Naombeni mnisaidie kuniombea wapendwa

Wakati wa mambo magumu Mungu ndiyo anajambo lake zuri juu yako hapo mbele , kumbuka Mungu ameruhusu hilo jaribio pia atakupa njia ya kupita hilo jaribu ni muda tu utaongea
 

Nakuombea hali hiyo ikutoke usiweke hofu nayo ikakuvuruga, epuka kukaa peke yako maana shetani ndipo anawachukua kiroho na kuzipa umauti kwa kujidhuru
 
Kuna msemo unasema ukionyeshwa jambo ndotoni basi limeshatatuliwa katika ulimwengu wa kiroho
 
Sometimes kuna mambo hutokea maishani hutusogeza/huturudisha karibu na mungu.

Mtumainie mungu kweny mapito yako na mtumainie yeye baada ya mapito yako.

Hata mungu hujisikia vibaya tunapomtafuta tuu wakati tukipitia magumu, mungu anapenda sana mahusiano ya karibu na binadamu, mahusiano ya kila siku, sio tuu tunapopata shida.

Nakutakia kila la kheri na nakuombea nguvu za yesu kristo, mzaliwa wa kwanza, yeye alizumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, anayetupenda sana, akuponye, akutunze na akulinde.

Amen.
 
Leejay49 unapopitia wakati mgumu kama huu ni vizur ukajikita kusoma biblia, haswa mistari inayoupa moyo amani na Assurance.

Isaya 41:9-13
[9]wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa;
[10]usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
[11]Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.
[12]Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.
[13]Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.
 

Umeota kitu gani Leejay49 ?

Maana si kwa kuwa na hofu hivyo, kumbuka adui humjaza mtu hofu ili aweze kumshinda...
 
Mkuu ingekua vyema ungesema ni ndoto gani(ungeielezea).....Mungu akuondolee hofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…