Mambo vipi. Nimepitia yote uliyoandika na nilichoelewa ni kwamba unahitaji kufanya
Career Change uingie kwenye
Tech Industry. Sijui kama nitakuwa nimekosea, ila kama ni kweli, utakuwa umefanya maamuzi mazuri sana.
Mwaka 2022 nikiwa na miaka 28 nilikuwa katika situation kama yako. Nilikuwa nahitaji kufanya career change pia kuingia kwenye Tech kutokea fani ya
Electrical Engineering. Japokuwa nilikuwa nishapata kazi tayari kama electrical engineer, ila sikuacha hii ndoto inipite. Niliamua nijifunze
Web Development kipengele cha
Frontend Development tu, na nashukuru mungu, ndani ya
miezi 8 nilimaliza
course zote zinazohitajika. Hivi sasa ni
Frontend Developer, na naipenda sana kazi yangu. NB: Sikusoma kwa hao
ALX, ndio mara ya kwanza nimewasikia humu.
Ukiwa kama mtu unayeamua
kubadili fani, ni vema sana kutumia muda kufikiri mara mbili ni kitu gani kilichokuvutia mpaka
uhamie upande wa pili. Asilimia kubwa huwa ni
fursa na
maslahi mazuri. Wengine hufanya kwa sababu wanapenda tu kuwa na
ujuzi tofauti. Pia ni sawa.
Kadiri nilivyosoma uliyoandika, sidhani kama nitakuwa nimekosea kukuweka kwenye kipengele cha fursa na maslahii mazuri. Ni kweli fursa ni nyingi na maslahi ni mazuri sana kwenye Tech. Mimi ni shuhuda. Nilifanya
remote internship kwa
miezi 6 mwanzoni mwa
2023, fedha niliyokuwa nalipwa, ilikuwa nzuri sana
. Changamoto pekee kwenye Tech ni safari ya
kujifunza yataka moyo sana na kutokukata tamaa. Utakutana na mdudu anaitwa
BUGS (developers wanaelewa). Ila mwisho wa siku kila kitu huwa poa.
Hivyo ufuatao ndio
ushauri wangu ili usibaki unasoma course nyingi nyingi ambazo sio milango mizuri sana kuingia kwenye Tech:
- Tafuta mlango mwepesi ila wa uhakika wa kuingia kwenye Tech. Mimi nilichagua Web Development. Ina category tatu, ila nikaamua kujifunza tu Frontend Development. Zingine ni Backend Development na Full Stack ( FD + BD). Sijajua App Development kama ni mlango mwepesi, watakupa mwongozo wataalam.
- Tumia sana course za Udemy. Udemy ni mtandao wangu pendwa kujifunza course yoyote maana kuna videos ambazo unajifunza wewe kwa wakati wako. Japo ni ya kulipia ila kuna namna ya kupata hizo course for free kwenye torrent sites au site zingine zinazovujisha.
- Kujifunza vitu vingi online ni FREE. Sidhani kama ni wazo zuri kulipia hiyo course unayotaka kuisoma wakati unaweza kuipata course ya topic hiyo hiyo for free na ukasoma kwa muda unaotaka wewe. Kampuni zingine zinaishi kwa kuuza tu courses au kufanya tu semina, ndio maana wameanza kukushauri usome na zingine zaidi toka kwao.
- Data analyis sidhani kama ni Tech ila Data Science ni Tech( japo sidhani kama ni mlango mwepesi). Wataalam watakupa mwongozo. Soma hii link ...data analysis is not typically classified as an IT (Information Technology) job...
- Umri sio kigezo kabisa linapokuja swala la kujifunza ujuzi mpya. Watu wa umri tofauti tofauti hujifunza vitu vipya. Usikatishwe tamaa kwamba umri umeenda.
Kila la kheri katika kufanya maamuzi. Ukiwa na maswali uliza na usikatishwe tamaa na mtu yoyote.
🙂