Naona kama upo Afrika na ukawa Introvert ni changamoto sana

Naona kama upo Afrika na ukawa Introvert ni changamoto sana

Siyo muda wote introvert anakua anataka kukaa peke yake tu kuna muda anafurahi uwepo wa watu karibu yake japo anaweza asichangie mada kwahiyo suala la usafiri au kuishi uswahilini siyo changamoto kwake, anaweza kuishi uswahili fresh tu ndo unaskia yule jamaa mpole haongei
 
Hizi mambo huwa bado sijazielewaga kabisa
Endelea kuishi tu mkuu. Nadhani hata hizi issue za personalities huwa zinaangaliwa zaidi na introverts maana wao ndo huwa wanajiona abnormal kwa kutoweza kwenda na flow ya kuhusiana na wengine. Ndio maana kwenye kutafuta kujielewa ndio hukutana na hizo issue za introverts vs extroverts.

Ila kama unapiga ulabu na hupati shida kwenye socialization kama extrovert. Mambo ya personality huwezi kuhangaika nayo maana upo "normal". Ni sawa na mtu ambaye mwenye maumbile madogo na mwenye maumbile ya wastani. Of course wa madogo ndio atahangaika kuitafuta validation and acceptance na mwisho atakutana na concepts ama ukweli ambao si interest ya mtu aliye normal
 
😅😅😅 ila nikila vitu vyangu nakua na uwezo mkubwa wa kuwasiliana na watu na hata kufanya michongo ,nikiwa mzima naona kama huo uwezo unapotea😅😅😅
Hapo shida ni confidence tu. Pombe hua inaondoa aibu.
 
Hapana, ukiingia katika maisha ya kawaida, introvert wanateseka sana sanaa maana maisha yetu wabongo ni ya kijamaa ambapo unatakiwa kujumuika na kuchangamana na watu ili uonekane ni mtu katika watu. Kinyume na hapo utaitwa unaringa, unajisikia, una roho mbaya, una matatizo ya akili ama kihisia etc..

Ndio maana introverts wakikutana mfano JF huwa wanafurahi kwa kupata sense of acceptance & belongingness ambayo kwenye maisha ya kawaida hawaipati
Mimi mkuu pia nina shida hiyo. Naweza kuchangamana vizuri kwenye makonferensi huko na ofisini lakini nafanya hivyo kwa vile tu inanilazimu. Nakuwa na furaha sana nikiwa peke yangu au nikiwa na rafiki ambaye tuna ushikaji wa karibu.

Kwa jamii inayotegemea connection na madili ya huko kwenye vilabu vya pombe na kwenye social gatherings aisee ni mtihani. I have lost several opportunities kutokana na hii ishu lakini nimetokea tu kujikubali hatimaye maana ukijilazimisha tu kuachana nayo unaweza ukaharibu zaidi.

Wiki jana nilikuwa na washikaji Dodoma mpaka wananishangaa. Ni wewe kweli unajichanganya hivi au ni mwingine? Wakati huo mi najikaza tu moyoni natamani nirudi hotelini nikapate uhuru wangu.

Introvert tunafiti vizuri Ulaya na Marekani lakini kwa jamii za Kiafrika aisee ni mtihani. Hapa kuna boya kaniongeza kwenye kamati ya mbunge mteule kesho inabidi tukutane mimi sijui ndiyo eti strategist. Yaani we acha tu! 😂😂😂
 
100%

Mimi nilikuwa Kama huyo Dogo wakati nakaa kwa uncle , kwanza Mara nyingi introvert huwa hawapandeli kuomba omba au kumpa MTU matatizo yake ayatatue.
Ni kweli mkuu,ni uhakika asilimia kubwa ya watu humu jf ni introvert,maana wengi wao wanapenda sana kusoma na kijifunza wakati, ulimwengu kwa sasa upo kwenye short videos,tik tok,reels na kadhalika sisemi wao hawatumii ila huo ni uhalisia

Prove me wrong
 
Haaaaa. Ila naona kama Wa Tz Wengi, wanaona kua introvert in Jambo la maana sana
Kuwa introvert mimi huwa naona ni changamoto ya kitabia. Wewe uwe mtu wa kujitenga halafu ujuone upo sawa
 
Mimi mkuu pia nina shida hiyo. Naweza kuchangamana vizuri kwenye makonferensi huko na ofisini lakini nafanya hivyo kwa vile tu inanilazimu. Nakuwa na furaha sana nikiwa peke yangu au nikiwa na rafiki ambaye tuna ushikaji wa karibu.

Kwa jamii inayotegemea connection na madili ya huko kwenye vilabu vya pombe na kwenye social gatherings aisee ni mtihani. I have lost several opportunities kutokana na hii ishu lakini nimetokea tu kujikubali hatimaye maana ukijilazimisha tu kuachana nayo unaweza ukaharibu zaidi.

Wiki jana nilikuwa na washikaji Dodoma mpaka wananishangaa. Ni wewe kweli unajichanganya hivi au ni mwingine? Wakati huo mi najikaza tu moyoni natamani nirudi hotelini nikapate uhuru wangu.

Introvert tunafiti vizuri Ulaya na Marekani lakini kwa jamii za Kiafrika aisee ni mtihani. Hapa kuna boya kaniongeza kwenye kamati ya mbunge kesho inabidi tukutane mimi sijui ndiyo eti strategist. Yaani we acha tu! 😂😂😂
Nkwela wane tuta ongea vipi sasa kuhusu nkema wane😂
 
Hizo ni haiba za kizungu...
Na research zao walifanyiwa wazungu...mimi na wewe hatumo.

Tabia zetu zinabadilika badilika kulingana na majira, hali ya maisha, watu wanaotuzunguka, nk

Inawezakanaje tabia za watu bilion 7 zigawanywe kwenye makundi manne tu.

Mimi zamani nilikuwa najua kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanahusu mambo ya hali ya hewa, uoto wa asili nk kumbe nilikuwa nakosea.
Mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na watu.....huu ni uchawa nalo ni badiliko la Tabia-nchi...Tabia zetu huwezi kuzi-google
Umesema ukweli.
 
Anachojaribu kuelezea kipo hivi

Ukiwa Tanzania unabidi kufanya socialization ili kuendana na jamii .

Kwakuwa jamii ya Tanzania haina ufahamu mzuri wa haya mambo ile kuwa unapenda kukaa peke yako inaweza tafsiriwa Kama kujipenda, kiburi, ubinafsi n.k

Na ukiwa na uwezo wa kifedha inaweza pelelekea watu kutafsiri kuwa unalinga Sana .

Japo ili kuendana na kasi ya maisha hawa introvert hutumia teknolojia kuwasiliana na watu wao na kufanya Kazi
Nilikuaga na hiyo tabia ya kukaa ndani mwishowe wapangaji wakaanza kunisema yaani huyu yeye ni mtu wakujifungia ndani tuu hata hatoki

Kuna siku nimechill ndani nikasikia Nyokaa huyo yaani walikua wanafanya hivyo ili nitoke nje tu
 
Back
Top Bottom