Naombeni ushauri, namuokoa vipi mwanangu wa miaka minne na kumkinga katika Hali hiii. Ni hivi, Leo nilikuwa nyumbani, na toka asubuhi nilikuwa nae nikicheza nae .
Sasa katika ongea ongea kaniambia Jambo lililonishtua kidogo. Ameniambia watoto wadogo wawili wa pale mtaani wamedakana. Na nilipouuliza kudakana ndio Nini akasema walienda kwenye migomba wakavua nguo na kudakana.
Kwa jinsi alivyoongea,Mimi nimeelewa kuwa hao watoto walifanya mapenzi japo yeye anasema walidakana. Haraka haraka nimejua kuwa lazima Kuna mtu kamwambia kitendo kile ni kudakana .
Kinachonitisha zaidi watoto anaosema wamedakana ni watoto wadogo wachekechea.
Kwa umri wake kuanza kuongea au kusikia Mambo Kama hayo naona Kama sio sawa.
Naombeni ushauri katika mazingira Kama haya namsaidia vipi mwanangu , na pili namweka vipi mbali na hao watoto wengine pasipo kuleta athari. Japo najua kumtenga sio dawa, maana hawezi kuishi ndani peke yake. Tushauriane katika malezi,kwenye Jambo Kama hili unafanyaje kumuokoa mwanao wa kike.
Kwa mtoto wa kike ni hatari ukizingatia ni mtaani hapo. Nadhani kupunguza madhara ni kuzungumza na wazazi wa watoto wote hao mtafute suluhisho kwa pamoja. Kumtenga mwanao peke yake haitosaidia zaidi, chukua wazazi wote wajulishwe na wawaonye vikali watoto wote ikiwezekana na adhabu juu kwa hao waliodakana. Na mjue hayo mambo wamejifunzia wapi mzuie. Kama uko uswahilini sana kazi ya ziada unayo, kuwa strict ukiwa unamfundisha naona mara nyingi kunasaidia. Sio unakuwa strict kimyakimya atakulia timing akitoka aharibikie bweni au chuo.
Angekuwa mtoto wa kiume kwake yeye hamna athari sana kuliko wa kike. Mapenzi mimi nilijifunza kwenye movies hasa za Kihindi, nikiwa awali nikawa napewa kisses na kukubatiwa na dogo mwenzangu, huyo baadae aliacha shule akiwa form 2 kama dada yake na aliolewa, first born wake ni wa kiume alimuita jina la ex wake wa mtaani kwetu.
Darasa la pili nikamwandikia Karen barua ya mapenzi nikaandika I love you so much kwa kukosea spelling hakuelewa sababu nilikuwa mjanja sana next level, akaenda kuuliza nikakamatwa na fimbo juu. Baadae madarasa ya juu tukawa tunafanya kitoto, hakuwa stricted kabisa nyumbani kwao.
Form one nikatongoza demu wa kwanza kumbe ni HIV+. Nikampanga, kuna rafiki yangu Rama (RIP) akatuona tunajifichaficha tunaongea tunafurahi akanidokeza. Huyo binti alikuwa mzuri na hakuwa analindwa sana nyumbani, sadly akaambukizwa na mwalimu wake wa primary. Sasa hivi ni mlokole fake ila anapanga wanaume.
Kutokana na kuokolewa dakika za mwisho, nikaachana na mapenzi nikawa muoga. Baadae nikaanza kutumia kinga mpaka siku nimebakiza moja na demu wangu akaja hapo tupo Form 4 nikaonja bila kinga nikajilaumu sana siku zote nilikuwa wapi. Huyo demu wangu alifariki, inaaminiwa na wote kwamba alirogwa na ndugu yake wa kambo.
Karen kwa sasa ana watoto wawili kila mmoja na baba yake ndani ya miaka miwili. Nikabaki mimi, mapenzi hayanitishi nimepitia mtaa mgumu kutoboa marafiki zangu wa utotoni wote wamezaa kiholela.
Nimeanzia mbali sana ila uswahilini kuna maisha mabovu sana kwa watoto hasa kama wazazi wenyewe kama ni oyaoya siku zisonge. We unategemea nini wazazi shule zinafunguliwa wanafurahi watoto waende kupambana na walimu wazazi wenyewe wapumzike.