Naombeni ushauri juu ya mtoto asiyepelekwa shule kisa hakuna ada

Ndio maana sina huo ujeuri wa kubeba mtoto, we unaelewa kwanini naomba ushauri sasa🄲
kwa maelezo yako mzazi mwenzio anaonekana ni baba bora tu sema ndio hivyo amekwama hajapenda mtoto wake akae nyumbani, kama unakipato angalau kidogo jadilianeni umchangie kidogo mtoto aende hata shule ya ada nafuu maana ada zinalipwa kwa awamu tatu nowadays sidhani kama mtashindwa watu wawili kuliko mtoto arudi kayumba mtamchanganya sana mtoto
 
Zuella zuu Kwa nini mtoto asome Private na sio Public schools?
Ikiwa mwisho wa siku wote chuo watasoma vyuo ivyo ivyo na Mishahara kazini itakuwa ni ile ile.

Tena kibaya zaidi uwezo wa kusomesha private ukawa hauna.
 
Pomoja na hilo ila nafasi yako kama mama haiwezi kupoteza, Una haki na wajibu wankuhakikisha hatma njema kwa mwanao.

Ilikuwepo sababu ya kutosha kumuachia mwenyewe apambane na mtoto labda?
Nilikiwa masomoni mtoto alikuwa mdogo, baba yake akawa hataki nirudi kusoma.. nyumbani kwetu wanataka nikasome ilikuwa mvutano mkubwa! Tulizinguana sana, Nikimsikiliza yeye kwetu wananizira wananimind, nikiwasikiliza kwetu nayeye anakaa kushoto kwaio unaelewa kilichotokea!

Mtoto alikuja kumchukua kwa kigezo cha shule, kwahiyo sikuona shida sana nikawa naenda kumuona mpaka tulivyoshindwana! Ikabidi abaki nisingeweza kuforce! Ofcource ilinila sana hii, i was traumatized! So sionkwa sababu siandiki kila kitu ndio nasheherekea hili!
 
Huu mwaka wa pili kakaa nyumbani, mbona mi mvumilivu sana jamani, hapo nakosea wapi?

Mtoto wa kiume , Miaka 8, Mwaka wa 2 yuko home. Alisoma 2024 std 1 . 2025 na 2026 hajaenda shule. Anaishi na Baba pekeyake.

For the sake of the Child.
Pambana umchukue mtoto ukae nae ww. Mwandikishe shule ya serikali.
Ila ujue tu jamaa atasusa kumlea mwanae. Ila haina jinsi shem.

Kwasasa jipange na ongea na ndugu zako wakupe support.
Ukiona uko na hali nzur na mazingira yanaruhusu.

Ndio uanze process za polisi .dawat la jinsia.

NB: hakikisha ukienda huku uwe na uwezo wa kukaa na mtoto. Maana ukienda hautashtak baba kutompeleka shule mwanae. Utaomba upewe mwanao ukae nae na umpeleke shule kwasababu baba yake ameshindwa na huu ni mwaka wa 2.
 
Sawa asante!
 
Dah sawa asante!
 
Yani huyo anasusa kila
Kitu ila kwenye swala la mtoto wake ni vita vikali, kwa kifupi nimejaribu mara kibao ata kwa kujipendekeza kumchukua dogo inashindikana!
Kwasasa jipange na ongea na ndugu zako wakupe support.
Ukiona uko na hali nzur na mazingira yanaruhusu.
Wanajua, kila mtu alishachoka, maana story ni zilezile kila mwaka
Ndio uanze process za polisi .dawat la jinsia.
Yani alishasema niende ila nikae nikijua naanzisha vita vikali sana
NB: hakikisha ukienda huku uwe na uwezo wa kukaa na mtoto. Maana ukienda hautashtak baba kutompeleka shule mwanae. Utaomba upewe mwanao ukae nae na umpeleke shule kwasababu baba yake ameshindwa na huu ni mwaka wa 2.
Hmmm hapo sasa!
 

Hata mimi nataman mtoto aendelee huko alipoanzia. Ila sasa huu ni mwaka wa 2. Anakaa home.
No way out. Na ana miaka 8. Akizembea mwaka utakatika tena alaf mwaka akiwa na miaka 9 ndio awe la 2. Mmh hapana kwa kweli.

Tena sikuhizi namba unayoandikishwa nayo std 2 ndio unaenda nayo had std 6.

Aende tu kayumba.
Mtoto akae na Mama.
Hata kwenye chumba kimoja.

Mwaka huu shem Seran pambana tu umfuate mwanao ukae nae. Na aanze std 2.
 
1. Jikubali kuwa maisha yamebadilika mfukoni na muikubali hali halisi

2. washirikishe wazazi wake na huyo mzazi mwenzako kama wapo hai au muone mtu wa heshima kwake, umshirikishe ili amshauri huyo mzazi mwenzako.

3. Kama mtoto ni wako wa kumzaa, mchukue uende umuandikishe ambayo una uwezo nayo, mtoto aendelee na masomo.

4. Baba wa huyo mtoto akilazimisha kumchomoa shuleni, nenda kwa vyombo vya sheria kama vile mamlaka za elimu ngazi yako ya kata, wilaya pamoja na mamlaka zilizopo maendeleo ya jamii.

TAHADHARI: kwenda kwako kwa mamlaka hzo usiwe na kusudi la kwenda kumtweza mzazi mwenzio na kumnanga, lakn iwe ni sehemu ya kwenda kutafuta suluhu yenye amani kwa mstakabali mwema wa mwanao.
 
Yani alishasema niende ila nikae nikijua naanzisha vita vikali sana

Kama vita ndio anataka. Anzisha tu. Unampambania mwanao.

Yuko mkoa gan?.

Alaf kabla ya kwenda dawat la jinsia. Ukienda anza kumsaka mkuu wa wilaya alaf yeye akurefer dawat la jinsia. Ili polisi waogope kuhongwa na jamaa.
 
LIKUD

Njooo utoe neno ndugu yangu.
 
Fanya namna ukae na mtoto wako, wanaume hatupo vizuri kwenye one-on-one care, hatupo vizuri hata kidogo. Malezi ya kila siku ni ya mama, baba ni overall caretaker.

Unless useme huyo jamaa hakuamini kama unaweza kuwa mlezi mzuri(unfit to raise the child).

Kwa mtu ambaye alikuwa na income ya kitosha, ghafla uchumi ukayumba, ni ngumu kuelewa kuwa picha halisi ni AMEFILISIKA, anahitaji mda. Huo mda haupo kwa ajili ya mtoto, so the best possible way ni kuchukua mtoto, mpeleke shule za kwaida, or else mpeleke shule unayoweza kuimudu.

Huwa nasema, hakuna kosa kubwa kama kulea watoto namna hii, you swing the kid here and there na mwisho wake mtoto anakuwa na psychological issues.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…