Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Ok, ndo tunataka kama aliuwawa na jeshi ijulikane. Iundwe tume. Ili kila kitu kijulikane. Porojo nyingi haziwezi saidia. Jeshi aliwezi ogopeka. hata wao ni binadamu, na wanachunguzwa. Kama jama zipo watajibu.
Fatilia mauaji ya alie kuwa Rais wa Bukinafaso, Sankara.
Aliuwawa na Mtu wake wa karibu, na baadhi ya waasi. Imepita miaka zaid ya thelathini. Rais aliekuwepo madarakani alie muuwa Sankara, aligoma uchunguzi usifanyike. Lakini baada ya kutoka madarakani, alishitakiwa na kuwekwa hatiani kwa mauwaji ya Rais Sankara zaidi ya miaka 37 iliyopita.
Leo mtapinga, lakini ipo siku haijarishi. Hata kama kuna watu jeshini waliusika ipo siku, itajulikana ukweli.
Tuanze na waliotangulia kabla yake. Wamepotea wengi katika mazingira ya kutatanisha lakini hatukuona nyuzi zenu kutaka tume huru ya uchunguzi!
 
Mimi siamini kuishi kwa hadithi, siamini kuishi kwa kuiga ati tu fulani hakufanya hivi basi tusifanye. Nchi ina uhai na wananchi ndiyo weye uhai. Mabadiliko hutokea. Hatuwezi ishi kwa hadithi ati mbona hiki kilitokea tuendelee hivyo hivyo. La hasha!
Unadai Magufuli kuuwa ati maiti waliokutwa kwenye viroba. Na kumuuwa Ben Saanane. Hivi Chama husika Ben alikuwa msaidizi wa Mbowe. Kwanini Mbowe hakwenda kutoa taarifa polisi kuhusu hayo mauaji kwa kuwa alikuwa na ushahidi. Hivi mtu wako wa karibu auwawe, na unajua nani kamuuwa, unashindwa kweli kuchukua hatua?

Hivi vyote ulivyovisema watu waliokuwa na uhakika wange fungua hata kesi ambazo ni private prosecution.
Hayo yote hayaondoi uhalali wa kuundwa tume ya kuchunguza kifo cha Rais.
Kila kitu kina namna yake na uja wakati muafaka. Marekani kumekuwa na mauaji ya watu weusi. Ikazoeleka. Mhakama zilitoa haki kwa polisi.

Lakini mauaji ya George Floyd yaligeuza kila kitu. Dunia nzima iliungana. Hata wakati wa kutoa maamuzi dhidi ya mtuhumiwa, yalitazama hasira za wananchi. Hatimae kwa mara ya kwanza mambo yalibadilika na huyu Askari kukutwa na makosa ya kuuwa kwa kukusudia.
Pamoja na hayo yote uliyoongea, ipo siku mabadiliko yanakuja Tanzania kuchunguza kunapotokea vifo vya utata vya viongozi wa Taifa.
Pia kwa taarifa yako, haya ndo maisha yangu. Nimezaliwa duniani kwa lengo maalum si kuishi tu kama unavyodhani. Hivyo si masumbuko kwangu bali ndo natimiza nilichoumbiwa kuja hapa duniani.
Umeganda kule kule katika imani kwamba kila kifo kina mkono wa mtu kana kwamba JPM hakustahili kufa.

Uanze kuchunguza kifo chake halafu ukute ni kweli moyo wake ulikuwa na matatizo ya muda mrefu, huoni kama huo ni usumbufu usio na sababu.

Unakuwa umeshajenga hali ya kutowaamini wasaidizi wote wa hayati pasipo sababu ya msingi.

Kila nafsi itaonja mauti ni suala la wakati tu, mimi na wewe tutaondoka juu ya uso wa hii dunia.

Siuoni utata wowote kifo cha JPM ingawa mimi ni mmoja wa wale walioukubali sana uwezo wake wa kufanya kazi na kufanya maamuzi magumu.
 
Wanataka kutuaminisha katika yale tunayoyasikia kwenye audio za mitandaoni, maisha ya chuki na kutafutana ubaya.

