Nape: CHADEMA wamepewa fedha na wazungu kuvuruga mchakato wa katiba

Sasa nyie ndo wenye dola iweje mje mlalamike kwenye mkutano wa hadhara badala ya kuwachukulia hatua ilihali mna taarifa muhim kama hizo.

Mi naona hizo ni stori za kutunga tu,Mmeumbuka maana mchakato huo mnataka kuhodhi kwani wakwenu peke yenu? Kila kitu tulikiona bungeni, Tusubiri 2015,Tatizo lenu CCM mnatuona sisi mazezeta hatujui kitu kinachoendelea
 
Kwa hiyo CHADEMA walipewa hela ili waingize ajenda ya katiba mpya kwenye ilani yao ya uchaguzi, Kisha wakapewa hela ili Waisukume ajenda hiyo japo wao hawakushinda uchaguzi, Basi wakafanikiwa kuisukuma kwa ufanisi mkubwa, na sasa wamepewa hela ili waivuruge, na sasa washaanza kuivuruga?

Pengine mwenye majibu ya maswali haya anisaidie na mimi nipate kufahamu; CHADEMA walianza kupewa hela toka walipokuwa wakiandaa ilani ambapo katiba mpya ilikuwa ndani yake au wamepewa juzi tu walivyotoka bungeni? Ikiwa walipewa toka mwanzo; aliekuwa kawapa awali ndo huyo huyo kawapa juzi au ni mtu wengine!

Kama majibu hayapo; Rejea dalili za CHAMA kinachoelekea kufa kwa maelezo zaidi kuhusu anachoongea Nape..
 
hizo hela nadhani walipewa na OBAMA alivyokuja pale ikulu!.
 
Yaani kuna watu mpaka leo wanachukulia kauli za Nape seriously? Really?
 
Mkuu, kwa kuwa Nape ni kiongozi wa chama tawala, kauli yake si ya kubeza hata kidogo. huwezi jua ana ushahidi kiasi gani katika hilo. sote tutafakari kwa pamoja

Sasa wao si wangekwenda mahakamani sasa wanalalama nini?
 
Huyu jamaa ni punguani sana, huyu haaminiki, alikuwa wapi kutueleza kabla ya tukio kutokea? hawa wanatafuta pakujifichia,

siasa za Tanzania ni za kijinga sana na ni za watu wajinga waliobaka siasa, sio kila mtu anafaa kuwa mwanasiasa bhana, Kila

likitokea tukio lazima suala fulani litafutwe ili kuwapoteza watanzania, na baadhi ya watanzania wamekuwa ni bendera tu

wanapelekeshwa na wanasiasa uchwara, Lazima siasa zetu zibadilike, Nape, Mwigulu na wengine kama hawa lazima waelewe

kuwa hii nchi si yao peke yao.

CCM ndo ina serikali, polisi, jeshi, usalama, magereza, Takukuru nk. nijuavyo siasa za Tanzania kama ingekuwa kweli ungeona

hivi vyombo, Mbona Kinana alienda China akakaa muda mrefu? mbona Mwigulu alienda China akaja na Bomu la Arusha? kwani

hivyo vyombo havikujua? Shame on him!!! wala chadema msijibu chochote huyu ni sisimizi, lengo lao wanataka kuwagawa

wapinzani ambao tayari wameungana kwa swala hili.
 
Tunaomba awe waz basi..hizo pesa wanatoa wap.!?

Nape mwenyewe anasema amesikia CDM wamepewa fedha na wafadhili wao ili kuvuruga mchakato wa katiba mpya. Kwa maana nyingine Nape hana uhakika na analosema, ni mambo ya kusikia mitaani (umbeya). Kama anaamini anachokisema ni ukweli basi aseme hao wafadhili ni akina nani na wa nchi gani, walitoa kiasi gani, nani alipokea hizo fedha ndani ya CDM, ikaingia akaunti ya nani, akaunti namba gani na benki ipi? Nape akishathibitisha hayo, vielelezo viende kwenye vyombo vya dola kwa hatua zaidi. Tofauti na hayo Nape atakuwa kiongozi mp.u.m.ba.v.u kwa sababu anapotosha umma kwa siasa za kipuuzi.
 
Duh kumbe fedha toka ughaibuni ndizo zinarusha chopper angani?

