Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Hapana mm sijamtaka yeye abadili ninachotaka Mimi kila mtu abaki na Imani yake
Sasa jamani: Ulivyoanza kudate hukujua ni dhehebu tofauti au hamkua na mpango wowote, mpango umekuja katikati?

Ni ubinafsi kutaka mwenzio abadili ikiwa wewe hutaki kufanya hivyo, nadhani nzuri ni ile kila mtu awe tayari kubadili then mmoja anaamua kuvolunteer.

I am afraid mmeanza kushindana kwenye kitu kidogo sana.

Halafu suala la madhehebu liko serious kiasi hiko eenhe??
 
Nakuambia.
Ukisikia Watu wengi wakisema ndoa ndoano hicho ndicho nilichoeleza.
Mtu hamfanani alafu unalazimisha kuanzishwa familia.

Unajua maana ya familià?
Familia ni kuwa kitu kimoja.
Sasa huyu anaimani hii, yule anaile, huyu anaelewa hivi yule anaelewa vile.
Huyu ndiyo yake ni hii, mwingine ndoto yake ni ile. Hapo ni machafuko hakuna familia.

Usabato au Ukatoliki haufanyi ndoa iwe na furaha. Ila mkiwa na imani sawa kumhusu Mungu hapo ndoa lazima iwe na furaha.

Wasabato wanaamini, siku ya ibada ni Sabato, jumamosi. Wakatoliki hamuamini. Wasabato hawaamini katika Kuombea marehemu, wakatoliki mnaamini. Wasabato hawaamini katika sala ya Mama Maria, wakatoliki wanaamini.
Wasabato hawali nguruwe, Wakatoliki mnakula.
Hivi hapo kuna familia kweli?

Mtakuwa pamoja kweli? Mtaweza kulea watoto au ndio mtawachanganya au kuwaacha walelewe na ulimwengu?

Kama ni mimi nashauri achaneni ikiwa kila mmoja amebaki kwenye ubinafsi wake.
Na isitokee yeyote akahamia kwa mwenzake kinafiki. Huko ndio kubaya zaidi.
Asante
 
Hakuna changamoto, tumewalea katika misingi ya biblia. Wote wamekua wakatoliki, but siku nyingine tunaenda wote usabatoni kusali, siku zingine tunaenda RC. Mungu ni yule yule, Kristu ni yule yule, kinachotuunganisha zaidi ni biblia. I guess it comes down to the two of you.
Wow...hii ni nzuri sana
 
Hakuna changamoto, tumewalea katika misingi ya biblia. Wote wamekua wakatoliki, but siku nyingine tunaenda wote usabatoni kusali, siku zingine tunaenda RC. Mungu ni yule yule, Kristu ni yule yule, kinachotuunganisha zaidi ni biblia. I guess it comes down to the two of you.
Wow...hii ni nzuri
 
Ndo ujue kwamba ni mbinafsi.
Mbona wewe hujaona kuingia kanisa la wasabato ni dhambi?

Mwambie kwamba hata kuoa mkatoliki ni dhambi akaoe msabato mwenzake. Ila ndo hivyo huwezi kumwambia..
Najua utaishia kuwa msabato kwa mapenzi uliyo nayo juu yake. Hapa tunapoteza muda kukushauri.
Hapana kipenzi usiseme hivyo jamani, still naangalia maoni yenu then nimshirikishe Mungu zaidi ili niamue maamuzi mazuri ambayo nitakuwa na amani siku zote za maisha yangu
 
Ni changamoto
Huo mstari wa mwisho,Sasa mama atawafundisha watoto Nini wakati Dini ya baba haijui? Kumbuka mlezi mkuu wa watoto ni mama.Mfano huyo dada ni mkatoliki ,katika ukatiloki kuna stages mfano,kubatiza watoto wakiwa bado wachanga,komunio,na kipaimara lkn kwa wasabato hiyo hamna.

Sasa nani atawasimamia Hawa watoto katika misingi ya Dini?
Ndio maana ni vizuri sana kuoana watu wa dhehebu Moja,na ikiwa mmependana madhehebu tofauti ni lazima mmoja afate Dini ya mwenzake(,Hasa mwanamke).

Ndio maana siku huzi unakuta familia Moja lakn watoto wana Dini tofauti.
 
Ndoa ili iwe na furaha itahitaji mambo makuu matatu
1. Upendo
2. Akili. Kuelewana. Hekima na busara.
3. Imani.
Hayo mambo matatu lazima mfananane. Ili muweze kuishi kwa furaha na kulea watoto wenu wawe kizazi Bora.