Alikuwa ni mtu wa miaka 60 aliyeugua moyo kwa zaidi ya miaka 10 ya uhai wake. Pengine ndio sababu hata akashindwa kusafiri kwenda Ulaya na Marekani, kiafya hakuwa imara kama kauli zake na maamuzi yake yalivyokuwa.
 
Ok, nami nimeelewa toka mwanzo ni watu wanamna gani wanao pinga uchunguzi kwa visingizio vya nafsi zao. Nikakumbuka usemi wa wahenga. "Mbaazi akikoswa maua usingizia jua". Asante!
Nani kapinga uchunguzi usifanyike yaani.. We chunguza tu. Samia ye keshasema ni tatizo la moyo.
 
Umeganda kule kule katika imani kwamba kila kifo kina mkono wa mtu kana kwamba JPM hakustahili kufa.

Uanze kuchunguza kifo chake halafu ukute ni kweli moyo wake ulikuwa na matatizo ya muda mrefu, huoni kama huo ni usumbufu usio na sababu.

Unakuwa umeshajenga hali ya kutowaamini wasaidizi wote wa hayati pasipo sababu ya msingi.

Kila nafsi itaonja mauti ni suala la wakati tu, mimi na wewe tutaondoka juu ya uso wa hii dunia.

Siuoni utata wowote kifo cha JPM ingawa mimi ni mmoja wa wale walioukubali sana uwezo wake wa kufanya kazi na kufanya maamuzi magumu.
Laumu walio weka sheria ya kuchunguza kifo na hasa kunapokuwepo na utata. Mtu kuumwa au kuwa na shida fulani akafa, na ukawepo utata. Uchunguzi ufanyika na sheria inaruhusu. Uchunguzi ufanyika kuondoa utata.
hadithi kuwa kulikuwa na hiki hayo ni yako.
Mauaji mangapi yametokea hospitalini au kwingineko lakini baada ya uchunguzi mambo uwekwa wazi.
Wewe kinakuuma nini uchunguzi kufanyika kwa alie kuwa Rais wa nchi. Unaanza leta visingizio ambavyo havina msingi.
Hapa hatuko kiushabiki, kikubwa uchunguzi ufanyike ili iwe wazi.
 
Mimi siamini kuishi kwa hadithi, siamini kuishi kwa kuiga ati tu fulani hakufanya hivi basi tusifanye. Nchi ina uhai na wananchi ndiyo weye uhai. Mabadiliko hutokea. Hatuwezi ishi kwa hadithi ati mbona hiki kilitokea tuendelee hivyo hivyo. La hasha!
Unadai Magufuli kuuwa ati maiti waliokutwa kwenye viroba. Na kumuuwa Ben Saanane. Hivi Chama husika Ben alikuwa msaidizi wa Mbowe. Kwanini Mbowe hakwenda kutoa taarifa polisi kuhusu hayo mauaji kwa kuwa alikuwa na ushahidi. Hivi mtu wako wa karibu auwawe, na unajua nani kamuuwa, unashindwa kweli kuchukua hatua?

Hivi vyote ulivyovisema watu waliokuwa na uhakika wange fungua hata kesi ambazo ni private prosecution.
Hayo yote hayaondoi uhalali wa kuundwa tume ya kuchunguza kifo cha Rais.
Kila kitu kina namna yake na uja wakati muafaka. Marekani kumekuwa na mauaji ya watu weusi. Ikazoeleka. Mhakama zilitoa haki kwa polisi.

Lakini mauaji ya George Floyd yaligeuza kila kitu. Dunia nzima iliungana. Hata wakati wa kutoa maamuzi dhidi ya mtuhumiwa, yalitazama hasira za wananchi. Hatimae kwa mara ya kwanza mambo yalibadilika na huyu Askari kukutwa na makosa ya kuuwa kwa kukusudia.
Pamoja na hayo yote uliyoongea, ipo siku mabadiliko yanakuja Tanzania kuchunguza kunapotokea vifo vya utata vya viongozi wa Taifa.
Pia kwa taarifa yako, haya ndo maisha yangu. Nimezaliwa duniani kwa lengo maalum si kuishi tu kama unavyodhani. Hivyo si masumbuko kwangu bali ndo natimiza nilichoumbiwa kuja hapa duniani.
JPM pia ana ndugu, ana mke na watoto, wewe ni nani wa kuipigania haki yake zaidi ya ndugu na watoto!!?? Una uhakika gani kama mke, ndugu na watoto hawajajiridhisha!!?? Unataka kutuambia umeumia zaidi ya mke na wanae!? Au we ndo Mama Jesca?
 
