Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

Binafsi napenda sana mfumo huu unaonesha gar n la lini.
Swala la kuuza mie naona hali ya gari ndio ifanya kiuzwe kwa bei gan na si namba japo namba nayo inamchango wake

Mfumo hauoneshi gari ni la lini bali limeingia nchini na kupewa usajili wa wakati fulani...
 
FRANCIS DA DON wazo lako ni zuri lakini inaondoa dhana ya mfumo wa biashara huria...

Ni bidhaa chache ambazo zimewekewa udhibiti wa mamlaka fulani, na bidhaa hizo ni zile zenye maslahi kwa serikali...

Lakini bidhaa kama uuzwaji wa magari, ni sawa tu na mtu anayeuza papai zake toka Maneromango au maembe yake toka Bagamoyo, kila mtu anajipangia bei yake...
 
Ngoja nimalizie bia kwanza, au basi, nitakujibu asubuhi
 
Is there any known Car Restoration Facility? Ukiacha hawa Makanjanja wa Makumbusho.
 
Mfumo unaoupendekeza OP, hauna tija kabisa zaidi ya kuwanufaisha Madalali wa Magari.

Nowadays kuna TBS. Ukitamka tu TBS mbele ya Dalali wa Magari utaona uso wake utakavyoChange ghafla.

Tunaelekea mbele na sio nyuma. Think Big. [emoji594]
 
Is there any known Car Restoration Facility? Ukiacha hawa Makanjanja wa Makumbusho.
Nani aanzishe facility kama hiyo ale hasara? , labda waanzishe randomized plate numbers
 
Nani aanzishe facility kama hiyo ale hasara? , labda waanzishe randomized plate numbers
Yaani Jombi wewe na hii inshu ya 'Randomised Number Plates' umeivalia Kibwebwe utadhania ni Katiba Mpya!?

Deep down inside of you, know that nothing good will come out of this.

Wishing you best of luck.
 
Maelezo yamejitosheleza kazi kwa wizara ya fedha kushughulikia hili
 
Binafsi napenda sana mfumo huu unaonesha gar n la lini.
Swala la kuuza mie naona hali ya gari ndio ifanya kiuzwe kwa bei gan na si namba japo namba nayo inamchango wake
Namba E mbona ilishafika mamia. Ilishaanza muda.
 
Mfumo unaoupendekeza una faida kwako wewe unayetaka kuuza gari lako ambalo pengine na wewe ulilinunua kutoka hukohuko Japan.

Baada ya kulitumia kwa muda kadhaa sasa unaona wenzio wanaoagiza magari kutoka Japan wasiagize wanunue lakwako. Ili kufanikisha hilo unatamani hata utaratibu wa plate number ubadilishwe ili ukunufaishe wewe.

Hapa Chief unaonesha kujipendelea wewe zaidi kuliko manufaa ya nchi.

Nadhani serikali inapata mapato makubwa zaidi ya kodi kwa magari yanayoagizwa kutoka nje kuliko kodi za kubadili umiliki kwa kuuziana ndani ya nchi.

Utaratibu huu wa plate number uendelee tu, unasaidia angalau kujua chombo cha moto kina muda gani tangu kisajiliwe nchini bila kijali umekifanyia matengenezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…