Nape: Kampuni za simu haziibi vifurushi vya intaneti vya wateja

Na kwa hakika wizi unafanyika namna hiyo kwa kuuzia watu bando fake unaambiea GB 5 kumbe ni GB 3 na hapo ugumu unakuja kwenye kujua kama hili bando ni kweli ni GB 5 au lah.....
Huwezi jua sababu wameseti meseji unayopata wewe ikuoneshe umepokea 5GB ila kimsingi umeibiwa.

Kifurushi changu cha sasa nilijiunga Voda cha buku 5 ni GB 3 za week nzima naona wamenipa GB halisi maana Zantel nao wamekuwa wezi sikuhizi Unajiunga elfu 2 kila siku 1.3GB za week ila hazitoboi
 
Nape ameshatulizwa na makampuni ya mitandao ya simu
Kashalambishwa 100G ya bakshishi atafanya nini tena?

Hapo ni mwendo wa kukinga posho kila mwezi wanammegea 100M yake kila kampuni la simu hutakaa usikie tena yale mambo ya fine walizokuwa wanapigwa na Magufuli.
 
Namuunga mkono asilimia mia moja waziri. Kuna uelewa mdogo wa watumiaji wa smart phones, hicho anachokisema ni sahihi kwa sababu binafsi kuna wakati nilihisi bundle langu linaisha bila kuelewa lina isha vipi.

Nilichofanya nili install app ya ku track all my internet usage, hii app inakuonesha kabisa una bundle lenye mb ngapi na jinsi linavyoenda likiisha. Pia hii app ilikua ina list apps zote kwenye simu ikianza ile inayotumia bundle zaidi, mfano ticktock, instagram, twiter, telegram etc.

Kwa hili nikaja kujua nini kinamaliza bundle langu. Hii app nilikuta inatumia hadi mb 12 saa nyingine wakati hata sijaifungua. Nilifanya maamuzi ya kuitoa kwenye simu yangu, tokea hapo bundle linatumika vizur.

Kwa hiyo ni kweli, hakuna anayesema anaibiwa bundle ataweza kuleta ushaidi wa hilo, sana sana tu mtu ana back ground apps zinazo run na kumaliza bundle lake na hazijui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu kashapewa rushwa tayari, application zinafanya kazi hata kama umezima bando?
 
Kwa hiyo hata kama umezima data application zinafanya kazi?
 
Shida ya watawala hapo ajili ya maslahi ya umma ni ajili ya maslahi ya familia zao, huyu kavuta rushwa zake
 
Watanzania wengi hawajui matumizi sahihi ya bando. Kuna watu wanaruhusu apps kuji-update na ku-run at the background hivyo kupelekea bando kutumika.
Mkuu huko kutokujuwa kwa watz kumeanza juzi? Simu janja zimekuja juzi nchi hii ni kwanini hayo malalamiko hayakuwepo before? Kiungwana unapaswa kuwataka radhi watz.
 
Voda wapo vema. Hakuna kama voda. Nipo Eyateli nimetumia GB 15 kwa SIKU 4 ni ajabu ila kwa VODA GB 3 WIKI NZIMA NA DATA SIZIMI
 
Voda wapo vema. Hakuna kama voda. Nipo Eyateli nimetumia GB 15 kwa SIKU 4 ni ajabu ila kwa VODA GB 3 WIKI NZIMA NA DATA SIZIMI
Yeah niliweka line yao kwa ajili ya Mpesa tu ila sasa ntakuwa najiungia bando humu.
 
1 gb ya zamani ndiyo 500 mb ya sasa, kwa matumizi yaleyale.
 
1 gb ya zamani ndiyo 500 mb ya sasa, kwa matumizi yaleyale.
Exactly, ndio wanachofanya yani! Sababu mb500 zinadumu hasa zikiwa ni halisi zikiwa mara 2 yake ndio kabisa kunakuwa hamna kipengele
 
Na kwa hakika wizi unafanyika namna hiyo kwa kuuzia watu bando fake unaambiea GB 5 kumbe ni GB 3 na hapo ugumu unakuja kwenye kujua kama hili bando ni kweli ni GB 5 au lah.....
Ukitaka kulijua baada ya kupokea hiyo txt ya kuwa umepata GB5, ingia instagram , youtube au kama sio mpenzi wa hizo sites ingia twitter au jf kisha baada ya nusu saa omba kujua salio lako.

Ukiomba salio baada ya kulitumia bando watakuletea kiasi sahihi (tofauti na kile cha geresha) hapo sasa ndo utashangaa unambiwa una 3gb.
 

Huu ndio mchezo na ninacho jiuliza Nape ametumia mbinu gani kufanya hitimisho hili?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ jamaa wahuni mno mzee ila wamejificha kwenye kichaka cha background apps.

Na sahizi android na iphone OS zao wamekupa user u admin uruhus app zipi zitumie data sio kama zamani kuwa zinajidokolea data kimya kimya.

Kwahio amna app inakula data background pasipo wewe kuiruhusu.
 
Huku huja sms umetumia 75% ya GB zako baada ya sekunde kadhaa hata hiyo 25% haipo tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…