Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Usinywe pombe au kuvuta bangi kisa watu wanaokuzunguka utaharibikiwa kuliko wao. Mie mwenyewe mchaga ila sinywi pombe na ma group hayajawahigi kunishawishi just be you. Pia hivi ni lazima uende kwenye ma club?
Ku-hangout na washkaji.... Weekend nyingi lazima kuna mtu atapendekeza twende sehemu flani tukale bata....
 
Rafiki yangu,
Pombe,Bangi,Sigara,Shisha na Starehe yoyote ile ambayo ni Addictive kwa Umri wako huo Ni hatari.Usidnagnyike wanaposema hairuhusiwi kwa wenye umri wa miaka 18 ukafikiri kwa sababu una 19 unaruhusiwa.

Ushauri wangu kama Unaweza kuamua kwamba maisha yako yote hutatumia hivo vitu basi Usijaribu.Watu wametumia vyote na hakuna walichopata.Kama ni kuhusu Starehe ziko nyingi sana.Hata kula Mlo mzuri sehemu nzuri,Kulala sehemu nzuri,kutembelea sehemu nzuri zilizotulia,kujifunza vitu vipaya kama Computer Programming,Kusoma Vitabu,Kuandika vitabu na machapisho JF vyote unaweza kuvifanya Starehe na Niamni nikikwambia kwamba Ni starehe nzuri zaidi kuliko Hizo nilizotaja hapo JUU

Hizo hapo juu ni starehe za watu ambao wako Frustrated na Maisha na kwa Umri wako bado hujawa Frustrated ili Utakapofikia hatua ya kuwa Frustrated Hutakuja huku kutuuliza bali utachagua moja na ndio itakuwa anguko lako
 
Back
Top Bottom