Naombeni elimu kuhusu kuweka lamination kwenye vyeti vya shule na hati ya kiwanja

Sio kila post unayoona mtandaoni ina ukweli

Hizo nyaraka zako muhimu ulizozifanyia lamination unapozitumia panapohusika wamewahi kukukatalia

Watu wanafanyiwa usahili, wanathibitishwa kazini kwa vyeti vilivyokuwa laminated wanashinda kesi za viwanja kwa docs zilizo laminated

Hilo si kweli
 
Hapana, sijawahi kukataliwa ila nimeuliza ili niweze kupata elimu zaidi kwenye ili
 
Kaa na vyeti vyako mpaka vichakae, ukiweka lamination ikaja kutokea una shauri mahakamani na vyeti vinahitajika itaoneka ni feki, si vile ulivyopewa na mamlaka ya nyaraka hizo
Bongo kuna miyeyusho sana kiukweli, sijui nchi za wenzetu ikoje lakini.

Chukulia mfano hizi kadi za NIDA jinsi zinavyolalamikiwa kuchakaa haraka, na usumbufu au ligi mpaka upate ingine ikitokea kikiharibika au kupotea, huku unaambiwa ukiweka lamination hakitambuliki 😃
 
hakika kuna mstari mwembamba sana kati ya ujinga na sheria
 
acha tu mkuu, hii taarifa imenishtua sana yaaani
 
Umeeleza kwa ufasaha sana.
 
 
acha tu mkuu, hii taarifa imenishtua sana yaaani
Pengine kuna sababu lakini vyeti vina serial number, ningekuwa naweza kuwashauri watafute namna ya kuhakiki kitaalamu tu, zipo nyingi na rahisi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…