Naombeni elimu kuhusu kuweka lamination kwenye vyeti vya shule na hati ya kiwanja

Kwanini cheti kionekane kua ni fake kisa tu kina lamination wakati cheti hichi hicho kita tambuliwa kua ni halali kama hakina lamination?

Nini kinafanya cheti chenye lamination kutiliwa mashaka?
kwani mtu hawezi kufake cheti kisha asiweke lamination?
 
How so ?

Mimi nilienda ofisi za uhamiaji na doc ambayo wasnt laminated, jamaa wakaniambia I need to make it laminated first before they serve me

Uha
inategemeana na mamlaka husika wanakionaje cheti chao
 


Kwanza mahakamani huwa kuna uongo na hii ndo sababu hasa ukiwa na mgogoro Kama huo unahusu ardhi.

Mimi nakumbuka mwaka 2017 tulikuwa na Case MTU mmoja alitaka kutapeli eneo letu kama heka moja.

Ila sasa tukaenda baraza la ardhi na wakadai vielelezo kama barua n.k

Tuliandika barua na kuifanya ionekane ya zamani

Japo tulikuwa sahihi Ila ilkpelekea kuandaa barua ya mauziano na kuipeleka Katika baraza na ardhi na case ikawa imeisha na ushindi juu.


So binadamu ni matapeli Sana ni muhimu Document zako kuwa katika muundo wa kuondoa maswali.
 
pole na ongera sana mkuu
 
Mkuu bado hujajibu swali langu kwa ufasaha,
Soma tena swali langu,
Hujaweka hoja yeyote ya kisheria inayokataza kwa vyeti kuwekwa lamination,

Hope utakuja na jibu ambalo lipo wazi na linaeleweka kisheria,
 
Mkuu bado hujajibu swali langu kwa ufasaha,
Soma tena swali langu,
Hujaweka hoja yeyote ya kisheria inayokataza kwa vyeti kuwekwa lamination,

Hope utakuja na jibu ambalo lipo wazi na linaeleweka kisheria,
Sifikirii kama umeelewa nilichoandika.

Hapa Tanzania hakuna sheria inayomzuia MTU kuweka documents zake lamination Kama vyeti , hati n.k

Ila tulijaribu kumfafanulia mtoa mada mambo mbalimbali ambayo yanweza kutokea .

Ikiwa haujaelewa basi Comment yangu either IPO tofauti na ufahamu wako wa kawaida.
 
Kwa sisi ambao hatuna vyeti wala nyaraka zozote hua tunaweka lamination,
Ili wototo wa watu wasipate mimba zisizo tarajiwan.😎
 
Lamination na kuwa vyeti fake haina uhusiano ,ila usiwe kwenye kadi ya bank ,kadi ya mwendokasi ...Unaweza kupoteza uwezo wa matumizi ,zile mashine zao zinahitaji direct contact na system zao.

Vyeti havina tatizo ukiweka lamination.
 
Asante sana mkuu, changamoto yangu nimefanyia lamination document zangu zote na sikuwahi kujua kama kufanya lumination ni kosa kwenye sura ya sheria.
KUWEKA LAMINATION HAKUNA SHIDA COMRADE KWANI CHETI NI NAMBA ILIYOPO KWENYE CHETI NA SIO LILE KARATASI, KAMA UMEWEKA LAMINATION NI VIZURI SANA HIYO NI NJIA MOJAWAPO YA UTUNZAJI WA NYARAKA MUHIMU KAMA CHETI, INAPENDEZA SANA KWA KUJARI NYARAKA ZAKO. KUHUSU HABARI YA KWENDA MAHAKAMANI KWAMBA WATAKATAA KUSHUGHULIKIA JAMBO LAKO KWA KUWA VYETI VYAKO VINA LAMINATION HICHO KITU HAKIPO, MARA KIBAO TUNAENDA KU CERTIFY VYETI MAHAKAMANI NA HAKUNA HAKIMU/WAKILI ANAYEULIZIA HIYO HOJA, CHA MSINGI CHETI CHENYE LAMINATION KIWE NI HALISI.
 
Asante na nahsukuru kwa kunielezea hiki ambacho kilikuwa kinanipa mashaka makubwa.
 
Huenda hata huyo afisa aliyeongea hivyo "kwamba vyeti visiwekewe lamination", naye pia vyeti vyake vyote ukute viko laminated.
 
Hizi kadi za NIDA za sasa swala sio kuchakaa haraka. Swala ni ubora na quality ya hizo kadi tokea zikitengenezwa.

Kuna watu wanatakiwa kuwekwa ndani kwa kufanya procurement ya kiwizi namna ile.

Zile kadi za kwanza mbona ni imara sana.
 
Bado sijaelewa connection ya vyeti kuwa laminate na kushindwa kuthibitishwa kuwa ni halali ama la.

Tanzania tuna shida ya utengenezaji wa sheria kwa msingi wa utaalamu unao eleweka. Hapo unakuta kuna mtu yupo sehemu katika ofisi ya serikali ana miwani ina lenzi kali kama Microscope na frame zilizotengenezwa kwa material ya kifupa ya pembe za tembo ameshapitiliza umri wa kustaafu ana ng'ang'ania tu kuendelee na majukumu ambayo yapo nje ya uwezo wake.

Huyo ndio kaamua kuwa documents kuwa laminated ni tatizo kwake so pia iwe ni tatizo kwa kila mtu. Upuuzi mtupu.
 
haujawahi kwenda ata kwenye interview mkuu mbona watu wanaenda navyo ivyo ivyo na lamination na vinapokewa tu,na cheti kuwa OG au fake uwa hauangalii muonekano wa juu,NECTA na NACTE uwa ndo wanathibitisha kupitia data base yao ,cheti OG au fake akitambuliwi kwa kuangalia kwa macho
 
Ninachokifahamu kwenye hati,huwa haiwekwi lamination kwa sababu ukifanya hivyo unaondoa uhalali wa karatasi hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…