Naombeni wazo la Biashara kwa mtaji wa kati ya Milioni 2-3 kwa Dar es Salaam

Naombeni wazo la Biashara kwa mtaji wa kati ya Milioni 2-3 kwa Dar es Salaam

Ugali Nyama Choma Mchana

Nunua jiko lako la kuchomea nyama Choma na Jiko lako la gesi Choka mapande yako mchana saa 4 tu ugali ushaivisha anza kutafuta ODA, Tega maeneo kuna boda boda Tia Kambi eneo hilo. Hamna boda atakula walinkwa mama ntilie... Uza 2500 ugali pande... Utanishukuru.

Kuku Choma/Kukaanga na Ndizi Mzuzu

Tega zako mahali hii ni biashara ya muda na wakati wote mapema tuu usifanye kama wengine Jiongeze Songa na ugali mchana Mtu anapga ugali kuku 2500.

Paja 1500 kidari 2000 ugali 500 Ushindwe mwenyewe... Usisahau kuwa na deli lako lenye katon hata za maji ya Hill hapo na mabarafu.

Uji/Chai/Tangawizi/Maziwa Jioni

Nunua Thermos zako kubwa zile tengeneza Uji wako Chai Tangawizi kisha tembelea sehemu zenye Boda Boda Jioni zungusha Kaa sehemu utaona Kijiwe kimoja kitamaliza thermos zote usipoangalia.

Acha Tamaaa,Uza 500 kikombe Ni biashara ya masaa yasiopungua Manne ila utatengeneza sio chini ya 40k faida kwa siku kwa mwezi Sidisha mwenyewe... Acha Tamaaa (ukumbuke kutoa zaka)

Nimekupa Top 3 zangu kama kweli unatafuta Pesa kindaki ndaki.
 
Back
Top Bottom