Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

sema na yy ndo anaona kuingia kanisa la Roma ni Kama dhambi jmn
Ndo ujue kwamba ni mbinafsi.
Mbona wewe hujaona kuingia kanisa la wasabato ni dhambi?

Mwambie kwamba hata kuoa mkatoliki ni dhambi akaoe msabato mwenzake. Ila ndo hivyo huwezi kumwambia..
Najua utaishia kuwa msabato kwa mapenzi uliyo nayo juu yake. Hapa tunapoteza muda kukushauri.
 
Mm Sina haja na yy kunifuata na stk ivyo ninachotaka kila mtu asali kivyake bhc
 

Ndoa ili iwe na furaha itahitaji mambo makuu matatu
1. Upendo
2. Akili. Kuelewana. Hekima na busara.
3. Imani.
Hayo mambo matatu lazima mfananane. Ili muweze kuishi kwa furaha na kulea watoto wenu wawe kizazi Bora.

Kikipungua chochote hapo ni bora kuachana mapema.

Hakunaga ndoa ya serikali. Kama kila mmoja hataki kuamini imani ya mwenzake tafsiri yake hapo hakuna familia itakayoanzishwa.
 
Sikushauri ufunge ya serikali,utawatesa sana watoto watashindwa wafate Dini ipi,ya baba au ya mama.

Ushauri wangu,sioni shida wewe kuwa msabato kama kweli unampenda mchumba wako,sioni ugumu hapo kwa sababu wote ni waabudu Kristu.
 
Duh🥺
 
Kwa ufupi kabisa na kwa msisitizo.
Ni wanaume wachache sana wanakubaliana na takwa lako. Yaani wewe uanze kum-control mumeo mapema tu hivyo? Yeye kapanga kufunga ndoa ya kanisani, wewe unataka umbadilishie utaratibu wake mfunge ndoa ya serikali. Sasa nani kichwa cha familia yenu? Ni wewe au mumeo? Unaelewa maana ya kichwa cha familia? Wewe unatafuta kuanza kumtawala mumeo mapema kabisa.


Nakushauri, kama huwezi kuwa msabato, vunja huo uchumba. Tafuta mkatoloki mwenzio mfunge ndoa. Afu katoliki nfo dhehebu la wakristo wengi huwezi kukosa mchumba in huko.

Hivi unajua changamoto wanazopata wale ambao wanapeana uhuru wa mke kwenda kanisa analotaka?
 
Sikushauri ufunge ya serikali,utawatesa sana watoto watashindwa wafate Dini ipi,ya baba au ya mama.

Ushauri wangu,sioni shida wewe kuwa msabato kama kweli unampenda mchumba wako,sioni ugumu hapo kwa sababu wote ni waabudu Kristu.
Tatz kila mtu amelelewa kwenye misingi ya dhehebu lake na usichukulie poa labda Kama hujawai kukutana na ii changamoto...na sio Kama napenda nataman iwe rhc ivyo kwangu lakn moyo ndo unanisaliti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…