Nape Nnauye: Tukosoane kwa hoja na lugha za staha. Kutukanwa kwa mama mmoja ni kutukanwa kwa kina mama wote Tanzania

CCM wanataka kuhamisha goli, walikuja na hoja ya ubaguzi imebuma, wakaja na hoja ya udini imegoma kupokelewa, sasa wanakuja na hoja ya muuza nchi eti anatukanwa. Huyu mama na Mbarawa wamefanya jambo la kijinga sana na mtu kuitwa mjinga sio tusi. Tibaijuka ni mwanamke mbona anampinga hadharani Samia, DCI Kingai na Nape ni watu wanaonyesha haja kubwa ya kuwepo na katiba mpya kudhibiti wajinga kupewa ofisi za umma.
 
Naunga mkono hoja na sitaki Mtu yeyote atukanwe maana matusi hutweza.
Lakini kusema "Hizi ni akili au matope" ni kauli ya kuonyesha uwezo wa chini wa kufikiri na si tusi.
Pia si kweli kwamba nikimaambia Anna Tibaijuka kwamba ana uelewa mdogo basi ndo nimewaambia wanawake wote. Hii dhana ya kulazimisha Samia aonekame Mwakilishi wa wanawake wote duniani imepitishwa na Bunge la CW au la SADC?
 
Kuwakamata watu siyo solution solution ni kukaa chini kama taifa na kushindanana kwa hoja
 
Mama mmoja akiuza bandari zetu maana yake akina mama wote wamauza bandari zetu za Tanganyika?
Mama mmoja akileta TOZO basi mama wote wametuletea TOZO,
Mama mmoja akipandisha gharama za bundle la internet basi .......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…