Naomba watu wenye uelewa wa juu wanijibu haya maswali mawili

Naomba watu wenye uelewa wa juu wanijibu haya maswali mawili

Ili nikupatie maelezo sahihi ya kisayansi kuhusu jaribio lako, nijibu maswali haya mawili:

1. Unapoweka chupa ndani ya ndoo, unaifunga kwa kifuniko kabisa, au unaiacha wazi?

2. Unapoiweka ndani ya maji, chupa imejaa maji ya moto kabisa bila nafasi ya hewa, au kuna nafasi ya hewa kati ya maji na kifuniko?
Jibu;

1. Unaifunga kabisa na mfuniko wake unabana unahakikisha hakuna maji yanayotoka wala yanayoingia ndani ya chupa

2. Chupa yako inakua imejaa maji mpaka juu ila unapoifunga utaona kuna nafasi kidogo inabakia kati ya maji na mfuniko na hii utaiona pale utapoizamisha chupa kwenye maji kunakua na kamvuke na kauwazi ndani ya chupa
 
Shida siyo swali lenyewe, shida ni maneno yako uliyounganisha kwenye swali. Maneno kama:
"Hapa nahitaji wenye akili ya kuona mambo kwa kina kirefu. Km unajijua wewe ni kilaza usijibu usichokielewa. Nataka watu makini tu wajibu haya maswali yangu." siku nyingine tafuta swali gumu ndiyo uliunganishie maneno kama haya
Ndio maana nikakwambia km hujaelewa nilichokimaanisha basi jifunze kwenye huu uzi jifunze hapo utaelewa nilikua na maana gani

Unajibu vipi maswali yasiyo na tija yanayoulizwa na wanaojiita wanasayansi ambao kwa miaka 60 ya uhuru wameshindwa kutengeneza hata kiwembe cha kunyolea mavuzi?
Kuelewa zaidi soma huu uzi nimetoa ufafanuzi nini nilichotaka ukielewe

Ndugu zangu wa kwenye uzi wa " Wazee wenzangu wa kuweka mzigo, karibuni tubashiri mechi za leo"... Njooni kwenye huu uzi tuweze kubashiri majibu..
 
Ukichukua Chupa ya lita 1 au lita 1½ ya Plastiki yenye maji ya moto let say 30/35 au 40 degrees Celsius, ukaiweka kweenye ndoo yenye maji ya lita 20 ya baridi.

Utagundua kwamba hii chupa yenye maji ya moto baada ya kuizamisha kwenye ndoo ya lita 20 yenye maji ya baridi kwanza itaenda mpaka chini sababu ya uzito halafu utaiona imepanda juu kabisa ya maji na kuanza kuelea.

Swali la kwanza; Kwanini chupa inaelea?

Lakini pia utagundua kwamba hio chupa yenye maji ya moto itakaa hapo juu ya maji ya baridi kwa kipindi fulani tu. Utafika muda hayo maji yenye moto ndani ya chupa ya lita 1 au lita 1½ yatapo na joto lake litakua sawa na maji yaliyopo kwenye ndoo ya lita 20.

Baada ya muda utaona chupa hio yenye maji ya lita 1 au lita 1½ inazama chini kabisa ya ndoo yenye maji ya lita 20.

Swali la pili; Kwanini chupa imezama?

Hapa nahitaji wenye akili ya kuona mambo kwa kina kirefu. Km unajijua wewe ni kilaza usijibu usichokielewa. Nataka watu makini tu wajibu haya maswali yangu.

Unaweza kujibu kwa kutumia Sayansi au utashi na uelewa wako wa kidunia ila tu uje kwenye jibu sahihi la kwanini?.

Karibu.
Nachangia kidooooogo! Akili yangu ni kiduchu! Swala la density! Density ya maji 1 gm/cm^. Chochote chenye density zaidi ya 1 kinazama, punguvu ya hapo kinaelea. Nami swali langu "kwa nini meli mashine kubwa inaelea?
 
Vizuri swaali lako umaweza ukalijibu au unataka tukujibu?
 
Jibu;

1. Unaifunga kabisa na mfuniko wake unabana unahakikisha hakuna maji yanayotoka wala yanayoingia ndani ya chupa

2. Chupa yako inakua imejaa maji mpaka juu ila unapoifunga utaona kuna nafasi kidogo inabakia kati ya maji na mfuniko na hii utaiona pale utapoizamisha chupa kwenye maji kunakua na kamvuke na kauwazi ndani ya chupa
Mnijibu!
 
Back
Top Bottom