Naombeni ushauri juu ya mtoto asiyepelekwa shule kisa hakuna ada

Sasa hivi umejipata?? If yes nenda nae mahakamani dai mtoto wako upambane nae mwenyeww,
Wanaume wana ujinga mwingi na huyo mtoto akiwa mbumbumbu lawama zitarudi kwako hata kama hauishi nae, na hilo suala
La mtoto kukosa masomo ndo iwe sababu no moja kokote uendako.
Mtoto mjinga ni mzigo wa mama siku zote.
 
Pole sana aisee, ila jipe moyo si kwamba Baba hampendi mtoto ila ndio hivyo nyakati hazilingani.
Uwezo wa kufanya atakavyo yeye Baba kwako wewe bado haujafikia na hata kama ingekuwa hivyo pengine angekataa msaada wako.
Katika hali ya kawaida huwezi kukaa na amani hata wakati mmoja,na kinachouma zaidi huna la kufanya, lakini pia darasa la pili kwa sasa ni darasa la mtihani , kuchelewa Sana anaweza kubakia hapo darasa la pili mwakani!
Inauma na kuumiza
Wakati ukijiuliza ufanye nini jua pia jitihada haizidi kudra, muombe Mungu akupe njia sahihi ikiwemo kuufanya moyo wa Baba mtoto uwe mwepesi, pia kumjalia Baba mtoto kipato aweze kumpeleka shule mtoto.

Lakini zingatia Sana maoni ya walio kuambaia uwende serikalini, huko hakika njia nyepesi ya haraka utalipata.

Pole sana na ujaliwe iwe heri kwako Baba na mtoto.
 
Serani pole,,,
Miaka 8 mtoto anatakiwa awe standard 3 au 4....
Grade 2 hizo ni chekechekea huko ems. Na hii Ina maana Kuna uzembe mkubwa katika malezi ya huyo mtoto
Halafu we Bado mdogo etii???? Huyo mtt ananganganiwa sababu baba anataka mahusiano na anajua utamrudia kwa kigezo cha huyo mtoto.
Kama kweli mtoto ni wako..... Nenda polisi dawati la jinsia ni lazima watakupa huyo mtoto. Kwa sababu kwa maelezo hayo Kuna makosa mengi ya kimalezi.
Somesha huyo mtoto kwa kipato chako.
 
Amen! Amen asante 🙏🏽❤️
 
Mtoto jinsia gani
 
Wabheja dada! Nitafanyia kazi huu ushauri, huyo baba mtoto huwa hatuna mawasiliano kabisa, ni mara moja sana where necessary inaweza kupita mwaka hatujaongea, so uwezekano wa kurudiana haupo kabisa! Nina ego ana super ego, kwahiyo amebaki mtoto tu katikati hapo ndio huyo anatamani ata nisiwepo katika maisha yao tena na ni kitu ambacho hakiwezekani lazima nihesabu nina mtoto sehemu! Ila yeye anafanya kama kukomesha hivi at the end anamuumiza mtoto! Kuhusu kumchukua nimejaribu mno iko complicated kuanzia ground ila ntapambana tu!
 
Seran kama uwezo wa kukaa na mtoto unao. Fanya ujasusi 😁😁😁 .

Hamia sehem nyingne. Kimya kimya. Muombe mtoto Pasaka ukae nae kwa bibi yake. (Mama yako) . Akifika unamchukua unampeleka ulipohamia na unamuandikisha shule.

Muache Baba mtoto ndio akutafute ww sasa. 😁😁😁😁.

All in all Pigana vita kiakili.
 
Mama yangu anasafiri sana so home habaki mtu, labda nijipange mwenyew, nilishauriwa na rafkiangu tukamuibe ila wakasema huwa ni case mbaya sana nikaogopa🙆🏽‍♀️
 
majibu yake yananikwaza sana sijui kwanini hata kaleta hii topic huku, kila anachoshauliwa anakazana baba mbishi hivi kuna mbishi mbele ya sheria??
Hivi huonagi wamama wanavopambania watoto wao hadi kuamua kuomba msaada hadi kwenye ma tv???
Na huyo mwanaume ashajua ushaifu wako anataka akunyooshe kupitia mtoto sasa mchekew uharibu future ya mwanao!
 
Mama yangu anasafiri sana so home habaki mtu, labda nijipange mwenyew, nilishauriwa na rafkiangu tukamuibe ila wakasema huwa ni case mbaya sana nikaogopa🙆🏽‍♀️

Hakuna case hapo.

Humuibi . Anakuja likizo kumsalimia bibi. Akija ndio harud tena kwa baba yake.

Mwaka 2010 . Mm niliwah kwenda mchukua mtoto wa dada angu kwa mwanaume walioachana nae.alikuwa hatak mtoto akae na mama yake. Tukasema bibi anamhitak mtoto sikukuu hii. Jamaa akakubali.
Mtoto Alikuwa na 5 yrs. Hakuwah kurud tena kwa baba yake. Now anamalizia chuo. Na miaka yote anakaa kwa Bibi.
(Too bad dada akifariki, jukumu la kumlea toka akiwa form 1 ni sisi wajomba) na tumeweza .

Kwahiyo omba msaada kwa ndugu wawil.watatu ambao unahisi wanauwezo wa kukusaidia.

Kaa na mwanao. Acha jamaa ndio akutafute.
Kwa namna yoyote ile dogo aanze shule mwaka huu. Na ukae nae.
 
Aww asantee! Ngoja nifanye hivi maana hii hali si mchezo.. ni ngumu ila ntajichetua tu
 
Bado hajawa tayari,, ninachojua Mimi katika kitengo kinawashughulikia masuala vizuri ni dawati la jinsia na hawarembi.
Akiwa tayari atachukua hatua
Sawa,,, pambania mwanao utakapokuwa tayari.
 
Kisheria mzazi anatakiwa kumuhudumia mtoto kwa kufuata mahitaji manne. Elimu ikiwa mojawapo ikatokea mzazi kwa makusudi akamnyima mtoto kimojawapo mzazi anaweza shikiliwa kisheria na kutakiwa kutimiza majukumu yake.

Shauri litaanzia level ya chini na linaweza kupanda mpaka mahakamani endapo baba atakua anagomea kutoa matumizi kwa makusudi.

Shauri laweza anzia ofisi ya kata au ya Ustawi wa Jamii na litapiga hatua kwenda mbele endapo kutakua na sintofahamu kwa level utayoanzia.

Kijiweni ningesema ditch mtoto kwa ndugu upande wa baba.
 
Thanks sana, ntalifanyia kazi 🤝🏽
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…