Naondoka Bungeni bila Mume wangu, Naondoka na Aibu na Mikopo ya kutisha

Naondoka Bungeni bila Mume wangu, Naondoka na Aibu na Mikopo ya kutisha

SASA NAKUPA ELIM7 MARA YA MWISHO .
kutatofauti ya kuwa kiongozi na kuwa na akil8 ya uongozi...sikusema mwanamke awezi kuwa kiongozi....nimesema wanamke hana akili uongozi ....sasa sijui kama wewe ujui todmfauti ya hayo maneno ...mama yangu anaweza kuwa kiongozi tatizo ni akili ya uongozi anayo? Wewe umekazania hoja ambayo inaonyesha ushahidi wa msivyo na akili ...kuhusu kuongoza hata kichaa anaweza kuwa kiongozi tofauti ni je kichaa anaweza kuwa kiongozi mwenye akili ya uongozi ....tumia akili kuelewa.....Akili ya uongozi ndiyo akili hadim7 zaidi kwa binadamu hata kwa wanaume ni wachache sana waliyo nayo ...ila kwa kiumbe mwanamke ni hakuna kabisa ndiyo maana nakuakikishia hakuna mwanamke hatakaye kuja kuwa kiongozi mzuri mwenye vision sahihi zitokazo kichwani mwake mwenyewe.
Ndiyo maana kwenye dini zenu kuna maandiko yanasema "kiongozi kipofu kuongoza vipofu " hivyo yanaonyesha vipofu wa akili wanaweza kuwa viongozi ....mimi sikusema wanamke awezi kuwa kiongozi nilicho sema ni kwamba mwanamke awezi kuwa na akili ya uongozi.
Sio Kweli kuna Easter kwenye Biblia Ana ,Dorkas walikuwa Wanawake makini hata dada yake Musa pia,hiyo ni mifano michache!Pia kuna Abigaili alimtetea mumewe kwa Daudi hata wimbo upo,unaozungumzia Hilo.
 
Akili za hao wanawake viongozi ziko kwenye kupunguza matatizo mengi sugu yanayosababishwa na BAADHI ya hao wanaume. 👇🤗
Mpendwa Mheshimiwa,

Yamepungua ila kama yameongezeka ,kushindwa kujenga misingi ya familia kuanzia chini ni tatizo.

Mama na baba wote wanatoka ,hao watoto watalelewa na nan ? Kwanza ni ukatili kumuacha mtoto wa miezi mwili au mitatu halafu unaenda kazini kwa kisingizio kwamba utarudi saa 6 kumnyonyesha .Ni bora kuandaa utaratibu hata wakae meternity leave ya miezi 8 na kuendelea .


Upande wa pili Mheshimiwa wanawake mnaharibu performance na utendaji wa kazi kwa ujumla : hapa tunaongelea availability ( siku mnazokuwa kazini ili kutoa huduma ) ,kwa wanawake ambao bado wako kwenye uzazi ni tatizo sana ,kila siku ni excuses : kwa mfano hapa kwetu wanawake wawili wamejifungua na hawapo ofisini kabla ya hapo kipind cha mimba wanapotea hata wiki kama wagonjwa.. Hii ni haki kweli au unafiki wa kuleta agenda za 50/50.

Kule ulaya wanawake wanapenda mshahara pungufu dhidi ya wanaume hata kama wana cheo sawa na elimu sawa .
 
Sasa Mheshimiwa mbona haujibu hoja kuu mna roam around the bush? Wewe ni Waziri wa sekta hii, unawasaidiaje wanawake ambao wanaathirika na haya huko bungeni ulipo wewe pia ..umalaya, uzinzi, maambukizi ya ukimwi, kupata cheo kupitia kutoa rushwa ya NGONO, kutishiwa, kuathirika kisaikolojia, ULEVI, matatizo ya ndoa zao yanayoyachamgiwa na wao kutokua na HOFU ya Mungu na kua waaminifu kwenye "korido" za bunge ,, yote haya nataka nijue wewe kama Waziri unachukua hatua Gani ili bunge liwe sehemu Salama na lenye heshima
Wewe kwani uliwahi kuwa mbunge wa bunge la ngapi?
 
Mpendwa Mheshimiwa,

Yamepungua ila kama yameongezeka ,kushindwa kujenga misingi ya familia kuanzia chini ni tatizo.

Mama na baba wote wanatoka ,hao watoto watalelewa na nan ? Kwanza ni ukatili kumuacha mtoto wa miezi mwili au mitatu halafu unaenda kazini kwa kisingizio kwamba utarudi saa 6 kumnyonyesha .Ni bora kuandaa utaratibu hata wakae meternity leave ya miezi 8 na kuendelea .


