Nape Nnauye: Tuachane na hii habari ya "Sisi Wanyonge", kauli hiyo inatulemaza

Unyonge ni maamuzi yako binafsi, nyoko uchague kuwa masikini/ Mnyonge then unataka huruma ya serikali?
Tafuta pesa uone kama utakubali kuitwa mnyonge. Kuzaliwa masikini /Mnyonge siyo kosa lako kwani huchagui familia ya kuzaliwa. Ila kujiendekeza kuwa wewe ni mnyonge /masikini hilo ni kosa/upumbavu lako/wako.
 
Nape yupo sahihi. Mtu akikuita mnyonge, anakuwa amekufukarisha. Wazungu wanasema..you have been disempowered!
Hii kauli ya wanyonge ilikuwa ni kuwadanganya watu na kuwatumia kisiasa.
Hata kama sina kitu...usiniite mnyonge kamwe!
Uko sahihi asilimia 100, kweli hata sina mia mbovu kamwe usiniite mnyonge.
 
Mbona kama Context haina mtiririko ? Au sijaelewa ?

Hapo Unyonge unatokea wapi katika hili suala na TCRA ?

Ingawa kama anamaanisha iwapo TCRA wanatunyonga indirectly kwa kuwanyonga mitandao na kuweka sheria kandamizi kwenye mambo ya teknohama basi kweli wale ni wanyongaji jambo ambalo by default linafanya wanaonyongwa kuwa wanyonge
 
Ulinganifu wa kila kitu kwa kitu kingine ni umaskini wa akili.

Kwahiyo ukiulizwa kwanini wewe ni mpumbavu utajibu kwa kuuliza mbona hata wazazi wako walikuwa ni wapumbavu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dah umenichekesha sana mkuu tena mbele za watu
 
Nape yupo sahihi. Mtu akikuita mnyonge, anakuwa amekufukarisha. Wazungu wanasema..you have been disempowered!
Hii kauli ya wanyonge ilikuwa ni kuwadanganya watu na kuwatumia kisiasa.
Hata kama sina kitu...usiniite mnyonge kamwe!
Well said kaka kuita watu wanyonge ni uzalilishaji
 
Kama siwezi kupata haki zangu kutokana na ambao wako kwenye system kuwa na nguvu neno unyonge litaendelea kuwepo
 
Jiwe alikuwa poa sana kwenye utendaji, si ndiye alijenga uwanja wa ndege Chato au si yeye mkuu?
 
Ukweli mchungu, Africa yote ni wanyonge mbele ya mzungu!

Hatuwezi kujiamini kwa wazungu, na huo ndio unyonge, ila Magufuli tuu ndiye angalau alithubutu Kuwaita mabeberu mchana kweupe
Ukraine Ni mnyonge kwa urusi

Afrika ni wanyonge kwa wazungu

Wanachadema ni wanyonge kwa CCM

WanaCCM Ni wanyonge kwa mwenyekiti wao

Wasio na madaraka serikalini Ni wanyonge kwa wenye vyeo!
 
Hapa nakuunga mkono kwa asilimia 100,sipendi watu wanafiki, umepewa nafasi basi msaidie Rais kufanya kazi na siyo kuimba mapambio ya kusifu.
 
Unyonge ni laana
Ila isiishie kwa wananchi tu, hata wao serikali Wana unyinge sana ndio maana kila siku wanakimbilia kuomba pesa. Huu unyonge nao ukomeshwe, japo najua hamuwez
 
Hapa nakuunga mkono kwa asilimia 100,sipendi watu wanafiki, umepewa nafasi basi msaidie Rais kufanya kazi na siyo kuimba mapambio ya kusifu.
Bila kufanya hivyo hiyo nafasi unaondolewa
 
Wanakata salio kabla haijatumika?? huo ni wizi, hili lisisubiri serikali watu wanaweza kushtaki hayo makampuni na hata kutumia pressure ya wabunge wao wanaweza kubadilisha huu wizi
Kushindwa kutetea bando lililokatwa bila kutumika ni moja ya unyonge
 
Wanasiasa sio wa kuwaamini..

Mama nae ajichunguze sana
Kama wanasiasa wanapambana kufuta neno "mnyonge" ili waishi bila kujali wanyonge, Basi sisi wanyonge tumekwishaa!

Natangaza, wanyonge tuupooooo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…