Naombeni elimu kuhusu kuweka lamination kwenye vyeti vya shule na hati ya kiwanja

Ninachokifahamu kwenye hati,huwa haiwekwi lamination kwa sababu ukifanya hivyo unaondoa uhalali wa karatasi hiyo
Kwa hiyo hati ikiwa na lamination inakuwa ni feki? Jamaa hebu tupe elimu juu ya hili, mimi nichojuwa hati ni namba na sio lile karatasi, cheti ni namba na sio lile karatasi.
 
Mpka sasa kupitia comments sijaona katazo la kisheria labda kama ikibidi tu wa tag wanataaluma hyo kutoka jukwaa la sheria.
 
Masheria ya Kijinga
 
Jamani nazidi kuogopa, nimeenda kuiuliza CHATGPT amekuja na aya majibu

SWALI LANGU KWA CHATGPT

Je ni kosa na hailuusiwi kufanya lamination kwenye vyeti vya kielimu pamoja na hati nyingine za kiserikali ?

ChatGPT said:​

Ndio, kwa kawaida hailuusiwi kufanya lamination kwenye vyeti vya kielimu au hati nyingine rasmi za kiserikali kama vile:
  • Cheti cha kuzaliwa
  • Kitambulisho cha taifa (NIDA)
  • Vyeti vya kuhitimu (NECTA, TCU, NACTE nk.)
  • Hati ya ndoa
  • Hati ya kiapo (affidavit)
  • Hati ya kusafiria (passport)
  • Leseni ya udereva

Sababu kuu kwa nini lamination haipendekezwi:​

  1. Huficha vipengele vya usalama (security features) – kama alama za maji (watermarks), holograms au signatures.
  2. Inaweza kuonekana kama kuficha/kubadilisha taarifa – na inaweza kufasiriwa kama kujifanya/plastic forgery.
  3. Haiwezi tena kuhalalishwa/notarized au kupewa rubber stamp – kwa sababu laminating huzuia muhuri kuingia kwenye karatasi.
  4. Mashirika mengi ya serikali na taasisi za elimu hawakubali vyeti vilivyolaminate – vinaweza kutupiliwa mbali wakati wa uhakiki (verification).

Nini kifanyike badala ya lamination?​

✅ Weka cheti kwenye plastic sleeve au file lenye uwazi kwa ajili ya kulinda bila kuharibu.
✅ Kama cheti kimeharibika, unaweza kuomba nakala mbadala (replacement) kutoka taasisi iliyokitoa.

Hitimisho:​

Ndiyo, ni kosa kwa kiwango fulani, hasa kama lengo ni kuhifadhi cheti lakini unamalizia kukifanya kisiweze kuthibitishwa rasmi tena. Ni vyema kujiepusha kabisa na lamination ya vyeti vya kielimu au hati rasmi.

​

 
Jamani wanasheria njooni mnitoe kwenye hii TANZIA YA KI-LAMINATION ambayo inanikabili ili niweze kuwa na uelewa.
 
Ukiweka nyaraka yoyote lamination tofauti na ulivyopewa basi inakua batili
 
Sidhani kama ukifanya lamination vinapoteza uhalali isipokuwa ninachokijua mimi ni kwamba ukifanyia lamination kuna wakati vyeti au nyaraka huwa zinahitajika kuwa certified/attested kwa kupigwa muhuri sasa kama umefanyia lamination hapa utakwama au itabidi ufumue lamination ili vipigwe muhuri.
Kwa mfano kama unaenda kuomba kazi nje ya nchi kwa kutumia vyeti vyako ulivyosomea Tanzania itahitajika wizara ya mambo ya nje wacertify/attest kuwa vyeti vyako ni vya halali hapo ndipo changamoto inapojitokeza.
 
Kwa ufupi sana, akiweka lamination doccs zenye muhuri wa moto hazitoonesha uhalali wa doccument.

Aweke almination docs zenye mhururi wa kawaida ila zenye muhuri wa moto asijaribu
 
Kwa ufupi sana, akiweka lamination doccs zenye muhuri wa moto hazitoonesha uhalali wa doccument.

Aweke almination docs zenye mhururi wa kawaida ila zenye muhuri wa moto asijaribu
Duh sio poa.
 
Kwa hiyo hati ikiwa na lamination inakuwa ni feki? Jamaa hebu tupe elimu juu ya hili, mimi nichojuwa hati ni namba na sio lile karatasi, cheti ni namba na sio lile karatasi.
Hapo sina maelezo mengi zaidi ya kuwa kuna siku nikiwa ofisi za ardhi na hati ikiwa katika hali isiyo nzuri sana ,kwa lengo la kubadili umiliki nikajisemea kuwa kwanini asingeiwekea lamination mpaka ichoke kiasi hiki,
Ofisa akasema haitakiwi kufanyiwa hivyo
 
ok hapo ni sawa, nimekuelewa
 
Kaa na vyeti vyako mpaka vichakae, ukiweka lamination ikaja kutokea una shauri mahakamani na vyeti vinahitajika itaoneka ni feki, si vile ulivyopewa na mamlaka ya nyaraka hizo
Sheria ipi inasema hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…