Nape: Wafanyabiashara wa fedha za kigeni walioporwa fedha zao wamefutwa machozi

Nape: Wafanyabiashara wa fedha za kigeni walioporwa fedha zao wamefutwa machozi

Legasi kwisha !!

FB_IMG_1679302343671.jpg
 
Kwa lengo gani? Je kwanini wahusika warudishiwe haki yao? Ilikuwa uporaji?

===
Nape akiwa Clouds FM amesema

"Rais Samia Suluhu Hassan katika miaka hii 2 ya uongozi amefanya kazi ya kuwafuta watu machozi na amefanya kazi ya kurudisha furaha na tabasamu kwenye maisha ya watu. "Wale wanasiasa wenzangu waliokimbia nchi machozi yao yamefutwa na na furaha imerudishwa kwao wamerudi nyumbani"

"Wale Wenye mahotel ambao hotel zao zilifungwa kwa sababu ya COVID 19 machozi yao yamefutwa kupitia royal tour. Watalii wamejaa. Wale waliokuwa na magari ya kusafirisha watalii waliokuwa wamepaki Arusha na kwingineko wamefutwa machozi na Rais Samia Suluhu Hassan".

"Wale wafanyabiashara waliokuwa wakiuza fedha za kigeni ambao maduka yao yalifungwa na fedha zao zikachukuliwa machozi yao yamefutwa kwa kurudishiwa fedha zao na kuruhusiwa kufungua maduka tena"

"Kubwa ni kwamba tumefurahishwa na umeendelea kutugusa sana Waziri Nape.


Asante kwa kufika na Tarehe 25 tutakuwa hapa kwenye Kilele cha Malkia wa Nguvu kwa ajili ya kuwapa tuzo akina dada na mama zetu waliosababisha na kufanya vyema katika nyanja mbalimbali".

Kwanza nimshukuru Mungu kwa kilichotokea mwaka 2021 pili nishukuru kwa mama Samia kuwa na roho ya kibinadamu.
 
Dola sasa hivi ni Sh ngapi? Ni 2300 hiyo hiyo,
Shilingi ya Tanzania imeimarika zaidi dhidi ya fedha nyingine za nchi jirani Tangia Magufuli afariki

Mfano hii ni Shilingi ya Kenya iliyokua sh 22 dhidi ya Tz na sasa ni Sh 17
View attachment 2558898


Halafu Mkapa unamfananisha vipi na Magufuli? Mkapa alifanya privatization na kufungua nchi kwa wawekezaji na uchumi ukakua, Magufuli alikuwa anafanya kinyume, kuua mashirika binafsi na kufukuza wawekezaji
WANAOMSHABIKIA MAREHEMU NI MAREHEMU KWENYE UBONGO.HAWANA ABC YA MAMBO YA KIUCHUMI NA HATA YA KISIASA NA KIJAMII
 
Kuna mtu niliwahi kukaa nae Arusha alikua na bureau, alinipa mkasa mzima

Aisee Hio siku walipofungua bureau zilikuja defender na 'vyuma' yaani walichukua pesa zote hata coin haikubaki, na katika askari waliotelekeza amri hii na kupeleka pesa bot wengi walitajirika maana kama unavyotujua wabongo huwezi kunipa maburungutu ya pesa ambayo hayana hesabu nikayafikisha yote

Ila Hawa watu nao walikua wanaibia taifa sana pesa na wengi walikua wanatakatisha sana pesa chafu, kiufupi walijisahau sana jiwe akaamua kuwapiga ambush kiroho mbaya,

Hii nchi watu hawaelewi tu, hakuna watu hawapendi kulipa Kodi kama matajiri, ukishaona mtu ana bilion kadhaa bank asimilia 90 ya hao watu ni janja janja nyingi tu na kuibia serikali mapato

Swala la kuwanyoosha Hawa matajiri waiba Kodi sijawahi kumpinga magufuli japokua nilikua simkubali, ila la kudeal na Hawa wezi wa Kodi hapo Mzee nilimkubali
NJIA ALOTUMIA NI YA KIJAMBAZI
WALIOLENGWA NI KASIKAZINI:WHY
 
Back
Top Bottom