Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, watu wengi humu JF hawaelewi hata nini kinaendelea kuhusu hii movie.
Ngoja leo hapa JF nifungue code chache.
Sote tunapaswa kujua kuwa kuna vita kubwa sana ya kimaslahi ndani ya CCM kwa sasa baada ya Magufuli kufariki dunia. Vibaraka wote wa JPM wamepangwa kunyofolewa kwenye madaraka ya serikali na chama ili vibaraka wa Hangaya (JK) washike hatamu. Anachokifanya Hangaya ni kutimiza mapatano ya uhuni wa 2015 uliofanywa na JK kupitia genge lake (akiwemo Nape, January, Kinana, Makamba nk) uliohakikisha ufalme haiendi kwa mmasai wala hauendi upinzani kwa kutumia koti la kisukuma (JPM). Alichokifanya JPM baada ya kuingia madarakani kilikuwa kiko kinyume na mapatano ya kupewa urais wa dezo na genge la Msoga, ule ulikuwa ni uasi dhidi ya JK. Huo ndio ukweli wa kwanza.
Ukweli wa pili ni kuwa, Pole Pole ndio mjumbe rasmi wa kuongea mbele ya umma kuwakilisha Sukuma gang. Pole Pole anatumika kutishia, kutikisa kiberiti na kutuma ujumbe dhidi ya utawala wa Msoga gang. Wale wote waliokuwa ndani ya utawala wa JPM na kwa sasa wako kimya, basi mdomo wao wa kusemea ni Pole Pole. Ukiona ngedere mjini basi ujue kuna mtu anamfuga!
Ukweli wa tatu ni kuwa Pole Pole yuko mbioni kufukuzwa, kusimamishwa au kufungwa mdomo kisiasa (kupewa cheo cha kufungwa mdomo kama ubalozi, RAS nk) na utawala wa sasa, na tayari hilo ameshalijua, press yake ya leo ilikuwa ni "Political strategy" ya kuwatisha watawala waogope kuchukua hatua walizozipanga au wakizichukua iwe more advantage kwake kisiasa, hiyo inaitwa Pre emptying approach. Tetesi za kusema leo Pole Pole alikuwa ajivue uanachama wa CCM mbele ya vyombo vya habari zilianzishwa na team ya Pole Pole, kimakusudi na kimkakati ili kutisha na kupima upepo wa watawala wa sasa. Ni mbinu ya kisiasa.
Ukweli wa nne ni kuwa Nape ndio mwanasiasa aliyepangwa rasmi na Msoga gang kujibizana na Pole Pole kwa sasa. Anachokifanya sasa Nape sio bahati mbaya, ni jambo limepangwa na analitekeleza. Muda sio mrefu Nape naye atakuwa na vipindi vya tv na platform za kuongea mitandaoni. Yaani ngedere atajibiwa na ngedere, maana wote wako mjini wanafugwa!
Mwisho kabisa ni kuwa Nape anarudishwa tena serikalini, muda sio mrefu, na huenda akarudishwa wizara ile ile aliyotolewa au kwenda wizara fulani mpya iliyoanzishwa na Magufuli ikihusika na wizara ile ile aliyokuwepo Nape.