone ya Tsh 500,000 anamdharau mwenye samsung ya Tsh 2,000,000.
3. CHAPA (BRAND) YAKO - Ni vizuri uendelee kutengeneza connection kwa wateja wengi ili ukuze jina lako. Huenda wenzako wanauza sana kwasababu ya majina yao (washatengeneza majina). Tengeneza jina lako, wapelekee mchele hadi mlangoni. Mteja akinunua hata debe moja kama anaishi umbali wa chini ya kilomita mbili; mtume kijana wako ambebee mzigo mteja.
✍️TANO: Usikate tamaa, changamoto na vikwazo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.