Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Yani mm sikuwai lijuaga ili dhehebu namna lilivyo..na at first nilishamkatalia akaniambia kuwa ya serikali tutafunga ili kila mtu abaki na dini yake lakini alipoanza kuwa serious na haya Mambo ndo amenigeuka anasema hataki ata kusikia inabd mm nimfate yeye
Mnadetije miaka 6 bila ku rule-out mambo sensitive kama haya?

Kuna mambo huwa inabidi yawekwe kwenye mstari mwanzo kabisa wa mahusiano...
 
Sijui, ndo naomba unijuze
Baadhi.

1. Watoto kukosa mwelekeo
2. Kukosekana kwa imani katika ndoa. Yaani mumeo anaweza kuhisi wewe unachepuka huko kanisani kwenu maana unaenda peke yako. Chukulia mfano, yeye awahi kurudi kabla yako.
3. Migogoro katika ndoa haitaisha. Masuala ya vyakula, mavazi, sadaka na michango kanisani itawagombanisha.

4. Kupungua heshima. Unasema umeolewa lakini mumeo/mkeo haendi kanisa hilo. Yaani inaonyesha ndoa yenu hamsikilizani.

5. Watoto kukosa amani. Mnawagawa watoto. Yaani ukiona mtoto anakosea unamwambia hayo huwa anafundishwa kanisani kwao (ambako wewe huendi).

6. Ugomvi hauishi katika ndoa. Ukisikia watu wanasema huyu mke hamsikilizi mtu isipokuwa mchungaji/padri ujue ni kwa sababu ya kutengana makanisa.

Yako mengi mno matatizo ya hawa.
 
Ndoa ili iwe na furaha itahitaji mambo makuu matatu
1. Upendo
2. Akili. Kuelewana. Hekima na busara.
3. Imani.
Hayo mambo matatu lazima mfananane. Ili muweze kuishi kwa furaha na kulea watoto wenu wawe kizazi Bora.

Kikipungua chochote hapo ni bora kuachana mapema.

Hakunaga ndoa ya serikali. Kama kila mmoja hataki kuamini imani ya mwenzake tafsiri yake hapo hakuna familia itakayoanzishwa.
Ushauri mzuri huu,fuata huu mtoa mada
 
Baadhi.

1. Watoto kukosa mwelekeo
2. Kukosekana kwa imani katika ndoa. Yaani mumeo anaweza kuhisi wewe unachepuka huko kanisani kwenu maana unaenda peke yako. Chukulia mfano, yeye awahi kurudi kabla yako.
3. Migogoro katika ndoa haitaisha. Masuala ya vyakula, mavazi, sadaka na michango kanisani itawagombanisha.

4. Kupungua heshima. Unasema umeolewa lakini mumeo/mkeo haendi kanisa hilo. Yaani inaonyesha ndoa yenu hamsikilizani.

5. Watoto kukosa amani. Mnawagawa watoto. Yaani ukiona mtoto anakosea unamwambia hayo huwa anafundishwa kanisani kwao (ambako wewe huendi).

6. Ugomvi hauishi katika ndoa. Ukisikia watu wanasema huyu mke hamsikilizi mtu isipokuwa mchungaji/padri ujue ni kwa sababu ya kutengana makanisa.

Yako mengi mno matatizo ya hawa.
Asante Sana...nitafanya maamuzi Kama ni kusuka au kunyoa
 
Habari zenu wapendwa.

Mimi ni binti wa miaka 24. Niko kwenye mahusiano na mchumba wangu ni miaka 6 Sasa tunaenda na ninampenda Sana mwanaume wangu.

Shida ya kuja hapa naombeni ushauri anataka kunioa ila changamoto inakuja upande wa dhehebu kwenye kubadili mimi napata ukakasi sana sijui kwanini, mimi ni mkatoliki pure na yeye ni msabato pure(kurya) mm sijawai dharau Imani yake ni vile tu nimelelewa kwenye misingi ya dini yangu. Anachotaka yeye ni ndoa ya kanisani na mm napata ugumu kubadili.

Nimejaribu kumshauri tufunge ya Serikali na watoto watakufata yeye lkn hatqki anataka ya kanisani. Mimi moyo wangu umekuwa mzito sijui kwanini na najiona sina amani kwenye huu uamuzi ambao nitafanya kumridhisha yeye sababu nampenda.

Nifanyeje🥺
Mungu ni mmoja hayo madhehebu yapo duniani tu acha kupoteza muda ndugu kama mnapendana kafunge ndoa kwake maisha yaendele miaka6 yote bado hamjafikia mamuzi tu.
 
🙌 Hatari...ni kweli usemacho🙏

Usiwaze kuhusu kufunga Ndoa.
Waza utaishije ndani na Ndoa. Hiyo ndio hoja.

Upendo, imani na Akili. Kama mnatofautiana pakubwa hapo ni bora uachane nako huko. Utalia sana.

