Nape: Sasa hivi vyuma vimelegea, Rais Samia kamwaga pesa mtaani tofauti na awamu iliyopita

Nape: Sasa hivi vyuma vimelegea, Rais Samia kamwaga pesa mtaani tofauti na awamu iliyopita

Je Kauli Ya Nape Ni Ya Kweli Kwamba Vyuma Vilikaza Na Sasa Vimeachia?

Kweli vimelegea nyama imeshuka bei kutoka 6000 kwa kg Hadi 8000 kwa kg

Mafuta ya aina yote bei imeshuka Sana kuliko miaka yote hongera sana kwake
Kichwa kubwa akili ndogo. Huyo ndio napy nauya
 
Je Kauli Ya Nape Ni Ya Kweli Kwamba Vyuma Vilikaza Na Sasa Vimeachia?

Kweli vimelegea nyama imeshuka bei kutoka 6000 kwa kg Hadi 8000 kwa kg

Mafuta ya aina yote bei imeshuka Sana kuliko miaka yote hongera sana kwake
Boya sana huyo,
 
Labda vimelegea huko Bungeni Kitaa "Things are Still Falling Apart"
 
Huyu dogo anawashwawashwa,
Anatafuta uteuzi

Na kwel anawashwa tena si kidogo wanasiasa kwa unafk yan mpk inauma sisi ndio tunaumia huku mtaani wao kila kitu bure pesa ipo bill zote wanalipwa alaf anatokea mshamba km huyu anaropoka
 
Huyo Nape ni mjinga fulani, anasema hivyo ili mama wa kambo ampe maisha
 
Naomba aje huku kwetu Kijiji cha Mtakuja atuoneshe hizo hela zilizomwagika mtaani.

Watu tunaumia kuuziwa nondo 12mm shilingi 26,000 pc 1 wakati Serikali ambayo ndiyo regulator wa bei ipo na haichukui hatua kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi[emoji24]
Sementi 20,000 bati za ragi 45000 sasa hivi kjjenga ni gharama kubwa
 
UNAFIKI UNAANGAMIZA TAIFA.

Kwanza naanza kwa kuandika kuwa nape anajikomba apate uteuzi hana lolote.

Pesa iliyomwagika mtaani mbona wengine hatuioni.

Hii habari hapa chini ni ya kijana aliemaliza degree yake University of Dar es salaam hana hata buku ya kula wala kunywa ,nanukuu

Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.

Changamoto ilianza majuzi huyu shemeji Ana roho mbaya kweli kumbe kipindi chote kaka angu huwa anampa 2000 ili anipe pesa ya msosi afu yeye anakata ananipa buku, nilikuja kugundua juzi broo aliposema kwa sauti nanukuu.,(hiyo buku mbili utampa dogo ya msosi) nikasema afadhari nitanunua namm Leo chips
emoji489.png
na Pepsi nijimwayemwaye, Sasa chaajabu shemeji akaja kunipa buku tu hapo tukaanza kugombana sasa akaanza kunifyezuri na kunifedheshesha mbele ya majirani wa kizaramo wavaa vijora, akisema tena kwa sauti ati amenichoka najaza kitambi tu kazi Sina nabweteka Kati pesa nizakaka angu.

Jana ilibidi yote nimwambie broo huku nikiwa na hasira sana kuliko mwanaume aliyemfumania mkewe . Broo akaniambia yote yaishe atanipa mtaji wa kazi.

SASA chaajabu Leo asubuhi naona ameniletea maji ya uhai kama Dazani tano hivi na MO energy kama dazani saba eti anasema nisimame kwenye mataa ya Sudani Temeke nianze kuuza huku nimebeba mimaji kichwani amesahau kuwa mimi nina degee kutoka UDSM chaajabu hajaniachia hata sent mpaka mdaa huu sielewi nakula nini wenyewe wameenda kazini, naombeni ushauri nifanyeje.


Nape nakuita mara tatu kabla ya kujikombakomba kasaidie wananchi wa jimbo lako juzi nimepita Mtama nimewahurumia watu wa pale kwa dhiki kuu inayowaandama. 😎 😕 😕 😉
 
Je Kauli Ya Nape Ni Ya Kweli Kwamba Vyuma Vilikaza Na Sasa Vimeachia?

Kweli vimelegea nyama imeshuka bei kutoka 6000 kwa kg Hadi 8000 kwa kg

Mafuta ya aina yote bei imeshuka Sana kuliko miaka yote hongera sana kwake
Hana Akili huyu Gharama za Maisha zimepanda ndio maana Mwendazake alimpigisha MAGOTI
 
Vijana wanaiita kitu ya namna hii " nitoke vipi?"
 
Kwani aliwahi kukiri kuwa vyuma vimekaza?....kama mwenye kumbukumbu anisaidie.

Tofauti na hivyo anyamaze tu.
 
Back
Top Bottom