Laumu walio weka sheria ya kuchunguza kifo na hasa kunapokuwepo na utata. Mtu kuumwa au kuwa na shida fulani akafa, na ukawepo utata. Uchunguzi ufanyika na sheria inaruhusu. Uchunguzi ufanyika kuondoa utata.
hadithi kuwa kulikuwa na hiki hayo ni yako.
Mauaji mangapi yametokea hospitalini au kwingineko lakini baada ya uchunguzi mambo uwekwa wazi.
Wewe kinakuuma nini uchunguzi kufanyika kwa alie kuwa Rais wa nchi. Unaanza leta visingizio ambavyo havina msingi.
Hapa hatuko kiushabiki, kikubwa uchunguzi ufanyike ili iwe wazi.
Kafanya uchunguzi basi.
 
Hakiniumi kitu uchunguzi kufanyika. Naona ni upotezaji wa muda na rasilimali pesa ambazo ni za walipa kodi.

Ameshaondoka JPM, ameshaingia katika vitabu vya historia, Mheshimiwa Rais pale bungeni alishaweka wazi yoyote mwenye ushahidi wa mchezo mbaya na auweke wazi ili mbivu na mbichi zijulikane.

Afya ya rais ni suala zito, na hayati siku zote alikuwa akitembea na daktari kwenye msafara wake. Naona kama ni upotezaji wa muda kutokukubaliana na taarifa rasmi za serikali.
 
Nani kapinga uchunguzi usifanyike yaani.. We chunguza tu. Samia ye keshasema ni tatizo la moyo.
sihusiki katika uchunguzi, serikali iliyoko madarakani ndo wahusika. Hivyo mama Samia alie sema Rais hajambo, na anatusalimia. Na akasema mafua mafua ni kawaida kwa binadamu. Baadae akatwambia Magufuli kafa kwa matatizo ya moyo. Huyu huyu anatakiwa aunde tume ichunguze chanzo cha kifo. Tuondoe utata.
Yeye alikuwa makamu wa Rais, hivi Rais ataumwa yeye asijue? Kwanini alituambia yupo na anatusalimia. Wakati taarifa zinasema alikuwa kalazwa Mzena Hospital.
Je Makamu wa Rais mama Samia haoni kuwa alidanganya Taifa? kuwa Rais yupo anatusalimia kumbe amelazwa anaumwa. Kwanini akuliambia Taifa ukweli kuwa Rais anaumwa kalazwa.
Hii inaleta hisia kuwa Rais hataki kuunda tume huru kuchunguza kifo kwani hata yeye alidanganya wananchi kuhusu kuumwa kwa Rais.
 
JPM pia ana ndugu, ana mke na watoto, wewe ni nani wa kuipigania haki yake zaidi ya ndugu na watoto!!?? Una uhakika gani kama mke, ndugu na watoto hawajajiridhisha!!?? Unataka kutuambia umeumia zaidi ya mke na wanae!? Au we ndo Mama Jesca?
Huyo ni mmoja wa jamaa zangu waliomkubali sana JPM, wanashindwa kukubaliana na ukweli kwamba mpendwa wetu ameshakuwa sehemu ya historia.

Ni maziwa, milima na miti ndio itakayobakia milele, viumbe wengine wote uhai wetu ni mfupi sana.
 
Habar watanzania lengo langu la kuanzisha huu uzi si kwa Nia Mbaya ila nikutaka tu Kumaliza Maswali ya Watanzania wengi wanao shuku kua Hayat kafanyiwa hujuma.

Baada ya kuona mambo mengi Yanayo endelea kwenye mitandao ya kijamii na mitaani. ni wazi kabisa Baadh ya watanzania walio wengi Wana shuku kifo cha Hayat Magufuli na kudhan kua kifo chake kina Hujuma.