Upande wa pili Mheshimiwa wanawake mnaharibu performance na utendaji wa kazi kwa ujumla : hapa tunaongelea availability ( siku mnazokuwa kazini ili kutoa huduma ) ,kwa wanawake ambao bado wako kwenye uzazi ni tatizo sana ,kila siku ni excuses : kwa mfano hapa kwetu wanawake wawili wamejifungua na hawapo ofisini kabla ya hapo kipind cha mimba wanapotea hata wiki kama wagonjwa.. Hii ni haki kweli au unafiki wa kuleta agenda za 50/50.

Kule ulaya wanawake wanapenda mshahara pungufu dhidi ya wanaume hata kama wana cheo sawa na elimu sawa .
Hivi ile Mei mosi walipotangaza likizo ya maternity kwa mke na mume, wewe ulikuwa wapi rafiki
 
Sio Kweli kuna Easter kwenye Biblia Ana ,Dorkas walikuwa Wanawake makini hata dada yake Musa pia,hiyo ni mifano michache!Pia kuna Abigaili alimtetea mumewe kwa Daudi hata wimbo upo,unaozungumzia Hilo.
Unachanganya mada ...sikusema wanamke hana akili zote bali akili ya uongozi ..anaweza kuwa na akili zingine ...huyo dada wa musa alikuwa kiongozi wa wapi? Kwanza alimpinga hadi mungu wa musa na kuadhibiwa kuishi porini kwa muda.
 
Ninaondoka Bungeni Bila Mume Wangu, Bali na Mikopo Mikubwa na Aibu

Jana katika Sekretarieti ya NRM, nilifanya mahojiano yenye hisia kali na mbunge wa kike aliyekuwa amechukua fomu za uteuzi. Aliniruhusu kuchapisha taarifa hii bila kutaja jina lake. Yale aliyoshiriki yalikuwa ya kuhuzunisha na kufumbua macho, yakionyesha gharama halisi ya siasa kwa wanawake wengi.

Alianza kwa kusema, "Ninaondoka bungeni bila mume wangu, bali na mikopo mikubwa na aibu." Alieleza kuhusu ndoa yenye furaha aliyokuwa nayo na mume wake pamoja na watoto wao, ambayo ilivunjika baada ya yeye kujiunga na bunge mwaka 2016. Kuanzia mwaka 2017, familia yao ilikuwa kwenye vita kila wakati; nyumba yao ikawa kama uwanja wa moto. Alieleza kuwa hakuwa na muda kwa mume na watoto wake, kwani maisha yake bungeni yalikuwa yamejaa mikutano, safari, na kukutana na wanaume kutoka ngazi zote za serikali.

Alikiri kwa kusema, "Ukweli ni kwamba, maisha ya bungeni ni tofauti—unakutana na wanaume wa aina zote katika vikao vya bunge na kusafiri nao nje ya nchi." Alisimulia jinsi walivyokuwa wakikaa wiki kadhaa nje ya nchi kwa shughuli za kibunge pamoja na wabunge wa kiume, na jinsi safari hizo zilivyogeuka kuwa njia ya kuingia katika mahusiano yasiyofaa. "Hata kama wewe ni mwanamke mwenye msimamo, utaishia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mbunge mwenzako, waziri, afisa mwandamizi wa serikali au usalama. Hii ndiyo hali halisi ambayo wabunge wanawake walioolewa hawasemi, lakini wanapitia."

Alieleza hali ya hatari ya safari hizo: "Unaenda nje ya nchi kwa wiki mbili na wabunge wa kiume na maafisa wa serikali, mnakaa kwenye hoteli moja, mnakula chakula pamoja—chai ya asubuhi, chakula cha mchana na cha jioni—na wanaume wote katika ujumbe huo wanakuvizia. Baadhi yao watakupa msaada wa kifedha, kukuahidi nafasi, miradi, safari—vyote." Alifichua kuwa wanawake wengi hushindwa kuhimili vishawishi hivyo vya kimapenzi, na wanaofanikiwa kuhimili hukumbana na madhara—kihisia, kifamilia, na kiafya. "Wengi wao wana maambukizi ya VVU," aliongeza kwa huzuni.

Alilalamikia jinsi alivyopoteza mwelekeo wa familia: "Nilipoteza hamu kwa mume wangu na kuanza kuzingatia zaidi wanaume niliokutana nao bungeni na serikalini. Sikutambua kuwa wanaume hawa walikuwa watumiaji tu." Alieleza kuwa mume wake alikuwa ametumia rasilimali nyingi kumuunga mkono kisiasa. "Tuliuza mali za familia, na alikosa kazi yenye mshahara mzuri katika shirika la kimataifa kwa sababu ya kujihusisha na siasa zangu. Baadaye alianzisha biashara, lakini wakati huo uharibifu ulikuwa umeshafanyika."

