Naombeni wazo la Biashara kwa mtaji wa kati ya Milioni 2-3 kwa Dar es Salaam

Naombeni wazo la Biashara kwa mtaji wa kati ya Milioni 2-3 kwa Dar es Salaam

Natafuta cargo shorts sipati napata zile za cadet zitapauka. Ila cargo pants zipo za kutosha. Ila nguo za kiume hazitoki sana na zina bei
Basi target yako iwe kwa wanawake mchanganyiko yaani Belo tofauti tofauti
Zina faida sana mitumba
 
Hiyo ya M pesa mchawi location tu na kwa wadada naona inawafaa sana haina mishkeli mingi.
Japo wadau wameipiga vita sana ila kwa mimi ningeichagua hiyo.

Chipsi zina mambo mengi na ni lazima utafute mtu wa kukusaidia, uendeshaji wake ni gharama lakini pia inahitaji sana umchunge mfanyakazi wako, tofauti na mpesa ambayo unaifanya mwenyewe.
Sawa mkuu
 
Nimepitia Ushauri mwingi wamekushauri Biashara ya chipsi nimeshtuka sana.

Yaani ni kama taifa linaangamia hasa vijana wa kiume kwa kula chips.

Sasa itafikia maala vilio kwenye ndoa kwamba wazee wanashindwa Kazi kwa kuendekeza chips. Chips siyo nzuri kwa wanaume ni hatari sana.
 
Sio kama inakufa ila ishakuwa kama duka la mangi kila mwenye milioni mbili tatu anakimbilia humo. Wenye mitandao wanachofanya ni kupunguza commission tu.

Imagine kuzungusha million 3 halafu upate laki na nusu kwa mwezi hujalipa pango wala mshahara wa mhudumu.
Dogo kama yuko Dar na hio hela, ningemshauri afanye kazi ambazo hazitaki capital investment, issue za cargo transportation, akiji position vizuri Jangwani au Kariakoo, atapiga sana hela na almost hakuna cha maana atakachowekeza.

Zipo kazi nyingi zinazotaka mtu aweze tu kuamka mapema na kuchelewa kulala ila pesa anapiga za maana sana.
 
Mkuu namaanisha nikitafuta kununua. Hapo nilikuwa nachangia hoja yako ya kuuza nguo. Niko na ujasiriamali mwingine ila nina friends wengi kwenye nguo naona hawakuanza na mtaji mkubwa.
Hapo sawa, nimekuelewa Boss
 
Dogo kama yuko Dar na hio hela, ningemshauri afanye kazi ambazo hazitaki capital investment, issue za cargo transportation, akiji position vizuri Jangwani au kariakoo, atapiga sana hela na almost hakuna cha maana atakachowekeza. Zipo kazi nyingi zinazotaka mtu aweze tu kuamka mapema na kuchelewa kulala ila pesa anapiga za maana sana.
Unaweza kufafanua kuhusu usafirishaji mizigo?
 
Unaweza kufafanua kuhusu usafirishaji mizigo?
Deal za mjini ni kwa ajili ya watoto wa mjini. Hicho nilichokiandika hapo kibebe ukifanyie kazi. Kama ni mtoto wa mjini hautakwama ila maelezo utafanya nikeshe hapa mkuu. Nimekupa na location ambayo hizo pigo zinafanyika sana na kwa wingi, panaitwa Jangwani parking ya fuso pale.
 
Back
Top Bottom