Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Dah nimejisikia vibaya sana kweli hivi huyu ndio nape yule wa kipindi cha Kampeni nape wa kusukumwa na polisi dah Mungu amjalie sana Nape
Tulia mkuu-karma inatabia ya kukurudishia sawasawa na ulivyotoa.
....ukinisoma kwenye mistari utanielewa.
 
Hakika hotuba fupi aliyoitoa Mh Nape ni ya kishujaa.Hakuna asiyejua mlikoitoa CCM wewe Na Kamanda Kinana.CCM ilikuwa imekufa mkaifufua lakini Leo shukurani yao tumeiona Bravo Nape Bravo Nape wewe ni Shujaa utabaki kuwa Shujaa
 
viongozi wa dini baada ya kutuambia tumuombee sasa hivi wako kimya ila yatawafika tu nao,yataanza kwa gwajima halafu watasema ah huyo achana naye mjeuri huyo halafu yatawafika nao pia kwani hata clouds walitarajia yaliyowafika?
 
Nimemuona Gwajima kwenye sauti ya Nape kuwatukana Usalama wa Taifa Letu. Hii ni hatari kuvunja amani. Usalama wa Taifa tusiwatukane.
 
Kampeni ya kwanza tususie kwenda uwanjani taifa stars ikicheza uwanjani, waende TFF
Msituletee siasa kwenye mpira, pambaneni huko huko hatupendi ujinga.
 
Kwel wew ni son of man [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
Tulishasema kuwa ukimfuga nyoka ukae na rungu sasa nyoka ameanza kuwauma watoto wa jirani wakiisha ataanza kuwauma wa aliye mfuga,ewe mungu tuepushie hiki kikombe
 
RPC anatumika vibaya lakini Anatakiwa kukumbuka cheo ni dhamana
 
Hawana uwezo wa kumfanya lolote nape.si walitumwa leo kwani wamefanya nini mbona nape ameongea sasa
 
Kila siku tunasema humu, wengi mnasubiri mpaka muumizwe ndipo muanze kusema haki haki! Kila siku tunashauri kila mtu asimame kwenye haki, kila mtu apinge uonevu bila kujificha kwenye magwanda ya vyama vyetu.. You don't listen, leo kimemtokea Nape, who would have thought? Kesho kitarudi kwa baadhi ya lunatics ambao bado wanashabikia ujinga ujinga...
 
Nape mdogo wangu, kuikuta CCM inachungulia shimoni haikupi leseni ya kukiuka taratibu za utumishi au kiutawala.

Ulitakiwa ureport kwa Mamlaka yake ya uteuzi na uwaachie. Ulilofanya ni kudhalilisha Rais, Makamu wake pia Waziri mkuu. Ulikuwa na lengo zuri sana ila hukuwa na weledi wa kudeal nalo. RC ulimchukulia kama Paul Makonda na si Mkuu wa Mkoa. Ulikosea Mkuu wangu. Pumzika ufikirie upya.

Ila kauli za CCM ulikuta inachungulia shimoni ukainyanyua naona ndizo zilizokusukuma hata ukafanya uliyoyafanya. Si kweli kama ulinyanyua CCM mdogo wangu bali kuna mchango wako.

Wewe wakati huo hukuaminika mpaka na hawa wanaokupaka uji kwenye lips sasa. Mzee Kinana ndiye mwenye haki ya kunena hayo na si wewe.

Pole dogo. Lakini pia, ulikuwa na motive ya kumuondoa RC ambe pia hakuwa chini yako wewe. Ni kama mtu na mdogo wake. Hukuwahi kuhisi haya maumivu uliyonayo angeyapata kwa move uliyokuwa nayo? Nafahamu unaumia sana. Haya ni maisha tuu. Maisha ni mchakato na kujifunza pia.

Naamini hutorudia kufanya makosa makubwa kama haya eti kwa kuwa tu ulipigania chama. You are wrong mdogo wangu.

Cha mwisho, usichopenda kufanyiwa usimfanyie mtu mwingine Nape. Kazi njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…