Serikal iheshimu mawazo ya watanzania tunao tilia shaka kifo cha Rais wetu na izingatie kwa kuunda Tume huru ya uchunguzi.

Mimi Binafsi nikikumbuka Tukio la ule Moshi uliomfata Hayat Magufuli Mtwara alipokua kwenye Gari bila kujulikana wapi umetokea na kuzua Taharuki nazid kua na mashaka kua Huenda zile zilikua baadhi ya mbinu za kutaka kujaribu na zilishindwa Lakini waliojaribu hawakuacha.

Huwezi kusema ule ulikua uchawi sababu hakuna uchawi na wala siamini uchawi kama upo.

Sasa ili kujiridhisha Basi serikal ifanye uchunguzi na uchunguzi uwe wa wazi ili kufuta hii shauku ya Baadhi ya watu kwani ikiendelea ivi na serikal kukaa kimia huwezi jua Baadaye itakua na madhara gani pia huto jua maadui baadae wanaweza kuutumia huu uvumi kama silaha so nibora serikal ilimalize kwanza ili swala kwani kila siku mambo yanazid kupamba moto.

Video ya tukio la moshi hio apo chini.

Naunga mkono hoja.
Ili kuondoa uvumi na kuwaridhisha pande zote. Wafanye kama kwa Sabaya
 
sihusiki katika uchunguzi, serikali iliyoko madarakani ndo wahusika. Hivyo mama Samia alie sema rahisi hajambo, na anatusalimia. Na akasema mafua mafua ni kawaida kwa binadamu. Baadae akatwambia Magufuli kafa kwa matatizo ya moyo. Huyu huyu anatakiwa aunde tume ichunguze chanzo cha kifo. Tuondoe utata.
Yeye alikuwa makamu wa Rais, hivi Rais ataumwa yeye asijue? Kwanini alituambia yupo na anatusalimia. Wakati taarifa zinasema alikuwa kalazwa Mziku Hospital.
Je Makamu wa Rais mama Samia aoni kuwa alidanganya Taifa? kuwa Rais yupo anatusalimia kumbe amelazwa anaumwa. Kwanini akuliambia Taifa ukweli kuwa Rais anaumwa kalazwa.
Hii inaleta hisia kuwa Rais hataki kuunda tume huru kuchunguza kifo kwani hata yeye alidanganya wananchi kuhusu kuumwa kwa Rais.
Mama Samia kistaarabu tu alituambia kuwa rais anaumwa, asingeweza kutueleza kwa kina hali aliyokuwa nayo kiafya.

Kuna masuala mengine huwezi kuambiwa kama yalivyo, unajiongeza kiakili na kujua nini kinaendelea, ndio maana ya neno diplomasia.

Huwezi kumhukumu Rais kwa sasa eti kwa kauli aliyotoa juu ya afya ya hayati. Wewe hujawahi kuongea leo usiku na mgonjwa akiwa hospitalini mkawa mnacheka halafu kesho asubuhi ukaambiwa kuwa amefariki muda mchache baada ya maongezi yenu kumalizika?.

Uhai wetu ni zawadi kutoka kwa Mungu, hatujui lini utafika mwisho.
 
Hakiniumi kitu uchunguzi kufanyika. Naona ni upotezaji wa muda na rasilimali pesa ambazo ni za walipa kodi.

Ameshaondoka JPM, ameshaingia katika vitabu vya historia, Mheshimiwa Rais pale bungeni alishaweka wazi yoyote mwenye ushahidi wa mchezo mbaya na auweke wazi ili mbivu na mbichi zijulikane.

