Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Pole mkuu...Umeongea point kaka nimejaribu njia zote zinadunda natoka naenda nkaaa maporini huko wiki nzima kutafuta vitu vizurii lakini wapiiiii naishia kuambulia patupu
Ila unatakiwa ujue kwamba asilimia kubwa ya watu ambao wamefanikiwa kwenye maisha ya utafutaji hasa kupitia kwenye upande huo wa kibiashara ni kwamba wameweza kujiungamanisha na upande wa kiroho iwe kwa kujua au kwa kutokujua na iwe upande wa kiroho wa gizani au upande wa kiroho wa nuruni, huwa haijalishi Ila nguvu za umiliki huwa haziko upande huu wa damu na nyama bali zipo upande wako wa pili ambao ni upande wa kiroho.
Kwahiyo Kuna watu ambao walijaribu biashara nyingi sana ambazo zote hazikuwapa mafanikio Ila baadae walikuja kukutana na biashara moja tu ambayo walivyoamua kuifanya hapo hapo wakaanza Kuona mafanikio ambayo hawajawahi yaona kwenye biashara nyingi walizowahi kuzifanya na hii biashara ndio tunasema sasa kwamba inayo muunganiko wa moja kwa moja na upande wako wa kiroho Kwahiyo inakuunganisha pasipo wewe mwenyewe kujua.
Inawezekana hujaelewa hapo Ila nakuhakikishia kwamba biashara ni kama mila na desturi zilizopo kwenye makabila, kwamba Kuna mila inaaminiwa sana na kabila fulani na wanaifuata kwasababu inawapa matokeo wanayoyataka pindi wanapoifuata Ila wewe mtu wa kabila lingine ukienda kuifuata hiyo mila haitakupatia chochote unachotaka kwasababu wewe asili yako haiko huko Kwahiyo na wewe ukitaka ufanikiwe kwenye mambo ya kimila nilazima ufuate zile mila ambazo zinafungamana na asili yako.
Tukirudi kwenye biashara ni the same, biashara ambayo inampa faida kubwa sana rafiki yako wewe ukienda kuijaribu unaweza usifanikiwe hata kwa japo faida kidogo, sana sana utapoteza mtaji wote huko kwasababu hiyo biashara haifungamani na wewe kiasili ila biashara hiyo hiyo ambayo wewe hufanikiwi nayo unakuta Kuna rafiki yenu mwingine kwenye hiyo cycle yenu nae anajaribu kuifanya ghafla anafanikiwa, sasa wewe unaweza kujihisi unagundu na mikosi ila wala sio kweli ni vile tu haujui namna ya ulimwengu unavyofanya kazi.
Kuna biashara ambazo zinafungamana na watu fulani fulani na Kuna biashara ambazo hazifungamani na watu fulani fulani.
Najua ni mambo ambayo yanashangaza halafu yamekaa kufikirika fikirika sana, ila ndio asili ilivyo na ndio maana always unaambiwa dunia inaendeshwa na watu wenye nguvu, sasa watu wenye nguvu sio kwamba wako na misuli mingi, hapana ila watu wenye nguvu huwa wanajua namna universe inavyofanya kazi na ndio maana unaona matajiri wengi huwa wanawekeza pesa nyingi kwenye vistartup venye idea nyepesi sana wakati wangeamua wangeweza kununua hizo algorithm na kuzifanya wao wenyewe ila wanafanya hivi kwasababu wanajua sio kila biashara lazima wewe uwe main player lakini unaweza kutembelea migongo au nyota ya watu wengine kwa kuwekeza kwao kwenye zile biashara ambazo zinafungamana na wao moja kwa moja na ukaendelea kula share zako kwa kadri ya ulivyowekeza.
NB
Hii ni code nimewafungulia sasa unaweza ukapita nayo au ukaipita... Yesu mwenyewe alikua fundi selemala kwani unadhani hakuona kazi zingine za kufanya 😆😆😆😆
Unatakiwa ujue hatima yako kwanza... kila mtu huko hapa duniani kwa lengo maalumu na hilo lengo ndio hatima na kwenye hatima yako ndiko kuliko na bahati yako... kwa hiyo ukijua hatima yako ndio umejua asili yako na ukijua asili yako basi itakua rahisi kujua biashara zinazoendana na asili hiyo... ukishindwa ndio unafanya try and error hadi utakapojipata though hii ni very boring na inachukua muda sana kujipata.Hiyo asili yangu ya biashara ntaijuaje...?!
Baki kwenye huu uzi hadi ukimalizika kuna kitu unaweza ukatoka nacho Thread 'Dunia ni uwanja wa vita za hatima.' Dunia ni uwanja wa vita za hatima.