Kwa sauti ya huzuni, alieleza jinsi ndoa yake ilivyovunjika: "Niliwaona wabunge wengi wa kike wakitumbukia kwenye mapenzi na wabunge wenzao, mawaziri, na maafisa wa serikali, nilijizuia mwanzoni. Lakini baadaye nilijikuta nimejiingiza pia. Mume wangu akawa kama hana maana tena, sihitaji mtu wa kawaida wakati mimi nina nguvu na uhusiano na watu serikalini." Alisema kwa masikitiko kuwa baadhi ya wanaume hao walikuwa na VVU, na hawakuwa na hofu ya kueneza maambukizi.

Sasa, baada ya vipindi viwili bungeni, amebaki na maumivu na huzuni: "Familia yangu imevunjika, nimebaki na mikopo mikubwa, na upweke kamili." Alieleza kuwa mshahara wake wa milioni 5 kwa mwezi unaenda kwa walanguzi wa pesa, na hawezi hata kuhudumia jimbo lake. "Matumizi ni makubwa sana; wanaume waliokuwa wakinisaidia hawapo tena."

Majuto yalionekana wazi: "Ninajuta siku niliyoingia kwenye siasa. Nilimpoteza mume mzuri, mwenye upendo. Sasa nina miaka 49 na niko peke yangu." Alisema mume wake wa zamani ameteseka kwa miaka kumi, na baadhi ya watu serikalini waliwekeza ili kumuangamiza kifedha au hata kumuua. Alisema alikuwa na ushawishi mkubwa kanisani lakini anajihisi kama msaliti wa familia na maadili yake.

Alitafakari kwa kina: "Kama nisingeingia kwenye siasa, mimi na mume wangu tungekuwa na furaha, mafanikio, na familia nzuri. Sasa niko peke yangu, na jimbo limekuwa mzigo mzito. Gharama ni kubwa na najihisi nimefedheheka." Alikiri kuwa huomba msamaha kila siku anaporudi jimboni bila msaada wa mume. "Mwaka 2021, aliuza ardhi yetu ili kuniwezesha kisiasa. Samahani kwa kumsaliti."

Hadithi yake ni onyo kwa wanawake wanaotamani kuingia kwenye siasa: "Ukiingia kwenye siasa, unakuwa mbinafsi sana na mwenye tamaa kubwa, unafikiria vyeo tu. Ukianza kuwa na ndoto kubwa, utaishia kulala na wanaume watakaokusaidia kufikia ndoto hizo. Wanawake wengi wameishia hivi. Mbunge wa kike anapokutana na wanasiasa wakuu na wabunge wenzake, heshima kwa mume wake hupotea kabisa."

Alihitimisha kwa tafakari ya kusikitisha: "Mwishowe, nimebaki na majuto na huzuni tu. Najutia maamuzi niliyofanya na maumivu niliyoyasababisha kwa familia yangu. Nalia kwa kupoteza ndoa na mapenzi ya maisha yangu. Natumaini hadithi yangu itakuwa somo kwa wengine—epukeni makosa niliyofanya. Watoto wangu hawatakuwa wanasiasa. Kila mwanasiasa ni mwongo na asiye na uaminifu. Wanachojua ni kutumia na kutupa. Wote hujifanya kuwa na nguvu na uhusiano."

Hadithi yake inaonyesha gharama halisi ya tamaa ya kufanikiwa kwa haraka au bila msimamo.

CnP
Kuna ndugu yetu alimsomesha mwanamke mwisho wa siku yule dada akawa mwalimu wa secondary,jamaa akalazimisha hadi akafunga nae ndoa akawa mkewe,mwaka huu alipoteuliwa kuwa mkuu wa shule huwezi amini mwezi wa tano akamtimua mumewe nyumbani na anadai talaka yake.
 
Tupo pamoja daima. Taaluma ya udaktari wa binadamu changanya na exposure ya huku ustawi wa jamii inaniongoza kuwa, watu wengi duniani hivi sasa wanahitaji huduma ya elimu zaidi badala ya ligi ya mashindano ya maneno. Mpe elimu stahiki na akiendelea na ligi, basi mtakie tu kila la heri, uwe mjinga tu maisha yaendelee halafu muda utakuja kuamua😅


Mh. Dorothy Gwajima, napata furaha sana kuona unajibu hoja za watu kama mwananchi wa kawaida kabisa, this humbleness is so great in human life, hujikwezi hata kidogo ingawa ni Waziri, hongera sana kwa hilo, and nikwambie navyokuona, you are so beautiful kimwonekano and spiritually, you have it all..!! 😘 You have brain and Beauty..!! 😘 You are amazing..!! 👏
 
Ni udhaifu wa mtu binafsi. Umashaingia kwenye ulaji wa kulipwa mamilioni kwa mwezi, unataka nini tena? Kama ni safari za njema, huwezi kwenda na mumeo?
Moja ya ndoto kubwa ya wanawake ni UHURU wa kuzidi.Mume huoni atambana?
 
Back
Top Bottom