Naomba ushauri kuhusu biashara yangu inakoelekea inaenda kukata roho sio muda

Yap 100%. Nilijaribu kumwelezea na mimi sema sikufunguka vizur. Ishu za kibiashara zipo kiroho sasa aangalie wapi pa kwenda na kufanikiwa. Pia ajitathimin yeye mwenyewe sio kila mtu anaweza kuwa mfanyabiashara ndo maana unaweza mpa mtu hata 100M ikafa yote.
Kabla ya kuingia kwenye biashara aangalie hayo mambo uliyomfafanulia hapo juu.
 
Mkuu hongers kwa ushauri wako. Mlengwa asipoufanyia kazi basi kutakuwa na tatizo sehemu.
 
Mzee ninavioo pale ofisini achaa nina super za kila aina tena zinanukia blaaa ila ujinga wake zeneywe utokaji wake ni mudg kwa sabab mbagala wengii ni kipato cha chini kwaiyo wanahitaji michele ya bei ndg na ndo yenye mznguko mkubwa
Kama ulivyosema ndivyo ilivyo basi hiyp location sio sahihi kwako. Jaribu kutanuo wigo fungua branch sehemu nyingine ya watu wengi wa kipato cha kati + weka huo mchele wako gredi za juu na hapo bakiza mchele unaoendana na mahitajo soko la hapo.
 
Kama ulivyosema ndivyo ilivyo basi hiyp location sio sahihi kwako. Jaribu kutanuo wigo fungua branch sehemu nyingine ya watu wengi wa kipato cha kati + weka huo mchele wako gredi za juu na hapo bakiza mchele unaoendana na mahitajo soko la hapo.
Shukranii sana ndo nalifanyia kazi hilo wazo
 
Sina uzoefu wa biashara ya mchele ila sababu nilishafanya biashara zingine so naomba nikushauri kulingana na uzoefu wangu kwenye biashara nyingine.

Umesema mpaka sasa una miezi saba,basi hiyo miezi ni michache kwa biashara kukomaa na kuweza kukupa faida ile uliyoipanga.Mara nyingi biashara nyingi huwa zinaanza kukua kwenye miezi sita ya pili,haani ndio angalau unaanza kufikia biashara kujiendesha bila hata ya kutengeneza faida.
Chakufanya chukua daftari lako la mauzo tangu umeanza biashara,piga hesabu ya kila mwezi kwa miezi hiyo saba uangalie je mauzo yalikua yakiongezeka kila mwezi? Tafuta wastani wa mauzo wa kila mwezi kwa siku kujua uhalisia wa ukuaji wa biashara yako,kama mauzo yanaongezeka hata kama ni kidogo basi jua biashara yako inakua ila ni kaa speed ndogo na inazidiwa na expenses so unahitaji kufikiria njia ya kupambana na hilo.Kwa hiyo mtaji unakata kwa sababu biashara ina matumizi makubwa.

Kwa upande wa kuhama biashara moja kwenda nyingine ni lazima ujue kuwa unaenda kuanza upya na kuanza upya kunahusisha kufanya makosa mengi ambayo huku kwenye mchele ulishayafanya na ukajisahihisha kufikia hapo ulipo sasa hivi.Tunapozungumzia uzoefu kwenye jambo fulan huwa tunamaanisha na hayo makosa ambayo kivyovyote hayaepukiki na yana gharimu muda,pesa,taarifa na network ya watu.
Pia lazima ujue kuwa classes kwenye maisha zipo na haziepukiki,kama unauza bidhaa fulani,huwa ni ngumu sana kuuza sana kama utachanganya watu wa tabaka la juu na watu wa tabaka la chini.Yaani huwezi kuwa na duka moja ukajaza bidhaa za matajir na masikini halaf ukategemea hao watu wote watakuja kwako,huo ni uongo hapo ni lazima tabaka moja litajichuja na hivyo utapata hasara tu.
Mfano matajiri watahitaji eneo lako lionekane kitajir yan lina mvuto na high classic sasa ukiweka eneo lako hivyo lower class wataogopa kuja hapo maana wao saikolojia yao na vitu hivyo haiendani kabisa kwa kuhofia bei,na kama watakuja wale wa juu hawatakuja maana aina ya wateja wako itawafukuza kwa kuona pamekaa kiswazi na ikitokea wakaja,wakiingia ndani wakakuta unavitu vya bei rahisi sana kwenye akili yao wanaogopa kuwa vitu vyako vyote havina quality hata kama ni kweli umejitahidi kuvitenga kulingana na ubora wake.
So chagua tabaka unalotaka kudeal nalo halafu komaa mpaka wakujue ujenge uaminifu nao na hapa utahitaji huduma bora kulingana na tabaka unalolilenga lakini pia uweze kutoa huduma hiyo muda wowote watakao hitaji huduma yako bila kupunguza ubora.
Kama unauza jumla kweli basi ni lazima uwe na jumla mbili,jumla kwa ajili ya watu wanaochukua kwa ajili ya matumizi ya kifamilia na jumla kwa ajili ya watu unaowajua kuwa wanamaduka.Bei ya mtu ambaye unajua kuwa anaduka inatakiwa iwe tofauti kabisa na bei uliyoibandika kwenye gunia kuwa ni bei ya jumla.Na mfanye mteja ajue kwamba kwako kuna bei fulani za wateule ambazo hazipo kwenye magunia ya mchele hapo utatengeneza wateja permanent,hii phyilosophy kajifunze kwenye maduka ya jumla kkooo
Cha mwisho wewe pita kwenye maduka ya rejareja ukatangaz3 mchele,waachie namba yako waambie wakupigie pindi wanapphitaji mchele ili uwape bei
Nakutakia kazi njema,usikate tamaa maana familia yako inakutegemea.Haya ndio maoni yangu kwako na samahani maana kuna maeneo nimechanganya vimisamiati vya kiingereza ila natumai tumeelewana.
 