Afya ya rais ni suala zito, na hayati siku zote alikuwa akitembea na daktari kwenye msafara wake. Naona kama ni upotezaji wa muda kutokukubaliana na taarifa rasmi za serikali.
Usiseme afya ya rais si suala zito. Unajua katiba inasema nini juu ya afya ya Rais. hata Tundu Lissu na Mnyika walihoji kwa mujibu wa katiba afya ya Rais inapokuwa tata. Nni ufanyika. Mama Samia anakwepa swala la kusema kupeleka ushahidi, uwezi peleka ushahidi bila kuwepo kwa tume huru. Huo ushahidi utapeleka wapi? Unataka mwenye ushahidi maisha yake yawe hatarini?
Yeye aunde Tume aone kama ushahidi haujapelekwa. Tuache vijimaneno vya kuremba na vilivyojaa hira za udanganyifu.
 
Kama wanashindwa kuamini kauli ya Rais Samia Hassan, watawezaje kuamini majibu/matokeo ya hiyo tume unayoipendekeza?
Majority ya watanzania Wanaamini JPM aliuawa. Sema hakuna solid evidence na kwa kuwa wenye mamlaka walisema cause of death ni Chronic atrial fibrillation, basi kwa Sasa tuishi nalo hilo lakini Wakati ni mwalimu na aliyeua kwa upanga sharti afe kwa Upanga.
 
Mama Samia kistaarabu tu alituambia kuwa rais anaumwa, asingeweza kutueleza kwa kina hali aliyokuwa nayo kiafya.

Kuna masuala mengine huwezi kuambiwa kama yalivyo, unajiongeza kiakili na kujua nini kinaendelea, ndio maana ya neno diplomasia.

Huwezi kumhukumu Rais kwa sasa eti kwa kauli aliyotoa juu ya afya ya hayati. Wewe hujawahi kuongea leo usiku na mgonjwa akiwa hospitalini mkawa mnacheka halafu kesho asubuhi ukaambiwa kuwa amefariki muda mchache baada ya maongezi yenu kumalizika?.

Uhai wetu ni zawadi kutoka kwa Mungu, hatujui lini utafika mwisho.
mama samia hakusema kuwa Rais anaumwa. Alisema rais hajambo na anawasalimia. Baadae aliongea kauli kuwa mafua mafua ni kawaida kwa binadamu. Hakusema huyo mwenye mafua ni nani? usipotoshe. Afya ya Rais ni jambo la wazi. kikwete tulielezwa hadi alichoumwa alipoenda kutibiwa.
Nyerere Rais msitaafu tulielezwa kila hatua.
Siongei kiushabiki hapa naongea kwa maslahi mapana ya Taifa. tuache ubabaishaji.
 
Majority ya watanzania Wanaamini JPM aliuawa. Sema hakuna solid evidence na kwa kuwa wenye mamlaka walisema cause of death ni Chronic atrial fibrillation, basi kwa Sasa tuishi nalo hilo lakini Wakati ni mwalimu na aliyeua kwa upanga sharti afe kwa Upanga.
Kazia hapo "aliyeua kwa upanga sharti afe kwa Upanga"
 
usiseme afya ya rais si suala zito. Unajua katika inasema nini juu ya afya ya Rais. hata tundu Lissu na Mnyika walihoji kwa mujibu wa katiba afya ya Rais inapokuwa tata. Nni ufanyika. Mama Samia anakwepa swala la kusema kupeleka ushahidi, uwezi peleka ushahidi bila kuwepo kwa tume huru. Huo ushahidi utapeleka wapi? Unataka mwenye ushahidi maisha yake yawe hatarini?
Yeye aunde Tume aone kama ushahidi haujapelekwa. Tuache vijimaneno vya kuremba na vilivyojaa hira za udanganyifu.
Huyu sio kiongozi wa kwanza afrika kufa akiwa madarakani. Isiwe nongwa kifo chake wakati tumeshatangaziwa nini haswa kimetokea.

Umeshindwa kwenda Mzena Hospital ukapewa taarifa na madaktari waliomhudumia mpaka akakata roho?. Umeshafanya jitihada za kumtafuta daktari wake aliyekuwa karibu nae kwa muda wote wa urais wake?.

Umeshafanya upelelezi binafsi kujua kama alikuwa hanywi pombe licha ya kuwa na matatizo ya umeme wa moyo?.

Usiwe mwepesi wa kumnyooshea Rais wa sasa kidole bila ya kufanya kazi ya kufikiria mengi kwa kina.
 
Back
Top Bottom