Kikipungua chochote hapo ni bora kuachana mapema.

Hakunaga ndoa ya serikali. Kama kila mmoja hataki kuamini imani ya mwenzake tafsiri yake hapo hakuna familia itakayoanzishwa.
ulikosea kuzipanga mkuu nimerekebisha😀
1.AKILI
2.UPENDO
3.IMANI
 
ukijifunza misingi ya BIBLIA vizuri nakuhakikishia lazima utafuata misingi ya SABATO.....
kua na madhehebu tofauti kwenye dini moja huo sio mpango wa Mungu halafu SABATO sio dhehebu
 
Hakuna ndoa inakaa vizuri kwa mama kusali A na baba kusali B. Amua kama kweli unataka kuishi maisha safi ya ndoa, mfuate mume wako, hakuna mwanaume anajielewa akafuata dini/dhehebu la mkewe.
 
Ushauri

1. Wengine tunaishi bila hizo Ndoa na tunaishi kwa furaha.
Ndoa kwa muktadha wa sasa ni kuruhusu kutawaliwa na external forces kama Mila, dini, na serikali.
Funga ndoa baadaye sana kwa maslahi ya mkeo au mumeo kupata haki zake pale siku usipokuwepo.. ishini walau miaka 20 huko ndio mfunge Ndoa.

2. Angalieni mazuri yaliyopo katika dini hizo mbili. Usabato na ukatoliki ndio yawe muongozo wa kulea watoto wenu.
Kila dini inamazuri na mabaya yake.
Jiangalieni ninyi wenyewé, kuona nani yupo vizuri kwenye sekta fulani ndio apewe kuifanyia kazi kuwalea hao watoto. Mfano, kama Mke unajua zaidi biblia basi mumeo ndio akuachie kazi ya kuwafundisha watoto lakini naye akijifunza. Yaani shirikianeni.

3. Msiruhusu external forces ikiwemo wazazi, jamii, dini kuongoza Familia yenu.

4. Tumieni kitabu mtakachoona kinawafaa kama ni Biblia kiwe ndio mwongozo wenu.
Hapo hakuna cha usabato wala Ukatoliki wala ulutheri. Hayo madhehebu hayapo kwenye hivyo vitabu ila yalianzishwa na Wanaume na wanawake kama mlivyo ninyi. Hivyo ohata ninyi mnaweza kuanzisha dhehebu lenu.

Mimi sikumshauri mwenza wangu abadili dini na wala sikutaka ajue dhehebu langu na hata sisemi najivunia yeye kunifuata kwani dhehebu kwangu has nothing to do kwenye mapenzi na kuongoza familia yangu. Muongozo upo kwenye Biblia.
Biblia haina Ukatoliki wala usabato. Biblia ni kitabu kikuu cha kuongoza wanadamu. Muhammad alitumia vitabu vya biblia kuunda dini yake ya uislamu.
Nanyi mnaweza kutumia biblia na quran kuunda dhehebu lenu.

5. Mnapotatua matatizo yenu makubwa na madogo kama hili la kutofautiana mtazamo kuhusu nani abadili dini. Msipende kushirikisha Watu. Wala msipende kufanya reference Kwa kuangalia mlipotoka bali angalieni maslahi yenu ninyi wawili na wapi mnataka kwenda.

6. Mtu akifafanua biblia au Quran asiweke mawazo yake mwenyewe bali aache biblia yenyewe ijisemee yenyewe.

7. Ndoa inajengwa na watu wawili tuu walioamua kupendana, kuwa kitu kimoja, na kuanzisha maisha yake.
 
Yani mm sikuwai lijuaga ili dhehebu namna lilivyo..na at first nilishamkatalia akaniambia kuwa ya serikali tutafunga ili kila mtu abaki na dini yake lakini alipoanza kuwa serious na haya Mambo ndo amenigeuka anasema hataki ata kusikia inabd mm nimfate yeye
Kama yeye ndiyo kageuka makubaliano bado all cards rests on you.....

Mkumbushe kuhusu makubaliano yenu, kama ataendelea kukaza shingo basi chukua maamuzi unayoona yanafaa kwako..

Japokuwa, dini kwa mwanamke sio kitu kikubwa sana, as long as huyo jamaa unaona anafaa kuwa baba wa wanao na mumeo, basi mfuate kwa kila kitu including dini..
 
Back
Top Bottom