Ushaurii mzuri sana kk nashukur sana
Leo kuna jirani kahama afu pembeni yangu anazidi kunitisha sio pekee angu tu kumbee ninaepitia kipind kigumu
Ila ngoja nikomae
 
Ushaurii mzuri sana kk nashukur sana
Leo kuna jirani kahama afu pembeni yangu anazidi kunitisha sio pekee angu tu kumbee ninaepitia kipind kigumu
Ila ngoja nikomae
Biashara inahitaji uvumilivu mkubwa sana,pigana unavyojua wewe ila siku ukisema unataka kuchange basi hakikisha umepiga hata miaka miwili kwa kuzingatia niliyokwambia.
Ogopa sana kuhama hama location na kudandia business mpya zinazoingia town kabla ya kuisimamisha hiyo uliyonayo.Na baadae utakuja kugundua kuwa hata "chimbo unalochukulia mzigo sio chimbo" zingatia sana hapo nilipoweka hizo alama.
 
Mkuu kwanza nikushauri location uliyopo ndio location sahihi kwa biashara ya mchele.Hii biashara nimezaliwa nimekuta wazazi wangu wanafanya mpaka sasa wanafanya
Biashara ya mchele inahitaji ujanja yaan ubadilike kulingana na mahitaji ya wateja hata kama shamba bei zimepanda jitahidi kutengeneza mchele wa bei ndogo nazani unajua namna ya kutengeneza, kingine tunaelekea kwenye miezi ya 12,1,2na3 hiyo miezi ndio muda wa kupata wateja maana huwa kunakuwa na uhitaji mkubwa wa mchele sababu ya bei.
Sasa hapo jitahidi kuandaa zana kwaajili ya kutengeneza mchele wa bei ndogo maana hicho kipindi wateja huwa hawaangalii uteja wanaangalia wapi kuna bei ndogo.
Kingine kila mteja wa jumla yaani kuanzia kg 50 anaekuja iwe kwabahati mbaya au makusudi hakikisha unachukua namba yake zingatia hilo halafu kila unaposhusha mzigo unawatumia sms au unawapigia kabisa simu kuwaambia mzigo umefika wa bei hii hii na hii hata kama hujashusha mzigo ikipita week tuma sms au piga simu tengeneza urafiki na wateja.
La mwisho biashara inahitaji uvumilivu na muda wa watu kukuzoea pia epuka kufunga funga ofisi yako wateja watajua haupo serious na kazi hata kama unafata mzigo tafuta mtu wa kumwachia usifunge ofisi.
Kwa uzoefu wangu maeneo sahihi kwa biashara ya nafaka yaan mchele ni tandika, mbagara, gongolambo,kawe na maeneo yote wanaopenda kuvaa madela 😂. (Sehemu zenye jamii ya waislamu wengi) All the best
 
We jamaa unakitu kwenye chimbo hapo umenena mimi bado cjalifahamu chimbo la kuchukua mzgo ili kushindana na ushindani mkubwa huu nilionao aisee
 
We jamaa unakitu kwenye chimbo hapo umenena mimi bado cjalifahamu chimbo la kuchukua mzgo ili kus
Unajua biashara ya mchele siriii imejificha kwenye sehem za kununua mchele basiii huko ndo siri ya wanaofanikiwa na wanaofelii ilipo
 
We jamaa unakitu kwenye chimbo hapo umenena mimi bado cjalifahamu chimbo la kuchukua mzgo ili kus

Unajua biashara ya mchele siriii imejificha kwenye sehem za kununua mchele basiii huko ndo siri ya wanaofanikiwa na wanaofelii ilipo
Naumiza kichwa kupata machimbo ambayo bei itakuwa rafiki nakosa kabisa aiseee
 
Uko sahihi mkuu
 
Tafuta sehemu nyingine kama vile amabayo ni ya kishua kidogo.
 
Jaribu kumix mchele kama wengine huenda bei ukaenda nao sawa, wanatuchanganyia super na Chenga kidogo halafu inaandikwa super *****
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…