Pamoja na anti-money laundering measures zote hizo pesa zinaingiaje hapa nchini? Serikali si izi freeze kama kweli zinakuja kwa nia ya kuharibu mchakato wa katiba.
...hapo mkuu umenena. labda anataka kutuambia Dr alikuja nazo kwenye magunia kama yale madawa ya kulevya ya "Masogange" akapita nayo airport na anazitunza nyumbani kwake?
Kama hayo yanafanyika na serikali inashindwa kudhibiti basi wawaachie serikali wanaoweza kudhibiti fedha haramu.
 
Huyu Nape na yeye alishafilisika kisiasa! Kabla ya kutoa tuhuma hizi anapaswa kututhibitishia tuhuma za nyuma alizowahi kuzitoa dhidi ya Cdm! Na Kama hawezi sisi tunamuona Kama Vuvuzela!
 
Katiba ilikuwa ni agenda ya wapinzani.

Serikali na dola ni vya CCM, so ingeweza kuzuia fedha haramu kuingia nchini.

Vyombo vya Dola havijui km kuna adui mkubwa nje mwenye nia ya kuleta machafuko nchini? Nape wasaidie kuwajua.

Msajili wa Vyama vya siasa anaielea CHADEMA na kumletea usumbufu aliyemteua? Si akifutilie mbali kutokana na tuhuma zoooote za Nape, Wassira, Lukuvi na Mwigulu?

Nchi wakoloni wetu...Membe anasubiri nini kuwasulubu mabalozi wa nchi hizo hapa nchini kwa kutuletea balaa kubwa?

My take:
Imefika wakati CHADEMA kupitia Lissu waandae na kuwasilisha muswada wa kusema uongo (Ant-Lie Bill) Bunge lijalo ili kukomesha akina Nape na wale wanaokana mashtaka halafu ushahidi ukathibitisha.
 


kwa bahati mbaya nape ni kijana mwenzetu lakini anatuaibisha, anazungumza kama vuvuzela ambalo hata kichaa anaweza kulipuliza. nape atuambie je yale maoni waliyotoa upinzani hayana mantiki, arudie kusoma kwa makini kisha ajibu kila hoja liyotolewa, asilete siasa nyepesi
 

Muacheni Jamani Nape aendelee kukiua chama chake kwa kuaniaki madhaifu ya Serikali inayoongozwa na chama chake! Kwasababu hii itakua kashfa kwa serikali watu kuingiza mafwedha na kufadhili vyama vya siasa bila ya Serikali ambayo ndo mmiliki wa taasisi zote za kibenki Na kifedha kufahamu! Hii inaonesha ata Kule Hazina kuu hakuna usawa!
 
serekali ya ccm ...ipo wapi kuchukua hatua...! wanaidhalilisha ccm kweli...
 
mkuu, Nape ni kiongozi wa chama tawala ambacho kina mikono mirefu. hivyo kauli ya Nape si ya kupuuzwa wala kuingiziwa mizaha. watanzania tutafakari kwa pamoja na hawa wanasiasa uchwara ambao wanazoea kutumiwa kuvuruga nchi yetu tuwakatae kabisa
...hiyo mikono mirefu si ingezikamata hizo pesa haramu? au serikali ni dhaifu?
 
Nape ni vuvuzela wa ccm. Hana jpya hapa. Maneno ya Nape yangetolewa na karani tu wa John Mnyika, saa hii angekuwa central kuutoa ushahidi, lakini kwa kuwa yametolewa na Vuvuzela wa ccm, hakuna anayemwona kwani hiyo ndio sera yao.
Kwa nini Usalama wa Taifa wanajifedhehesha hivi? Yaani mabilioni yaingizwe nchini, sijui kwa mabox au kwenye account gani lakini mshindwe kuuliza walizipata wapi? Mpaka Nape amewaamsha lakini bado hamjachukua hatua?? Kweli dunia mhhhh.
Afadhali Nape hakusema Dr. Slaa alikwenda kuuza kitu huko amesema alienda kuomba msaada, Mwenye kiti wa ccm anazunguka kwenda kuomba Neti za kuzuia nzi wale wakubwa akaambiwa ati ni za kuzuia mbu. Jamani, namwonea huruma.
Pita mitaani, watu wamezifanya za kuzuia kuku wasiliwe na mwewe. Dah!
Pole sana Nape.
CCm mnawalinda wauza Sembe, waziri anasema, Hakuna mbunge wa ccm atakayepona wakitajwa! Maajabu gani haya??
nji hii.
 

mbona maneno yako hayana mtiririko unaoeleweka. unarukaruka tu! mara hili mara lile. subiri viroba vimalizike kichwani ndiyo uchangie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…