Kaa naye, muulize kwa nini hataki awe mkatoliki, aje na hoja. Kisha na wewe useme kwa nini hutaki kuwa Msabato uende na hoja.

Hakikisha hoja zenu zote zijikite kwenye kitabu mnachokiamini, iwe ni Biblia.
Kila hoja itakayotolewa msingi wake mkuu iwe ni Biblia.
Sio maoni ya mchungaji, padri, papa, Kuhani, askofu, au mzee wa kanisa au Mzazi. Bali chochote kitakachojadiliwa kitokee kwenye biblia na mifano.

Sio umlaumu mwenzako wakati bado hamjajadili jambo hili.
 
Nimeshaongea nae kila kitu na kwa namna niwezavyo lkn hataki..afu kinachonishàgaza sio ata mtu wa kanisani enda yake ya Mara moja au mbili kwa mwaka..Ila tu nyumban kwao baba yake ni mchungaji wa kanisa nahisi ndo Mana inakuwa hivi
Imani ni mapokeo. Yeye haendi kabisani kila siku lakini ana mapokeo ya kisabato. .

Kifupi combination ya msabato na mkatoliki ni ngumu sana, endapo mmoja badili dhehebu. Itawasumbua

Ingekuwa madhehebu mengine ya kikristo huwa ni fasta kidogo.

Yaani mkatoliki kwenda madhehebu nje na msabato ni rahisi sana.
 
I wish iwe hivyo pia... Vipi kuhusu watoto? Haiwapi changamoto??
Hakuna changamoto, tumewalea katika misingi ya biblia. Wote wamekua wakatoliki, but siku nyingine tunaenda wote usabatoni kusali, siku zingine tunaenda RC. Mungu ni yule yule, Kristu ni yule yule, kinachotuunganisha zaidi ni biblia. I guess it comes down to the two of you.
 
Usiwaze kuhusu kufunga Ndoa.
Waza utaishije ndani na Ndoa. Hiyo ndio hoja.

Upendo, imani na Akili. Kama mnatofautiana pakubwa hapo ni bora uachane nako huko. Utalia sana.

Kaa naye, muulize kwa nini hataki awe mkatoliki, aje na hoja. Kisha na wewe useme kwa nini hutaki kuwa Msabato uende na hoja.

Hakikisha hoja zenu zote zijikite kwenye kitabu mnachokiamini, iwe ni Biblia.
Kila hoja itakayotolewa msingi wake mkuu iwe ni Biblia.
Sio maoni ya mchungaji, padri, papa, Kuhani, askofu, au mzee wa kanisa au Mzazi. Bali chochote kitakachojadiliwa kitokee kwenye biblia na mifano.

Sio umlaumu mwenzako wakati bado hamjajadili jambo hili.
Asante Sana
 
Sasa jamani: Ulivyoanza kudate hukujua ni dhehebu tofauti au hamkua na mpango wowote, mpango umekuja katikati?

Ni ubinafsi kutaka mwenzio abadili ikiwa wewe hutaki kufanya hivyo, nadhani nzuri ni ile kila mtu awe tayari kubadili then mmoja anaamua kuvolunteer.

I am afraid mmeanza kushindana kwenye kitu kidogo sana.

Halafu suala la madhehebu liko serious kiasi hiko eenhe??
 
Imani ni mapokeo. Yeye haendi kabisani kila siku lakini ana mapokeo ya kisabato. .

Kifupi combination ya msabato na mkatoliki ni ngumu sana, endapo mmoja badili dhehebu. Itawasumbua

Ingekuwa madhehebu mengine ya kikristo huwa ni fasta kidogo.

Yaani mkatoliki kwenda madhehebu nje na msabato ni rahisi sana.
Ni kwel kabisaa
 
Rc hamna ndoa ya mseto Kati ya mkatoliki na msabato... Ipo Kati ya Rc na KKT, Rc na Moravian, Rc na Anglican... Lkn yy hataki anataka nifate vile anavyotaka yy
Ndoa ya mseto si unafunga na mtu wa dini nyingine (mkristo na muslim) ukifunga na madhehebu mingine ya kikristo ukiacha sabato haitwi ndoa ya mseto.
 
Tafuta mkatoliki mwenzio binti. Unataka kwenda kwenye ndoa ambayo hata hutaki kujua watoto wako wanaendaje kanisani? Yaani ukazae watoto halafu huna time nao kuhusu issue za kanisa!

Halafu huna freedom ya masuala ya mapishi? Wewe utanunua chakula flani, mumeo atasema hicho chakula usipikie hapa. Utafanyaje?

Kifupi, kwenye ndoa inataka watu mna mtazamo unaofanana kiimani na kijamii.
Safi sana.
 
Asante Sana...nitafanya maamuzi Kama ni kusuka au kunyoa
Mshirikishe Mungu kwenye maamuzi yako. Take time.

Btw, you're still too young. Usije tu ukaamua kwa kuchukulia kigezo kuwa ni rahisi sana kupata mchumba sahihi.
 
Back
Top Bottom