Naona kama upo Afrika na ukawa Introvert ni changamoto sana

Huyo sio introvert; ana tatizo jingine kama sio timidity tu. Jaribuni kushauriana naye au ikibidi pateni ushauri wa psychologists.

Introvert hashindwi kujitegemea au kuwasiliana na watu inapobidi. Anaweza hata kuhudhuria tafrija, akatoa neno fupi (akibanwa), lakini akateleza kimya kimya (sneak out) mara baada ya ratiba muhimu kukamilika.
 
Haaaaa. Ila naona kama Wa Tz Wengi, wanaona kua introvert in Jambo la maana sana
Hapana, ukiingia katika maisha ya kawaida, introvert wanateseka sana sanaa maana maisha yetu wabongo ni ya kijamaa ambapo unatakiwa kujumuika na kuchangamana na watu ili uonekane ni mtu katika watu. Kinyume na hapo utaitwa unaringa, unajisikia, una roho mbaya, una matatizo ya akili ama kihisia etc..

Ndio maana introverts wakikutana mfano JF huwa wanafurahi kwa kupata sense of acceptance & belongingness ambayo kwenye maisha ya kawaida hawaipati
 
Hizi mambo huwa bado sijazielewaga kabisa
 
Hizi mambo huwa bado sijazielewaga kabisa
Anachojaribu kuelezea kipo hivi

Ukiwa Tanzania unabidi kufanya socialization ili kuendana na jamii .

Kwakuwa jamii ya Tanzania haina ufahamu mzuri wa haya mambo ile kuwa unapenda kukaa peke yako inaweza tafsiriwa Kama kujipenda, kiburi, ubinafsi n.k

Na ukiwa na uwezo wa kifedha inaweza pelelekea watu kutafsiri kuwa unalinga Sana .

Japo ili kuendana na kasi ya maisha hawa introvert hutumia teknolojia kuwasiliana na watu wao na kufanya Kazi
 
Introvert bora bongo ukiwa huko ulaya msongo wa mawazo utakuuwa wewe si unaina vifo vingi huko kwao ni suicide?

Bongo unaweza ukawa introvert na maisha yakaenda tofauti na huko kwa watu
 
Hapo nimekupata
 
Hawa huwa wasikilizaji wazuri sana
Huwaza kwanza kabla ya kutoa jibu, hawakurupuki
Sio wakimya bali wanapenda utulivu

Kuwa na marafiki wachache sio mbaya pia na wako hivyo

Hakuna ugumu kuishi bongo
 
Je haiwezi kuwa ni kutozoeana na watu wa eneo husika baada ya kwenda ukitokea eneo lingine.
 
Nina fikiria wengi hatuelewa maana ya kuwa introvert

Kuwa introvert hamzuii mtu kupanda
Daladala ,, maana unaweza panda daladala na wala usionger ja yeyeto yule..
Yaani sisi bana, tuna ujinga mwingi sana.. Yaani mtu hataki kuelewa mambo, anasikiliza jujuu anaenda kutoa mada tiktok.
 
Je haiwezi kuwa ni kutozoeana na watu wa eneo husika baada ya kwenda ukitokea eneo lingine.
Huyo dogo hata kwao yupo hivyo hivyo. Hapo kwangu kwenyewe ana miaka miwili japo huku siku 1 au 2 akitokea chuo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