Naona kama upo Afrika na ukawa Introvert ni changamoto sana

Kuna mambo tunajipendekeza tu ila ni tabia za wazungu na research zilifanyika kwao.

Kuna haja nasisi kuanza kuresearch tabia zetu.

safarini Khartoum Sudani.
Mazingira ndiyo yana nafasi katika tabia, haiba na saikolojia ya mtu. Nature vs. Nurture.

Hata hivyo uzuri wa sayansi ni kwamba ili kitu kiweze kukubalika ni lazima kiwe na uhakikifu. Maana yake ni kwamba utafiti ukishafanyika na ukachapishwa katika reputable refereed journals maana yake mtu ye yote duniani anaweza kufanya utafiti ule ule kwa kufuata utaratibu ule ule na akapata matokeo yale yale. Ukipata matokeo tofauti maana yake ama umekosea mahali katika jaribio lako na kama hujakosea basi pengine kuna fenomena nyingine inayoweza kuelezea matokeo yako mapya (nurture) au pengine matokeo ya mtafiti wa kwanza yana matatizo na hivyo unaweza kupinga nadharia yake. Kama ni sayansi ya kweli ndivyo inavyopaswa kuwa haijalishi unafanyia utafiti wako Ulaya, Afrika, Asia au wapi!

Shida yetu Waafrika tunapenda sana kulalamika na kudogosha tafiti za wenzetu waliowekeza mabilioni ya dola katika tafiti zao na kufikia mahitimisho yao kulingana na mazingira yao. Kufanya tafiti zetu hatutaki na za hao wenzetu nazo tunazibeza. Ndiyo hayo hayo ya kukataa chanjo kwa kudai eti wazungu wanataka kutuua na wakati huo huo sisi hatutengenezi za kwetu na madawa karibu yote tunayotumia ni ya hao hao tunaowatuhumu kwamba wanataka kutuua. Ajabu sana!

Ingieni lab. Fanyeni tafiti ili kupinga haya mahitimisho ya kizungu. Maana huwezi kupinga utafiti wa mtu kwa maneno na porojo tu kama ilivyo kawaida yetu!
 
Akipanda daladala atakereka sana na kelele za kwenye daladala kuanzia radio mpaka konda na wakati mwingine hadi abiria wanapiga kelele
Introvert anaweza kaa sehemu yenye kelele kama ndiyo option pekee iliyopo lakini hatochangia chochote atabaki kuwa msikilizaji tu ..

Hivyo point yangu inarudi pale pale watz wengi wahajui maana ya introvert wengi wanaigixa kuwa hivyo
 
Na mimi nina tabia hiyo ila ninajitahidi sana ni badirike
 
Iam a real introvert.
 
Introvert anaweza kaa sehemu yenye kelele kama ndiyo option pekee iliyopo lakini hatochangia chochote atabaki kuwa msikilizaji tu ..

Hivyo point yangu inarudi pale pale watz wengi wahajui maana ya introvert wengi wanaigixa kuwa hivyo
 
Wewe kama ni introvert halafu unakosa sifa zifuatazo, wherever you are...you are a deadman walking buddy!!!
Introvert unatakiwa uwe na sifa hizi tatu:
1) Uwe kipanga/akili nyingi.
2) Uwe na kipaji, a really talented fella.
3) Uwe na familia tajiri, familia inayojiweza.

No need to sugarcoat it, Kibongo bongo kuwa introvert ni hasara!
Wabongo wengi ni masikini, Bongo inatakiwa urambe miguu ya watu na upambane kwelikweli ili utoboe. Kwahiyo kama hauna hizo sifa tatu hapo juu na ni Introvert, UMEKWISHA!!!
 
Dah!
 
Kumbe kuwa introvert hupandi daladala
Introverts wanaweza kupanda daladala, ila ni kero sana kwao.
Umeshawahi kugombea usafiri mkongwe!?
Kuna baadhi ya route Dar inatakiwa ujichetua na kujitoa akili haswa ili uweze kupata seat.

Introverts wana kaaibu fulani hivi kaajabu!
Route ya Mbagala-Kawe (IF YOU KNOW YOU KNOW) inamtengenezea vidonda vya tumbo introvert, atakufa kabla ya wakati, inatakiwa anunue gari!!!
 
Basi majamaa wanateseka sana
 
Yote matatu uliyoandika sio kweli, ni myths tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…